Roving Journalist
JF Roving Journalist
- Apr 18, 2017
- 3,984
- 13,760
Waziri Masauni: Tendo la ndoa sio haki ya msingi kwa Wafungwa
Waziri wa Mambo ya Ndani Hamad Yussuf Masauni amesema mchakato wa haki ya faragha kwa wafungwa kukutana na wenza wao utaanza kutolewa pale ambapo mifumo ya kisheria na miundombinu ya magereza itakapokidhi kutolewa kwa haki hiyo.
Amesema pamoja na hivyo suala la tendo la ndoa ni haki ya mfungwa lakini si haki ya msingi, kwa kuwa haki za msingi ni chakula, mavazi na malazi.
Waziri Masauni amesema “Itakapofika muda wa kuanza mchakato huo tutazingatia mila, usalama, desturi za Watanzania, wakati wmingine siyo jambo zuri kila mtu kujua hawa wanaenda kufanya tendo la ndoa.”