Waziri Mchengerwa: Muhimbili mpya siyo mradi wa afya tu, ni uwekezaji wa kimkakati

Hospitali ya Taifa Muhimbili

Public Institution
Joined
Apr 9, 2026
Posts
13
Reaction score
38
WhatsApp Image 2026-05-11 at 12.49.08.jpeg

WAZIRI MCHENGERWA: MUHIMBILI MPYA SIYO MRADI WA AFYA TU, NI UWEKEZAJI WA KIMKAKATI

Serikali imeeleza kuwa kuijenga upya Hospitali ya Taifa Muhimbili si mradi wa afya pekee bali ni uwekezaji wa kimkakati wenye maslahi mapana ya kitaifa na kimataifa katika sekta ya tiba, elimu, utafiti na uchumi wa huduma za afya.

Akizungumza leo bungeni Dodoma wakati wa kuwasilisha bajeti ya Wizara ya Afya ya mwaka 2026/27, Waziri wa Afya Mohamed Mchengerwa amesema mradi huo unalenga kuifanya Tanzania kuwa kitovu cha huduma za kibingwa na ubingwa bobezi barani Afrika huku ukipunguza gharama za kuwapeleka wagonjwa kutibiwa nje ya nchi.

"Mradi wa Muhimbili mpya si mradi wa afya pekee bali ni uwekezaji wa kimkakati katika uchumi wa kisasa kwani utapunguza rufaa za matibabu nje ya nchi, kuongeza utalii wa tiba, kuvutia wawekezaji na mashirika ya kimataifa pamoja na kusaidia kukuza vipaji na utaalam wa wataalam wa afya nchini." amesema Mh.Mchengerwa

Aidha ameongeza kuwa kukamilika kwa Muhimbili mpya kutaifanya hospitali hiyo kupanda kutoka ngazi ya tatu hadi ngazi ya nne ya ubora wa utoaji huduma kwa viwango vya kimataifa, hatua ambayo itaongeza uwezo wa Tanzania kutoa huduma za kisasa zaidi za matibabu, mafunzo na tafiti.

Itakumbukwa kuwa ujenzi wa Muhimbili Mpya ni sehemu ya mpango wa muda mrefu ulioanza mwaka 2018 na unatarajiwa kutekelezwa kwa kipindi cha miaka mitano kwa gharama ya dola za Marekani milioni 468.469 (USD 468,469,000), sawa na zaidi ya shilingi trilioni 1.2 za Kitanzania. Kati ya fedha hizo, takribani dola za Marekani milioni 363.9 ni mkopo kutoka Korea Kusini, huku dola milioni 104.572 zikiwa ni mchango wa Serikali ya Tanzania kwa ajili ya kodi, maandalizi ya eneo la mradi pamoja na gharama nyinginezo.
 
Mkuu andika moja tu tushaona.

View attachment 3587346

Ile iliopo pale mnabomoa? Maana kuna extension ya MOI inakengwa,kuna jengo jipya la MOI na kuna majengo mengi tu mapya.
 
Majizi makubwa nyie , tunajua hilo ni dili la MKOPO wa BILIONI 700 kutoka Korea, Mchengerwa na Naibu Katibu Mkuu wake Emmanuely Tayali, wameshakula mgawo wao kujandalia mazingira ya uchaguzi 2030 2040. Ipo siku hizo hela mtazitapika wahuni wakubwa nyie. Mnaacha kuboresha hospitali za Rufaa za Mikoa mnalazimisha watu waje Dar es Salaam iliyokwishajaa.
 
Ile iliopo pale mnabomoa? Maana kuna extension ya MOI inakengwa,kuna jengo jipya la MOI na kuna majengo mengi tu mapya.
Wakukujibu uni tag

Ila hawa wanaweza bomoa
Maana kwenye bomoa na jenga wanajuwa,ila badaye kwenye huduma ndiyo sifuri

Ova
 
View attachment 3587346
WAZIRI MCHENGERWA: MUHIMBILI MPYA SIYO MRADI WA AFYA TU, NI UWEKEZAJI WA KIMKAKATI

Serikali imeeleza kuwa kuijenga upya Hospitali ya Taifa Muhimbili si mradi wa afya pekee bali ni uwekezaji wa kimkakati wenye maslahi mapana ya kitaifa na kimataifa katika sekta ya tiba, elimu, utafiti na uchumi wa huduma za afya.

