Waziri Mchengerwa: Nitavunja Mabaraza ya Serikali za mitaa yenye mivutano

Waziri Mchengerwa: Nitavunja Mabaraza ya Serikali za mitaa yenye mivutano

Suley2019

JF-Expert Member
Joined
Oct 7, 2019
Posts
2,203
Reaction score
5,610
Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa, Mohamed Mchengerwa amesema atavunja mabaraza ya madiwani yenye mivutano inayokwamisha maendeleo ya wananchi.

Waziri Mchengerwa ametoa kauli hiyo wakati wa kukagua ujenzi wa Hospitali ya Wilaya inayojengwa Kata ya Kibelege katika Halmashauri ya Mji Ifakara na kubaini kuwa imeshindwa kukamilika kutokana na mivutano ya kisiasa uliotokea mara tu fedha za ujenzi wa hospitali hiyo zilipofika.

Amesema mivutano ya kisiasa ya madiwani husababisha miradi mbalimbali ya maendeleo kusimama na kutokamilika kwa wakati na kusisitiza kuwa atachukua hatua mara moja ikiwa ni pamoja na kuvunja Baraza la Madiwani la halmashauri husika.

Aidha, Mchengerwa ametumia fursa hiyo kuwaagiza watendaji katika halmashauri nchi nzima kuacha mivutano na wanasiasa na kusababisha ucheleweshaji wa miradi ya maendeleo.
 
Elewa neno Mabaraza, kwenu km kuna kibaraza cha nje mnakaa kibarazani sasa haya ni Mabaraza yenye mvutano, kikiwa kimoja ni kibaraza yakiwa mengi ni Mabaraza kwa Msaada wa TUKI na BAKITA
 
Sasa si lazima mjadiliane? Kuna majadiliano yasiyokuwa na mvutano,? Au kukubaliana Kila kitu ndio ina ruhusa ya serikali,?
 
Back
Top Bottom