Waziri Mavunde: Mradi mkubwa wa dhahabu Sengerema kuchochea ukuaji wa uchumi nchini

Waziri Mavunde: Mradi mkubwa wa dhahabu Sengerema kuchochea ukuaji wa uchumi nchini

Stephano Mgendanyi

JF-Expert Member
Joined
May 16, 2020
Posts
3,119
Reaction score
1,430

WAZIRI MAVUNDE: MRADI MKUBWA WA DHAHABU SENGEREMA KUCHOCHEA UKUAJI WA UCHUMI NCHINI​

☑️ Serikali yasaini mkataba wa nyongeza ya hisa kutoka asilimia 16 hadi 20 na Kampuni ya Nyanzaga

☑️ Mwekezaji arejesha Leseni Serikalini, Waziri Mavunde aagiza kupewa wachimbaji wadogo

☑️ Mradi kugharimu zaidi ya shilingi trilioni 1

☑️ Ni mgodi mkubwa wa dhahabu kuanzishwa tangu 2009

▪️Rais Samia apongezwa kwa mazingira wezeshi ya Uwekezaji

📍Sengerema, Mwanza.

Waziri wa Madini, Mhe. Anthony Mavunde, amesema kuwa utekelezaji wa Mradi wa Dhahabu wa Nyanzaga, unaotekelezwa kwa ubia kati ya Serikali ya Tanzania na Kampuni ya Perseus Mining Limited kupitia Kampuni ya Nyanzaga Mining Company Ltd, utakuwa kichocheo muhimu cha ukuaji wa uchumi wa taifa na ustawi wa wananchi katika kipindi chote cha utekelezaji wake.

Amesema hayo Agosti 20, 2025 katika Kijiji cha Sotta Wilaya ya Sengerema Mkoani Mwanza akiwa Mgeni Rasmi katika Hafla ya Utiaji Saini Makubaliano ya Nyongeza Kati ya Serikali na Kampuni ya Nyanzaga Mining Company Limited kwa Ajili ya Uchimbaji Mkubwa wa Madini ya Dhahabu Kupitia Kampuni ya Ubia ya Sotta Mining Corporation Limited.

Katika Hafla hiyo, Serikali imesaini mkataba wa nyongeza na Kampuni ya Nyanzaga Mining Limited kutoka asilimia 16 hadi 20 za umiliki wa hisa za Kampuni ya Ubia ya Sotta.

Akizungumza katika Hafla hiyo, Waziri Mavunde amebainisha kuwa zaidi ya shilingi trilioni 1 zinatarajiwa kuwekezwa katika utekelezaji wa mradi huo, hatua ambayo itasaidia kufungua fursa mpya za kiuchumi na kijamii kwa Watanzania hususan wananchi wa Wilaya ya Sengerema, Mkoa wa Mwanza na taifa kwa ujumla

Ameeleza manufaa ya Mradi huo kuwa ni pamoja na Ajira kwa Watanzania kwani Mradi utatoa ajira za moja kwa moja na zisizo za moja kwa moja kwa maelfu ya wananchi, na hivyo kupunguza changamoto ya ukosefu wa ajira; Ushiriki wa Watanzania ambapo Serikali imeweka mkazo katika kuhakikisha wananchi wanashiriki kikamilifu kupitia utoaji wa huduma na bidhaa mbalimbali zinazohitajika kwenye mradi.

Mafanikio mengine ni Mapato ya Serikali kupitia kodi, tozo na gawio la hisa za Serikali (20% free carried interest), ambapo mradi utaiingizia Serikali mapato

Naye, Mkuu wa Mkoa wa Mwanza, Mhe. Said Mtanda ameeleza kuwa kiasi cha fedha cha dola za Marekani milioni 500 zitakazotumika kujenga mradi huo, zitasaidia kubadilisha Mkoa wa Mwanza, na kwamba kuanzishwa kwa mradi huo utasaidia zaidi kuongeza mapato ya Serikali katika Mkoa huo.

Awali akizungumza, Msajili wa Hazina Nehemia Mchechu ameeleza kuwa, Mgodi huo utaletea taifa maendeleo endelevu, ni moja ya miradi mikubwa zaidi ya madini Tanzania na utaleta faida kubwa kwa taifa na kwamba utaingizia Serikali shilingi bilioni 400 lakini pia mapato kupitia Kodi, gawio na vitu vingine, lakini pia utaleta ajira,

“mradi huu utaimarisha uchumi wetu, katika kipindi cha mnyukano wa uchumi duniani, kilichotusaidia ni madini, ni bidhaa inayotuletea fedha nyingi sana za kigeni na kusaidia kuimarisha uchumi

Screenshot 2025-08-22 at 20-09-40 Instagram.png
Screenshot 2025-08-22 at 20-09-47 Instagram.png
Screenshot 2025-08-22 at 20-10-08 Instagram.png
Screenshot 2025-08-22 at 20-10-25 Instagram.png
 

Attachments

  • Screenshot 2025-08-22 at 20-09-59 Instagram.png
    Screenshot 2025-08-22 at 20-09-59 Instagram.png
    512.1 KB · Views: 37
Back
Top Bottom