Akizungumza leo bungeni Dodoma wakati wa kuwasilisha bajeti ya Wizara ya Afya ya mwaka 2026/27, Waziri wa Afya Mohamed Mchengerwa amesema mradi huo unalenga kuifanya Tanzania kuwa kitovu cha huduma za kibingwa na ubingwa bobezi barani Afrika huku ukipunguza gharama za kuwapeleka wagonjwa kutibiwa nje ya nchi.

"Mradi wa Muhimbili mpya si mradi wa afya pekee bali ni uwekezaji wa kimkakati katika uchumi wa kisasa kwani utapunguza rufaa za matibabu nje ya nchi, kuongeza utalii wa tiba, kuvutia wawekezaji na mashirika ya kimataifa pamoja na kusaidia kukuza vipaji na utaalam wa wataalam wa afya nchini." amesema Mh.Mchengerwa

Aidha ameongeza kuwa kukamilika kwa Muhimbili mpya kutaifanya hospitali hiyo kupanda kutoka ngazi ya tatu hadi ngazi ya nne ya ubora wa utoaji huduma kwa viwango vya kimataifa, hatua ambayo itaongeza uwezo wa Tanzania kutoa huduma za kisasa zaidi za matibabu, mafunzo na tafiti.

Itakumbukwa kuwa ujenzi wa Muhimbili Mpya ni sehemu ya mpango wa muda mrefu ulioanza mwaka 2018 na unatarajiwa kutekelezwa kwa kipindi cha miaka mitano kwa gharama ya dola za Marekani milioni 468.469 (USD 468,469,000), sawa na zaidi ya shilingi trilioni 1.2 za Kitanzania. Kati ya fedha hizo, takribani dola za Marekani milioni 363.9 ni mkopo kutoka Korea Kusini, huku dola milioni 104.572 zikiwa ni mchango wa Serikali ya Tanzania kwa ajili ya kodi, maandalizi ya eneo la mradi pamoja na gharama nyinginezo.
Yale yale ya DP word gharama za zitapungua, mapato yataongezeka.
 
Ile iliopo pale mnabomoa? Maana kuna extension ya MOI inakengwa,kuna jengo jipya la MOI na kuna majengo mengi tu mapya.
Ubaya ni kuwa majengo mengi pale hayana hata miaka 25. Na mengi ndani ya miaka 25 hiyo yamefanyiwa maboresho makubwa. Moja ya mambo yaliyotufelisha waafrika baada ya uhuru ni kupenda vitu grand na 'vinavyong'aa' ili tusifiwe badala ya kuangalia mambo kiuchumi zaidi. Leo bado hiyo mentality haijatutoka.
 
Nyerere hakutaka hivyo vitu grand.

Amandla...
 
Wanasiasa wetu wanajua sana kutumia maneno matamu ya kulewesha kiasi kwamba usipokuwa mwerevu unahamasika kumpongeza. Najsribu kuwaza kama haya mawazo ya kuijenga upya muhimbili ni wazo la mtu mmoja au mawazo jumuishi ya wataalamu wote katika wizara ya afya. Na kama ni mawazo ya wabobevu wote wa wizara ya afya, basi tuna safari ndefu sana kama taifa.
 
Wakukujibu uni tag

Ila hawa wanaweza bomoa
Maana kwenye bomoa na jenga wanajuwa,ila badaye kwenye huduma ndiyo sifuri

Ova
Hivi tunavyojadili hapa kuna jengo linajengwa pembeni ya MOI. Sasa na hilo litavunjwa au majengo mapya yanabaki?
 
View attachment 3587346
WAZIRI MCHENGERWA: MUHIMBILI MPYA SIYO MRADI WA AFYA TU, NI UWEKEZAJI WA KIMKAKATI

Serikali imeeleza kuwa kuijenga upya Hospitali ya Taifa Muhimbili si mradi wa afya pekee bali ni uwekezaji wa kimkakati wenye maslahi mapana ya kitaifa na kimataifa katika sekta ya tiba, elimu, utafiti na uchumi wa huduma za afya.

Akizungumza leo bungeni Dodoma wakati wa kuwasilisha bajeti ya Wizara ya Afya ya mwaka 2026/27, Waziri wa Afya Mohamed Mchengerwa amesema mradi huo unalenga kuifanya Tanzania kuwa kitovu cha huduma za kibingwa na ubingwa bobezi barani Afrika huku ukipunguza gharama za kuwapeleka wagonjwa kutibiwa nje ya nchi.

