Waziri Mavunde - Maonesho ya Madini Geita Kuboresha Kufikia Hadhi ya Kimataifa

Waziri Mavunde - Maonesho ya Madini Geita Kuboresha Kufikia Hadhi ya Kimataifa

Stephano Mgendanyi

JF-Expert Member
Joined
May 16, 2020
Posts
2,833
Reaction score
1,301

MAONESHO YA MADINI GEITA KUBORESHWA KUFIKIA HADHI YA KIMATAIFA-MAVUNDE

- Rais Samia Suluhu Hassan kufunga maonesho

-I dadi ya washiriki wa nje ya nchi waongezeka

- RC Shigela aeleza mpango wa kujenga majengo ya kudumu na kuboresha miundombinu

📍Bombabili EPZ, Geita

Waziri wa Madini Mh. Anthony Mavunde amepongeza maonesho ya 7 ya Teknolojia ya Madini mkoani Geita kwa kuendelea kukua na kuongeza idadi kubwa zaidi ya washiriki wa ndani na nje ya nchi na hivyo kufikisha idadi ya zaidi ya washiriki 800 kwa mwaka huu 2024 na hivyo kuutaka mkoa wa Geita kuimarisha miundombinu ya eneo la Maonesho ili kuyafanya ya Kimataifa.

Waziri Mavunde ameyasema hayo leo Geita,wakati akikagua maonesho na kutoa hati za pongezi,ushiriki na ushindi kwa waoneshaji wa bidhaa na huduma.

“Ni dhamira ya Serikali kuona maonesho haya yanakuwa na kufikia hadhi ya kimataifa,hivyo Wizara ya Madini na Mkoa wa Geita tutashikiriana kwa ukaribu ili azma na ndoto hii kutimia.

Maonesho ya mwaka huu yamevutia udhamini mkubwa na ushiriki wa wadau wengi sana wa nje na ndani ya nchi,na hii ni dalili njema ya ukuaji wa maonesho haya mwaka hadi mwaka”Alisema Mavunde

Akitoa salamu zake,Mkuu wa Mkoa wa Geita amewapongeza washiriki wote wa mwaka huu kwa kuwa mahiri na wabunifu na hivyo kuyafanya maonesho haya kuvutia watu wengi wakiwemo wageni kutoka nchi mbalimbali.

Mh Shigela pia ameeleza mkakati wa mkoa ni kujenga miundombinu ya kudumu na kuboresha eneo la maonesho ili kukidhi mahitaji ya kimataifa.

Maonesho haya ya 7 ya Teknolojia ya Madini mkoani Geita yanafikia tamati tarehe 13.10.2024 kwa kuhitimishwa na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Samia S. Hassan ambaye anatarajiwa kuwa Mgeni Rasmi.
 

Attachments

  • WhatsApp Image 2024-10-12 at 19.22.19.jpeg
    WhatsApp Image 2024-10-12 at 19.22.19.jpeg
    215.4 KB · Views: 5
  • WhatsApp Image 2024-10-12 at 19.22.19(1).jpeg
    WhatsApp Image 2024-10-12 at 19.22.19(1).jpeg
    177.3 KB · Views: 5
  • WhatsApp Image 2024-10-12 at 19.22.19(2).jpeg
    WhatsApp Image 2024-10-12 at 19.22.19(2).jpeg
    171.3 KB · Views: 6
  • WhatsApp Image 2024-10-12 at 19.22.20.jpeg
    WhatsApp Image 2024-10-12 at 19.22.20.jpeg
    169.1 KB · Views: 6
  • WhatsApp Image 2024-10-12 at 19.22.20(1).jpeg
    WhatsApp Image 2024-10-12 at 19.22.20(1).jpeg
    140.7 KB · Views: 4
  • WhatsApp Image 2024-10-12 at 19.22.20(2).jpeg
    WhatsApp Image 2024-10-12 at 19.22.20(2).jpeg
    146 KB · Views: 6
  • WhatsApp Image 2024-10-12 at 19.22.21.jpeg
    WhatsApp Image 2024-10-12 at 19.22.21.jpeg
    204.7 KB · Views: 6
  • WhatsApp Image 2024-10-12 at 19.22.21(1).jpeg
    WhatsApp Image 2024-10-12 at 19.22.21(1).jpeg
    236.6 KB · Views: 6
  • WhatsApp Image 2024-10-12 at 19.22.21(2).jpeg
    WhatsApp Image 2024-10-12 at 19.22.21(2).jpeg
    132.9 KB · Views: 6
  • WhatsApp Image 2024-10-12 at 19.22.22.jpeg
    WhatsApp Image 2024-10-12 at 19.22.22.jpeg
    100.7 KB · Views: 7
Back
Top Bottom