Wizara ya Madini
Govt Institution
- Apr 12, 2025
- 50
- 20
Waziri wa Madini, Mhe. Anthony Mavunde leo Juni 4, 2025 amezindua zoezi la ulipaji fidia kwa Wananchi wa Kata ya Ngwalla Wilayani Songwe Mkoa wa Songwe kwa ajili ya kupisha ujenzi wa mradi wa uchimbaji na uchakataji wa Madini Adimu (Rare Earth Elements).
katika hafla ya Uzinduzi huo, amekabidhi Hundi yenye thamani ya shilingi 5,335,675,909 kwa Wananchi 120 waliopitiwa na mradi kwa lengo la kupisha ujenzi wa mradi huo ambao utagharimu zaidi ya shilingi bilioni 771.
Waziri Mavunde amesema kuwa, kuwepo kwa mgodi huo kunatarajiwa kuongeza chachu ya maendeleo ya kiuchumi na kijamii katika Kata ya Ngwalla na maeneo ya jirani. Madini Adimu yana umuhimu mkubwa katika sekta ya teknolojia, sumaku za magari ya umeme , vifaa vya afya na viwanda, hivyo kuifanya Tanzania kuwa miongoni mwa nchi zinazochangia kwa kiasi kikubwa katika mnyororo wa thamani wa madini hayo kimataifa.
Katika hatua nyingine, Waziri Mavunde amezindua Kituo Kidogo cha Polisi katika Kijiji cha Ngwalla, Wilayani Songwe, Mkoa wa Songwe kilichojengwa na Kampuni ya Mamba Minerals Corporation Ltd kama sehemu ya utekelezaji wa mpango wa Uwajibikaji kwa Jamii (Corporate Social Responsibility - CSR).
Kituo hicho kimegharimu zaidi ya Shilingi milioni 120 ambacho kimejengwa kwa lengo la kuimarisha ulinzi na usalama wa raia na mali zao katika eneo linalozunguka mgodi wa Madini Adimu (Rare Earth Elements).
Akizungumza katika hafla ya Uzinduzi huo uliohudhuriwa na viongozi wa Serikali, wawakilishi wa Kampuni, Vyombo vya Ulinzi na Usalama pamoja na Wananchi, Waziri Mavunde amesema ujenzi wa kituo hicho ni hatua muhimu inayokwenda sambamba na juhudi za Serikali za kuimarisha ulinzi katika maeneo ya kimkakati.
"Kituo hiki si tu kwamba kitaimarisha ulinzi wa raia na mali zao, bali pia kitakuwa kichocheo cha maendeleo ya kijamii na kiuchumi kwa wakazi wa Ngwalla na maeneo jirani. Hivyo natoa pongezi zangu kwa Kampuni ya Mamba Minerals Corporation Ltd kwa kuanza kutekeleza miradi ya kijamii hata kabla ya kuanza rasmi kwa uzalishaji wa madini, jambo linaloonesha nia njema na ushirikiano wa dhati kati ya kampuni na jamii," amesema Waziri Mavunde.
"Hili ni somo kwa wawekezaji wengine kwamba Social License ni muhimu kama ilivyo Mining License. Bila ridhaa na ushirikiano wa jamii, maendeleo hayatakuwa na msingi imara," amesema Waziri Mavunde.
Aidha, amesisitiza kuwa Sheria ya Madini, Sura Namba 123, inawataka wamiliki wa leseni kushirikiana na Halmashauri husika katika kutekeleza vipaumbele vya maendeleo vinavyopendekezwa kwa jamii.
Sambamba na hayo, Waziri Mavunde amezindua vyumba vya Madarasa mawili vilivyoghalimu kiasi cha zaidi ya shilingi Milioni 64 na maktaba iliyogharimu zaidi ya shilingi Milioni 44. na kutoa wito kwa wadau wa madini nchini kuhakikisha kuwa miradi ya CSR inalenga kuleta mabadiliko ya kweli kwa wananchi, hususan katika nyanja za elimu, afya, miundombinu na usalama.
Pia, Waziri Mavunde ameahidi kuwa Wizara yake itaendelea kusimamia kwa karibu utekelezaji wa miradi yote ya kijamii inayotokana na shughuli za uchimbaji madini ili kuhakikisha kuwa rasilimali za nchi zinawanufaisha Watanzania kwa wote na kuwataka wananchi wa Ngwalla kuendelea kushirikiana na wawekezaji kwa amani na mshikamano, huku akiahidi kuwa Serikali itaendelea kusimamia kwa karibu kuhakikisha kuwa rasilimali madini kuleta tija kwa Taifa.
Akizungumza katika hafla hiyo, Meneja Mkuu wa Kampuni ya Mamba Minerals Corporation Ltd, Juma Diwani, amesema kuwa maandalizi ya ujenzi wa mgodi wa Madini Adimu yanaendelea kwa kasi, huku ujenzi rasmi ukitarakiwa kuanza Desemba 2025, huku uzalishaji rasmi ukitarajiwa kuanza mwishoni mwa mwaka 2026.
"Tumejipanga kuanza kazi rasmi ndani ya mwaka mmoja ujao. Sambamba na ujenzi wa mgodi, pia tutaweka kiwanda cha kusafisha na kuchenjua madini hapa hapa nchini pamoja na mtambo wa kuzalisha umeme wa zaidi ya megawati 10 kwa lengo la kuongeza thamani madini haya hapa nchini na kuleta ajira kwa Watanzania," amesisitiza Diwani.
Diwani ameongeza kuwa hadi sasa, kampuni hiyo imetumia zaidi ya Shilingi bilioni 2.5 katika miradi mbalimbali ya kijamii kijijini Ngwalla, ikiwa ni pamoja na miundombinu ya shule, huduma za afya, maji safi na sasa kituo cha Polisi.
Naye, Mthamini Mkuu wa Serikali Evalyne Mugasha ameipongeza Kampuni ya Mamba Minerals Corporation Ltd kwa kukamilisha zoezi la utathimini na kuanza kutoa fidia kwa Wananchi wa Kata ya Ngwalla.