PAYE
JF-Expert Member
- Jun 19, 2025
- 459
- 644
Serikali imesema hakuna mwananchi yeyote atakayeenda kwenye Kituo chochote cha kutolea huduma za afya au Hospitali, akakosa kupatiwa matibabu eti kwa sababu hana fedha.
Akizungumza kwenye kikao kazi cha watumishi wa sekta ya afya Mkoa wa Dar es Salaam leo, Jumatatu Desemba 08.2025, Waziri wa Afya Mohamed Mchengerwa amesema serikali kupitia Hospitali zake imeweka utaratibu wa kutoa msamaha kwa wananchi wasio na uwezo, jambo ambalo ameelekeza lisimamiwe kikamilifu.
Katika suala hilo, Waziri Mchengerwa ametolea mfano Hospitali ya Taifa Muhimbili (MNH) ambayo kwa mwaka inatoa msamaha usiopungua bilioni 19.