Roving Journalist
JF Roving Journalist
- Apr 18, 2017
- 3,984
- 13,760
Kutoka mkoani Mwanza, Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa – TAMISEMI, Mohamed Mchengerwa ameamua kuzungumza na Waandishi wa Habari kujibu madai kadha wa kadha yanayo husishwa na Uchaguzi wa Serikali za Mitaa
ALICHOELEZA MCHENGERWA
Mkanganyiko wa Uchaguzi
Natambua kumekuwa na mkanganyiko kati ya daftari la kudumu la linalosimamiwa na Tume Huru ya Uchaguzina Daftari la Makazi au la Wapiga Kura watakaopiga kura tarehe 27 Novemba 2024.
Kutokana na mkanganyiko huo, Ofisi ya Rais - TAMISEMI imehakikisha wananchi wanapata uelewa na ufahamu kwamba marekebisho ya daftari yanayosimamiwa na Tume Huru ya Uchaguzi ni tofauti na la Makazi ambalo linahusika na Uchaguzi wa Serikali za Mitaa.
Wito kwa Watanzania
Nitumie fursa hii kuwaomba wananchi kujitokeza kwa wingi kujiandikisha ili kuwachagua viongozi wa mitaa, vijiji na vitongoji.
Usipojiandikisha sasa kwa ajili ya uchaguzi wa serikali za mitaa, maana yake utakuwa sifa ya kupiga kura tarehe 27 Novemba, 2024.
Elimu zaidi inahitajika
Lazima tukiri kuwa mkanganyiko huu unapaswa kuendelea kutolewa elimu na ikumbukwe kwamba mchakato wa uchaguzi ni mchakato wa mwaka mzima. Si mchakato ulioanza leo. Sisi OR-TAMISEMI toka mwaka jana mwezi wa 10 kwasababu mchakato wa uchaguzi ni kalenda ya mwaka mzima. Mchakato huu haufanywi na OR-TAMISEMI; ni mchakato wa kila mmoja wetu. Mchakato huu ni wa kila Mtanzania na kila aliyetimiza umri wa miaka 18 na kuendelea.
Lakini pia, mchakato huu unavihusu vyama vya siasa. Kila chama kina wajibu wa kuhakikisha tunatoa elimu kwa Watanzania... na elimu hizo ziwe ni kutoa mkanganyiko unaoweza kujitokeza kuhusu Daftari la Kudumu linalosimamiwa na Tume Huru na Daftari la Makazi linalohusika na Serikali za Mitaa.
Lazima tukiri kwamba katika zoezi linaloendelea kuna mambo yaliyojitokeza ambayo wadau wa vyama wamekuwa wakiyasema pengine hayajakaa sawa. Na baadhi ya masuala haya nitayatolea ufafanuzi.
TAMISEMI kutohamasisha
- Ipo hoja ya TAMISEMI kutohamasisha au kutoa elimu kuhusu Uchaguzi wa Serikali za Mitaa. Baadhi ya watu wamekuwa wakilalamika kuwa kazi kubwa haijafanyika ya kutoa elimu. Napenda kuwaambia wananchi kuwa mchakato huu ni wa mwaka mzima na tumetoa elimu katika kila kona ya nchi... Tumetoa elimu kwenye, vyombo vya habari, mitandao lakini pia wasanii wametoa elimu vijijini na mijini na wengine wametumia lugha za maeneo hayo ili wahusika waelewe kile ambacho uchaguzi umekusudia.
...Nithibitishe kuwa hakuna wakati ambapo TAMISEMI imejiandaa kama wakati huu. Hii ni kwa maana kwamba uchaguzi huu umeandaliwa kuliko chaguzi zote zilizopita...
Jambo lingine ambalo ningependa kulitolea ufafanuzi ni kuhusu wasimamizi wa vituo kukataa kutoa takwimu za uandikishaji wa mawakala.
Kuna watu wamekuwa wakitaka kupata takwimu za uandikishaji kwa waandishi. Nitoe ufafanuzi kuhusu hili. Mawakala wanatekeleza jukumu lao la msingi la kuhakikisha wananchi wanajiandikisha kwa mujibu wa kanuni na miongozo pasipo bughudha.
Suala la ukaguzi wa daftari lipo kwa mujibu wa kanuni za uchaguzi. Mkisema vizuri kanuni ya 10, fasiri ya 4 na 5, Tangazo la Serikali Na. 572, na kanuni ya 11, fasiri ya 4 na 5, Tangazo la Serikali Na. 571, 573 na 574, limeweka wazi baadhi ya zoezi kukamilika. Lumeweka wazi kuwa baada ya zoezi kukamilika, orodha itaweka wazi kwa wananchi wote, wakiwemo na viongozi wa vyama vya siasa watakafua daftari ili kujiridhisha na usahihi wa orodha iliyotolewa.
Jukumu walilo nalo mawakala wote wa vyama vya siasa wana wajibu wa kuwatambua wale wote wanaokwenda kujiandikisha.
Ukiwa kuna kasoro, kuna fursa ya kurekebisha kasoro hizo na kanuni imeweka wazi wa nini kifanyike iwapo kutakuwa na kasoro zilizobainika. Kanuni hizi zilishirikisha vyama vyote 19.
Uandikishaji wa watu wenye umri mdogo
Kumekuwepo na taarifa kwamba yapo maeneo ambapo baadhi ya watu wameandikishwa ambao pengine umri wao mdogo. Ni taarifa ambazo nimezisikia, lakini hatujapata uthibitisho wa taarifa hizi. Nichukue fursa hii kueleza kwamba kanuni zetu za uchaguzi zimetoa maelezo ya kina kuhusu ni nani mwenye haki ya kujiandikisha kupiga kura kwenye uchaguzi wa Serikali za Mitaa, kuwa ni miaka 18 au zaidi.
...niwakumbushe kujikita katika misingi ya kanuni ili kila mmoja wetu atapatiwa haki yake ya msingi.
Kulikuwepo na malalamiko kwamba tarehe ya kuchukua na kurudisha fomu ni siku moja. Baada ya kupokea maoni, Serikali ilikubaliana kwamba tarehe ya kuchukua na kurejesha fomu itakuwa kuanzia tarehe 26 Oktoba hadi Novemba 1, 2024. Hivyo, nawasihi wananchi wote wenye sifa za kugombea kujitokeza na kutimiza haki yao ya kikatiba.
Waliojiandikisha ni 45%
Watanzania wenye sifa na waliojiandikisha ni 45%, hali ambayo inaonesha kuna hamasa kuelekea katika uchaguzi huo unaotarajiwa kufanyika Novemba 27, 2024
Mikoa inayofanya vizuri katika uandikishaji ni Tanga, Ruvuma, Songwe, Iringa na Njombe. Mikoa ambayo ipo chini katika uandikishaji ni Katavi, Kilimanjaro, Geita na Manyara.