Waziri Mavunde Awataka Watanzania Kuchangamkia Manunuzi ya Bidhaa ya Trilioni 3.1 Migodini

Waziri Mavunde Awataka Watanzania Kuchangamkia Manunuzi ya Bidhaa ya Trilioni 3.1 Migodini

Stephano Mgendanyi

JF-Expert Member
Joined
May 16, 2020
Posts
2,833
Reaction score
1,301

WAZIRI MAVUNDE AWATAKA WATANZANIA KUCHANGAMKIA MANUNUZI YA BIDHAA YA TRILIONI 3.1 MIGODINI

-Azindua rasmi Chama cha Watoa Huduma na Wauzaji wa Bidhaa Migodini

-Afurahishwa na Watanzania kuzingatia ubora

-Awataka kushirikiana na kusaidiana

-Rais Samia apongezwa kuvutia uwekezaji

Dar es salaam

Waziri wa Madini Mh. Anthony Mavunde amewataka watanzania wanaoshiriki kwenye mnyororo wa thamani wa sekta ya madini kuchangamkia fursa kubwa iliyopo ya manunuzi ya bidhaa na utoaji huduma migodini ambayo kwa mwaka wa fedha 2023/24 jumla ya kiasi cha Tsh Trilioni 3.1 zimetumika katika eneo la manunuzi ya bidhaa na huduma.

Waziri Mavunde ameyasema hayo jana Jijini Dar es salaam wakati wa hafla ya uzinduzi wa Chama cha Watoa Huduma na Wasambazaji wa bidhaa Migodini (TAMISA).

“Uwekezaji nchini Tanzania kwenye sekta ya madini unakua siku hadi siku na hii inatokana na mazingira mazuri ya uwekezaji yaliyowekwa na serikali chini ya uongozi wa Mh. Rais Dkt. Samia S. Hassan.

Chama hichi kitasaidia kuwa na sauti ya pamoja katika kuwajengea uwezo watanzania na kuwaimarisha ili kuwa shindani katika utoaji wa huduma na usambazaji wa bidhaa migodini.

Natamani sana kuziona hizi Trilioni 3.1 zinabaki mikononi mwa watanzania ili kuchochea uchumi wa nchi yetu kwa kuanzisha viwanda vya kuzalisha bidhaa na huduma zenye mahitaji makubwa migodini.

Nawapongeza sana TAMISA kwa kupokea na kuyafanyia kazi maagizo yangu ya uanzishwaji wa chama hichi cha watoa huduma na wasambazaji wa bidhaa migodini,ni mategemeo yangu kwamba mtakuwa jukwaa zurila mafanikio ya sekta binafsi Tanzania”Alisema Mavunde

Akitoa maelezo ya awali,Mwenyekiti wa TAMISA Ndg. Peter Kumalilwa amesema chama hichi kina malengo mahsusi ya kuwaleta pamoja watoa huduma na wasambazaji wa bidhaa migodini,kuishauri serikali namna bora ya kuwajengea uwezo watanzania kunufaika na sekta ya madini na kushirikiana na serikali kutatua matatizo ya msingi kwenye suala la Local content.

Akitoa salamu za sekta binafsi,Mjumbe wa Bodi ya wakurugenzi TPSF ; Na Mwenyekiti wa Kongani ya Huduma ( Service Cluster) Ndg. Octavian Mshiu amepongeza hatua ambazo serikali inazichukua kwa sasa kuvutia uwekezaji na kukuza sekta binafsi nchini na kuahidi kwamba TPSF itakuwa bega kwa bega na wadau wote kuhakikisha watanzania wanachangamkia uchumi wa madini
 

Attachments

  • WhatsApp Image 2024-09-14 at 11.04.52.jpeg
    WhatsApp Image 2024-09-14 at 11.04.52.jpeg
    93.3 KB · Views: 3
  • WhatsApp Image 2024-09-14 at 11.04.54.jpeg
    WhatsApp Image 2024-09-14 at 11.04.54.jpeg
    134.7 KB · Views: 3
  • WhatsApp Image 2024-09-14 at 11.04.54(1).jpeg
    WhatsApp Image 2024-09-14 at 11.04.54(1).jpeg
    127.7 KB · Views: 3
  • WhatsApp Image 2024-09-14 at 11.04.55.jpeg
    WhatsApp Image 2024-09-14 at 11.04.55.jpeg
    150.3 KB · Views: 3
  • WhatsApp Image 2024-09-14 at 11.04.55(1).jpeg
    WhatsApp Image 2024-09-14 at 11.04.55(1).jpeg
    101.3 KB · Views: 3
  • WhatsApp Image 2024-09-14 at 11.04.56.jpeg
    WhatsApp Image 2024-09-14 at 11.04.56.jpeg
    118 KB · Views: 3
  • WhatsApp Image 2024-09-14 at 11.04.56(1).jpeg
    WhatsApp Image 2024-09-14 at 11.04.56(1).jpeg
    123.9 KB · Views: 3
  • WhatsApp Image 2024-09-14 at 11.04.57.jpeg
    WhatsApp Image 2024-09-14 at 11.04.57.jpeg
    128.5 KB · Views: 3
  • WhatsApp Image 2024-09-14 at 11.04.57(1).jpeg
    WhatsApp Image 2024-09-14 at 11.04.57(1).jpeg
    149 KB · Views: 3
  • WhatsApp Image 2024-09-14 at 11.04.58.jpeg
    WhatsApp Image 2024-09-14 at 11.04.58.jpeg
    135.8 KB · Views: 2
Hizi naona tu kama ni red tapes na ukiritimba..., hapo issue si ni suppliers wa migodini kuanzia chakula peni hadi mavitu yote...., kwenye hio usishangae kinachoangaliwa ni utatoa kiasi gani au kulainisha kiasi gani ili upewe tenda, na wengi hapo ni wachuuzi wanachukua mtaani wanaongeza cha kwao na cha wanaotoa tenda na kubaki na chenji...

Kwa Wananchi kunufaika na madini haya mikataba ingekuwa mizuri ya sisi kupata asilimia za kutosha sio kushangilia hizi tenda ambazo kupata shavu lazima utoe kitu kidogo....; Tungechukua template ya mikata angalau ya Botswana huenda tusingehangaika kukatana matozo kitaa (migodi ingechangia tosha mambo yote haya)...

We need to aim for the moon hata tuki miss angalau tutapata stars as of now hata mawingu hatupati....
 
Anyways......
Nimekua kwenye secta ya madini for more than 25 good years.
Ebu ngoja nikae kimya tu, maana kwasasa bado sina wakili.
 
Back
Top Bottom