Ushirombo, Heshima mbele,
Kwa hiyo unataka kumfananisha Masha na Obama? Hivi Masha alishawahi hata kushiriki katika kazi na uongozi wa Kijamii zaidi ya kuwa na law firm yenye Ukungu wa EPA? Ninadiriki kusema Masha hana uzoefu wa kuongoza umma,
Naomba kutokukubaliana
Ushirombo, Heshima mbele,
Kwa hiyo unataka kumfananisha Masha na Obama? Hivi Masha alishawahi hata kushiriki katika kazi na uongozi wa Kijamii zaidi ya kuwa na law firm yenye Ukungu wa EPA? Ninadiriki kusema Masha hana uzoefu wa kuongoza umma,
Naomba kutokukubaliana
Ndiyo mana huwa simpendi Mengi na nitasimamia hapo hapo...Mzee huyu anajidai ni msaada kwa watanzania ila hana chochote
Ndiyo mana huwa simpendi Mengi na nitasimamia hapo hapo...Mzee huyu anajidai ni msaada kwa watanzania ila hana chochote
Kwa swala la kusimamia hapo hapo nakemea kwa JINA LA YESU ubadilike na uwe na upendo kwa wenzako: kwa swala la kuwa msaada kwa watanzania inamaana wewe huoni msaada unaotolewa na Mengi?? Hivi wewe ulishawahi kufuatwa ukaambiwa unadaiwa bills kwa kuangalia Television stations zake?? Je angefuata mfumo wa GTV na DSTV wanyonge wangeweza kujua nini kinaendelea nchini mwao na hata duniani kote?? watu wanaangalia aljazeera na cnn bure through ITV ukienda GTV au DSTV ni pesa ambayo mnyonge hawezi kuimudu sasa huu si msaada tosha??
GEMBE usifiche hekima yako ficha upumbavu wako mkuu
Ushirombo, Heshima mbele,
Kwa hiyo unataka kumfananisha Masha na Obama? Hivi Masha alishawahi hata kushiriki katika kazi na uongozi wa Kijamii zaidi ya kuwa na law firm yenye Ukungu wa EPA? Ninadiriki kusema Masha hana uzoefu wa kuongoza umma,
Naomba kutokukubaliana
Naam hapa siongezi kitu maana umesema yote!!!!!!
Mkuu Waga msamehe tu bwana Gembe , naamini ameteleza katika kutoa lile lililo moyoni mwake na kulianika ili dunia nzima ijue.Sisi wengine tushamsamehe na tunaamini si msimamo unaoweza kumsaidia wala kumpevusha kimawazo.Hapa JF kunakuelimishana,kupashana, kuyooshana na hatimaye kama mchango ni mswano kabisa kupongezana kwa faida ya wengine wote.Unajua kuna wakulu wengine wanaamuaga kukurupuka kuandika mambo mengine ambayo hayana msingi sijui ili waweze kuongeza idadi ya post zao?? Hapa tunahitaji kuitetea jamii na kujitahidi kuwaelekeza hawa wenzetu ambao ni viongozi waweze kuiweka nchi kwenye mstari ulionyooka si mahala pa kuja kusema mauza uza yako kuwa simpendi huyu nampenda huyu inatusaidia nini sisi?? mwaga points za maana watu tutakuwa na wewe ukurasa mmoja lakini si kubwabwaja tu pasipo na sababu za msingi
Sidhani kama Ushirombo alimaanisha kumfananisha Obama na Masha bali nadhani pointi yake ilikuwa ni hoja kuwa vijana hawafai kwasababu ya Masha haina mantiki...Kuna vijana wengi sana tu wenye hekima na busara na wenye kufanya maamuzi inavyotakiwa.
Naomba uelewe pia kuwa nafasi hiyo wa uwaziri wa mambo ya ndani aliteuliwa na hakuchaguliwa,similarity moja na Obama ni kwamba wote walichaguliwa kutoka majmboni mwao kuingia bungeni/senete,ila kwenye uongozi wao wa serikali ni tofauti sana mmoja ni rais aliyechaguliwa na wananchi na mwingine ni waziri wa mambo ya ndani aliyeteuliwa na rais.
Ndugu yangu kumdhuru kivipi? Yani akitokea mtu mwenye msimamo dhidi ya haki za wananchi kutozingatiwa basi yeye ndiyo wenye uwezo wa kumdhuru mwezie? Nani alikuwa amdhuru nani? Nadhani madhara uliyoyazungumzia inawezekana(correct me if iam wrong) ni ya kisiasa ama kisheria,ila madai kuwa mchagga Mengi si rahisi kumdhuru Masha kwasababu kaoa uchaggani....
