Waufukweni
JF-Expert Member
- May 16, 2024
- 2,060
- 5,648
Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais TAMISEMI, Mohammed Mchengerwa, ametangaza rasmi tarehe ya kuchukua na kurejesha fomu za kugombea kwenye Uchaguzi wa Serikali za Mitaa kuwa ni kuanzia tarehe 26 Oktoba hadi Novemba 1, 2024. Mchengerwa amewasihi wananchi wote wenye sifa za kugombea, kama ilivyoainishwa katika kanuni za uchaguzi, kujitokeza na kutimiza haki yao ya kikatiba.
"Kulikuwepo na malalamiko kwamba tarehe ya kuchukua na kurudisha fomu ni siku moja. Baada ya kupokea maoni, Serikali ilikubaliana kwamba tarehe ya kuchukua na kurejesha fomu itakuwa kuanzia tarehe 26 Oktoba hadi Novemba 1, 2024. Hivyo, nawasihi wananchi wote wenye sifa za kugombea kujitokeza na kutimiza haki yao ya kikatiba." alisema Mchengerwa.
Aidha, Mchengerwa amesisitiza umuhimu wa wasimamizi wa uchaguzi na wasaidizi wake kusimamia kanuni kwa usahihi na kuhakikisha mchakato unafanyika kwa haki na uwazi.
Pia, Soma:
+ Waziri Mchengerwa: Hakuna Uthibitisho wa madai ya Uandikishaji Wanafunzi Kupiga Kura
+ Waziri Mchengerwa: Uchaguzi wa Serikali za Mitaa Bara utafanyika 27 November, 2024