"Mradi wa Muhimbili mpya si mradi wa afya pekee bali ni uwekezaji wa kimkakati katika uchumi wa kisasa kwani utapunguza rufaa za matibabu nje ya nchi, kuongeza utalii wa tiba, kuvutia wawekezaji na mashirika ya kimataifa pamoja na kusaidia kukuza vipaji na utaalam wa wataalam wa afya nchini." amesema Mh.Mchengerwa

Aidha ameongeza kuwa kukamilika kwa Muhimbili mpya kutaifanya hospitali hiyo kupanda kutoka ngazi ya tatu hadi ngazi ya nne ya ubora wa utoaji huduma kwa viwango vya kimataifa, hatua ambayo itaongeza uwezo wa Tanzania kutoa huduma za kisasa zaidi za matibabu, mafunzo na tafiti.

Itakumbukwa kuwa ujenzi wa Muhimbili Mpya ni sehemu ya mpango wa muda mrefu ulioanza mwaka 2018 na unatarajiwa kutekelezwa kwa kipindi cha miaka mitano kwa gharama ya dola za Marekani milioni 468.469 (USD 468,469,000), sawa na zaidi ya shilingi trilioni 1.2 za Kitanzania. Kati ya fedha hizo, takribani dola za Marekani milioni 363.9 ni mkopo kutoka Korea Kusini, huku dola milioni 104.572 zikiwa ni mchango wa Serikali ya Tanzania kwa ajili ya kodi, maandalizi ya eneo la mradi pamoja na gharama nyinginezo.
Kwa hali ya sasa, na hali ya huduma zetu za afya ilivyo katika hospitali zetu za rufaa za kanda, hospitali za Rufaa za mikoa, hospitali za wilaya, vituo vya afya pamoja na dhahanati; Kupeleka 1.2 Trilioni kwenda kubomoa majengo ya hospitali ya sasa ya Muhimbili ili tujenge mengine ya kisasa ni uwekezaji mbaya.
Nchi hii ina cardiac center moja tu, ipo JKCI!
Almost hospitali zetu za mikoa zote hazina MRI.
Wasaidizi wa Rais tunaowajibu wa kumshauri vizuri Rais kwa kuzingatia maslahi mapana ya nchi.
Watu wa Mara, Kagera, Kigoma, Katavi, Rukwa, Songwe n.k maisha yao hayataokolewa Muhimbili.
Na tukiwa wakweli, hivi Dar es salaam kuna shida ya hospitali?
Muhimbili imezungukwa na Agakhan, Regency, Rabinsia, Hindu mandal, Saifee, Kairuki, Masana, Boch, Kitonka, Kitengule, n.k Kuna shida gani pale huduma?
 
Hivi tunavyojadili hapa kuna jengo linajengwa pembeni ya MOI. Sasa na hilo litavunjwa au majengo mapya yanabaki?
Hawana plan hawa siku zote
Wao wanajuwa vunja jenga
Wanafikiri majengo mazuri
Ndiyo kuwa na huduma bora

Ova
 
Kwa hali ya sasa, na hali ya huduma zetu za afya ilivyo katika hospitali zetu za rufaa za kanda, hospitali za Rufaa za mikoa, hospitali za wilaya, vituo vya afya pamoja na dhahanati; Kupeleka 1.2 Trilioni kwenda kubomoa majengo ya hospitali ya sasa ya Muhimbili ili tujenge mengine ya kisasa ni uwekezaji mbaya.
Nchi hii ina cardiac center moja tu, ipo JKCI!
Almost hospitali zetu za mikoa zote hazina MRI.
Wasaidizi wa Rais tunaowajibu wa kumshauri vizuri Rais kwa kuzingatia maslahi mapana ya nchi.
Watu wa Mara, Kagera, Kigoma, Katavi, Rukwa, Songwe n.k maisha yao hayataokolewa Muhimbili.
Na tukiwa wakweli, hivi Dar es salaam kuna shida ya hospitali?
Muhimbili imezungukwa na Agakhan, Regency, Rabinsia, Hindu mandal, Saifee, Kairuki, Masana, Boch, Kitonka, Kitengule, n.k Kuna shida gani pale huduma?
Whn hawa

Ova
 
Wanasiasa wetu wanajua sana kutumia maneno matamu ya kulewesha kiasi kwamba usipokuwa mwerevu unahamasika kumpongeza. Najsribu kuwaza kama haya mawazo ya kuijenga upya muhimbili ni wazo la mtu mmoja au mawazo jumuishi ya wataalamu wote katika wizara ya afya. Na kama ni mawazo ya wabobevu wote wa wizara ya afya, basi tuna safari ndefu sana kama taifa.

Inasikitisha sana
 
Back
Top Bottom