Then kwanini hukuangalia upande wa pili wa shilingi na kusema Masha hawezi kumdhuru Mengi kwasababu kaoa uchaggani? Kwanini hukusema Masha ama mke wake watapita wapi kama wakimfilisi Mengi kwa njama?
Naelewa umekuwa dissapointed mkuu lakini still naomba ubalance ili kuweza kuleta mantiki ya haki na sense kimjadala bila unnecessary biasiness.
Nipashe Leo
Masha abwaga manyanga kwa Mengi
Yeye ndiyo Waziri aliyesema jambo; na yeye mwenyewe kalifuta. Yote mawili yako ndani ya uwezo wake. Sasa, kujaribu kuonesha kuwa kwa vile jambo ambalo yeye alilisema baadaye kaona kuwa hakuna ulazima wa kulitekeleza katika piramidi ya vitu vya muhimu kwake siyo kumtendea haki.
Nadhani tumekubali mwanzoni alisema maneno ambayo hayakuwa na hekima sana na yalikuwa ya kusetup yeye mwenyewe; lakini pia tukubali kuwa hekima imeshinda. Japo kwa wengine wangependa kuona hiyo showdown kati ya mwanasiasa mfanyabiashara, na mfanyabiashara mpenda siasa..
Kama ni mpira, timu zote hazikufia uwanjani; mashabiki rudini majumbani kwenu.
Nafikiri kabla hujakurupuka na hii nyepesi, ulitakiwa kujiuliza kwanza nani aliyejitokeza to the public kwanza, kabla ya mwingine, au? Maana nitasema je kua Masha atamdhuru Mengi wakati aliyeanza kushitaki kwetu public ni Mengi?
- Mkulu wangu Mushi vipi leo mbona nilishaanza kukuaminia, hivi unajua toka nimuoe mke wangu sijawahi kufika kwao na ninaendelea na maisha kama kawa na huenda nisije kufika kabisa huko kwao, sasa eti unasema kuwa Mengi anaweza ku-afford kukosa kwenda kwao kwa sababu ya Masha na this nonesense? Vipi ndugu yangu yaani umeshindwa hata kuona ishus muhimu za taifa kwenye this sagga kama kutoheshimika kwa sheria na wenye nguvu wawili wasiojua mipaka ya nguvu zao!
- What a joke! nimekua dissappointed off course yes kwa sababu nilitegemea this drama itaenda kwenye sheria ili kuweka muongozo wa sheria kwa the future generation kuhusu mipaka ya utanuaji kwa viongozi na matajiri katika taifa letu, sihitaji balance kwenye kuwa na haya mawazo, na ninaamini betweeen maneno yangu na yako hapa kwenye this thread sio taabu ku-read betweeen the lines hoja za nani kati yangu na wewe zina matatizo ya balance na bias.
Have a nice day mkuu, next time jifunze kusoma betweeen the lines kinachosemwa, kabla ya kukurupuka!
Naomba uweke msisitizo kwenye neno ulilotumia "Kumdhuru" Kuhusu public wewe ulisema uchaggani...
-Mengi hawezi kumuharibia Masha kisiasa na ndio sababu mpaka sasa hajataja jina la huyo waziri, tulioliwa hapa ni wananchi maana hii ni a missed opportunity ya kusimamia utawala wa kisheria, watu wawili wenye nguvu za ajabu in our society wasiojua mipaka ya nguvu zao na kuishia kutusumbua wananchi bure.
Nadhani pia kutokana na previous statement zako...Masha naye hawezi kumwaribia Mengi na ndiyo maana nikauliza vipi siku saba? Ungesema wote hawawezi kuharibiana ningekuelewa zaidi.
- By the way, mbona wakiguswa Mrema, na Mengi unakuwa mkali sana bwana Mushi? au? Bwa! ha! ha! ha!
Sijui kwanini umemmention Mrema along side Mengi kwenye watu "wawili" ninaonekana kuwa "mkali" kama wakiguswa,sijui..Labda kwasababu wote ni wachagga,nadhani utakuwa happy.
Uzuri hapa ni kwamba hata kama unamtetea mtu ndugu Field Marshall ni lazima uwe na pointi za ku back up na si tu kuwa mnazi...Mimi si mnazi,ni mchambuzi tu na kwa uhakika nitakuwa upande wa wazalendo regardless kuwa ni wakristo,waislam ama wachagga.