Waufukweni
JF-Expert Member
- May 16, 2024
- 2,060
- 5,648
Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais-TAMISEMI, Mohamed Mchengerwa, amepongeza vyama 19 vya siasa kwa kushiriki kwa uwazi na utulivu katika Uchaguzi wa Serikali za Mitaa wa mwaka 2024, licha ya baadhi yao kushindwa kupata nafasi mbalimbali za uongozi.
Akizungumza Novemba 28, 2024, jijini Dodoma wakati wa kutangaza matokeo ya jumla ya uchaguzi huo, Mchengerwa amrwataka wanasiasa kuendelea kushikamana na kujiimarisha kwa chaguzi zijazo, akisisitiza umuhimu wa mshikamano katika kukuza demokrasia ya nchi.
Pia, Soma: CCM yashinda 98.83% Wenyeviti Serikali za Mitaa
Aidha, amewataka viongozi wa vyama hivyo na wanachama wao kuendelea kushirikiana katika kulijenga taifa kwa kuzingatia uzalendo, huku akiwakumbusha kuwa uchaguzi huu ni hatua moja kati ya chaguzi nyingi zinazofuata.