Waziri Masauni: NIDA kuna shida ya usimamizi, Uongozi una shida, Watu wanateseka kupata Vitambulisho

Waziri Masauni: NIDA kuna shida ya usimamizi, Uongozi una shida, Watu wanateseka kupata Vitambulisho

Pole sana.

Nadhani NIDA ipo Top 5 ya mamlaka za serikali zinazokera zaidi nchini Tanzania.

Mi nilipata shida sana haya kuandikishwa tu na kupigwa picha.

Unapoteza siku nzima, tunafika unaambiwa kaanzie kwa Sijui nani nani huko..

Nilipopata namba nikatemana nao, nikatafuta Maza mmoja kijumbe wa CCM nikampa 20k afuatilie huko ofisi yao ya kata, kikitoka aniletee.
Taasisi nyingine?
 

Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mhandisi Hamad Masauni amelazimika kutoka Ofisini na kufuatilia utendaji wa Mamlaka ya Vitambulisho vya Taifa (NIDA) ambapo mamlaka hiyo imekuwa ikilalamikiwa na Wananchi kwa utendaji na utoaji wa Vitambulisho usioridhisha.

Waziri Masauni amefika katika Ofisi ya NIDA iliyopo Manispaa ya Ubungo na kukuta zaidi ya Wananchi 100 wakiwemo Wanafunzi waliohitimu Kidato cha Sita, hivi karibuni waliopo katika mchakato wa kuomba mkopo wa Elimu ya Juu wanatakiwa kuwa na Kitambulisho cha Taifa wakiwa hawapati huduma wanayostahili.

Pia soma;

KERO - Ugawaji wa NIDA wilaya ya Busega unasuasua zaidi ya mwezi. Wanafunzi tunaotegemea namba kuomba mkopo HESLB hatarini kukwama
Lete solution siyo waziri nae analalamika.
 
Hiyo Nida kawe ndio utalia , miongoni mwa ofisi za serikali zina unyanyasaji wa kutisha ni pale , watu wanafokewa kama watoto
Kupata huduma sasa mtihani kabisa kupoteza masiku na masiku kawaida ila utaambulia masimango kama unaenda kuomba hela,
Wazee inauma sana hamjui tu
Jamani Watanzania wenzetu mliopata dhamana ya kutusaidia ,tusaidieni wenzenu

Maisha yametupiga hata nyie mtupige? NIDA BADILIKENI BADILIKENI
Muundo wake ndiyo chanzo cha matatizo + Wizara mama ndiyo imeoza haswa
 
Kwa hiyo mnaendelea kucheka na nyani!!
Haiwezekani kutolewa kitambulisho ichukue mwaka na zaidi hizo computer kazi zake ni nini!?
Ilitakiwa hiyo ofisi kufukuza wote kuanzia waziri hadi mfagiaji na mleta Chai.
Huu ni uzembe wa Hali ya juu!.
Nilipoteza kitambulisho wameniambia kupata hadi miez 5 ipite.nawakati nina dokoment zote.nida ni uchafu watumish wake wafagiliwe wote
 
Bila kutoa Hongo hupati kitambulisho cha Uraia cha NIDA.
 
Back
Top Bottom