Waziri Mchengerwa zuia ziara ya Madiwani Maswa kwenda Mbarali haina tija

Waziri Mchengerwa zuia ziara ya Madiwani Maswa kwenda Mbarali haina tija

Mwanantogakulya

Senior Member
Joined
Mar 18, 2025
Posts
157
Reaction score
155
Madiwani Maswa kwenda Mbarali kujifunza kilimo cha mpunga hayo ni matumizi mabaya ya fedha za walipa kodi.

Madiwani hao wamebakiza miezi miwili baraza hilo livunjwe sasa kuwapeleka Mbarali kuna tija gani wakati zao la mpunga kwa wilaya ya Maswa linalimwa maeneo ya Malampaka na wakulima wanapata mazao kwa uzalishaji bora.

Mazingira ya mbarali hasa katika shamba la Kapunga lile ni la Muwekezaji ambaye anatumia zana za kisasa katika kulima,kumwagilia hadi kuvuna huwezi kumlinganisha na mkulima wa kawaida wa Maswa.
Serikali ya mkoa wa Simiyu kutoa kibali cha kwenda kufanya ziara hiyo ni matumizi.mabaya ya fedha za serikali wakati bado tuna upungufu wa madawati kwa wanafunzi wa shule za msingi ambao wanakaa chini katika shule mbalimbali ikiwemo shule ya Msingi Ipililo B.

Bado mji wa Maswa ni mchafu ambao unatakataka na ambazo wameshindwa kuziondoa katika eneo la stendi ya zamani na maeneo mengine ya mji likiwemo eneo la stendi mpya ya Mabasi hivyo kweli tutaweza kuupandisha hadhi kuwa Halmashauri ya mji lakini fedha za usafi hazipo leo zaidi ya Sh Milioni 20 zinatumika kusafirisha madiwani kwenda kutembea kutumia pesa za walipa kodi haya ni matumizi ya hovyo sana na Waziri wa Tamisemi, Mh Mohamed Mchengerwa unakubalina na jambo hilo.

Kwa sasa kuna ugomvi mkubwa wa fedha kati Mamlaka ya mji mdogo wa Maswa na halmashauri ya wilaya ambayo haitaki kuihudumia kikamilifu mamlaka hiyo kwa kushindwa kuipa ikusanye vyanzo vyake vya mapato lakini pesa ya kwenda kuzulula Mbarali mkoani Mbeya imepatikana.

Katika mtego huo wamemwigiza DC Maswa, Dkt Vicent Anney na DED Maswa,Mtipa Maisha kuingia kwenye ziara hiyo ya kwenda kuzurula na kutumia magari ya serikali.
 
  • Thanks
Reactions: Wij
Back
Top Bottom