Waziri Medard Kalemani asiondolewe Wizara ya Nishati

Waziri Medard Kalemani asiondolewe Wizara ya Nishati

The Boss

JF-Expert Member
Joined
Aug 18, 2009
Posts
49,282
Reaction score
117,244
Pamoja na mapungufu yake Waziri Kalemani bado ana vision sahihi ya umeme nafuu Kwa Watanzania.

Kampeni ya kumchafua na kumshambulia ikemewe kwa nguvu zote.

Kuna madadali wa kununua umeme wa gesi wameanza kampeni ya kumchafua na kumchomekea Mama wale matapeli wa zamani

Kama Professa Muhongo na Ngeleja ili waanze upigaji tena.
 
aondolewe kwa sababu gani?! kwa ajili ya wahujumu? wataondoka wao sio Dr. Kalemani.

Dr. Kalemani Kazi yake imetukuka na jitihada zake za kizalendo zinajieleza zenyewe kamwe hakuna wa kumchafua na akachafuka.

Rekodi yake inamfuata popote pale alipo, wasijaribu kupima kina cha maji
 
Pamoja na mapungufu yake Waziri Kalemani bado ana vision sahihi ya umeme nafuu Kwa Watanzania...
Tatzo sio remote tatzo ni mshika remote...na mshika remote hao uliowataja ndo wapambe wake wakimwambia weka diestivii anaweka, weka katuni toa tibisiii hatuipendi anatoa and remote haina uwezo wa kusema no kwa mshika remote...remote kazi yake ni kumfurahisha mshika remote baasi.
 
Umefika wakati wa Tanesco kupata mshindani, haya yote tunayoyaona sasa yanasababishwa na ukiritimba wa Tanesco kuhodhi kila kitu.

Ndio maana wanatokea hao wajanja wanataka kumuharibia Waziri kama unavyosema japo sina hakika.

Miaka yote Tanesco imekuwa inaendeshwa kwa hasara na kutoa huduma mbovu licha ya kuwa shirika pekee linalotoa nishati ya umeme nchini tena bila upinzani.
 
Naunga mkono hoja
puuzi Mtupu, Muhongo anaingiaje hapo. OOh!!! Muhongo na Ngereja..Wewe ni Fara sana Ebu tuelezee Muunganiko uliopo kati ya Muhongo na Kuwepo tatizo la LUKU. Acha Upuuzi wa Kuwakashifu watu.

Ni kweli viongozi uliowatuhumu walipata kuhudumu kama mawaziri kwenye wizara hiyo. Sasa ebu tuambie influence zao kwenye swala la umeme. Nyambafuuu
 
Pamoja na mapungufu yake Waziri Kalemani bado ana vision sahihi ya umeme nafuu Kwa Watanzania...
Narudia tena na tena, Merdard Kalemani, Doto Biteko, Dr Dorothy Gwajima, Prof Ndalichako, mganga mkuu wa serikali, sio msaada kwa sasa kwenye serikali ya awamu ya Sita. Kuna vijana wadogo wenye uwezo kuliko lini kundi ambalo kwa sasa wamekata tamaa tangu 17.3.2021.
 
Pamoja na mapungufu yake Waziri Kalemani bado ana vision sahihi ya umeme nafuu Kwa Watanzania....
Nadhani ungesema ana vision ya umeme wa maji na sio wa bei nafuu. Una uhakika gani huo umeme wa maji utakuwa wa bei nafuu, wakati tumekopa 6.5t huku ukiwa hujui terms za marejesho? Kwahiyo kama ni Utetezi ama ushauri fanya kwa vigezo vingine, lakini sio unafuu wa bei.
 
Pamoja na mapungufu yake Waziri Kalemani bado ana vision sahihi ya umeme nafuu Kwa Watanzania.

Kampeni ya kumchafua na kumshambulia ikemewe kwa nguvu zote....
Hakuna mtu aliyekuwa above kukosolewa. Tusipokubaliana na utendaji wake. Na nyie ambao mnaona anafanya vizuri mna haki ya kutupinga na kutuonyesha wapi hatumtendei haki.

Hizi lugha za kujivisha bendera ya uzalendo hakututishi maana tunajua ukimya wetu umechangia sana kutufikisha hapa tulipo. Na kama mtu wenu ni mzalendo msomi kweli atasikiliza zaidi criticism zetu kuliko mapambio yenu ili aboreshe utendaji wenu pale atakapoona kuwa ukosoaji wetu una ukweli.

Amandla...
 
Pamoja na mapungufu yake Waziri Kalemani bado ana vision sahihi ya umeme nafuu Kwa Watanzania.

Kampeni ya kumchafua na kumshambulia ikemewe kwa nguvu zote....
Hadi tunavyoripoti muda huu, TANESCO iko hoi haina fedha za kutekeleza miradi mipya ya umeme na mikoa ya simiyu,katavi ,kigoma na Geita miradi mipya ya umeme imekwama kufanyika kwa asilimia 100 kwa kukosa fedha ña nchi iko uchumi wa Kati. Kalemani hajiongezi alizoea kufanyiwa kazi na JPM hata huko Jimboni kwake.
 
aondolewe kwa sababu gani?! kwa ajili ya wahujumu? wataondoka wao sio Dr. Kalemani.

Dr. Kalemani Kazi yake imetukuka na jitihada zake za kizalendo zinajieleza zenyewe kamwe hakuna wa kumchafua na akachafuka.

Rekodi yake inamfuata popote pale alipo, wasijaribu kupima kina cha maji

Kipindi cha Magufuli wajinga wengi walijiita wazalendo, ndio maana mengi waliyokuwa wakiyazumgumza na kufanya kipindi cha Magufuli, sasa hivi wanaongea na kutenda tofauti. Mfano suala la covid nk.
 
Hakuna mtu aliyekuwa above kukosolewa. Tusipokubaliana na utendaji wake. Na nyie ambao mnaona anafanya vizuri mna haki ya kutupinga na kutuonyesha wapi hatumtendei haki. Hizi lugha za kujivisha bendera ya uzalendo hakututishi maana tunajua ukimya wetu umechangia sana kutufikisha hapa tulipo. Na kama mtu wenu ni mzalendo msomi kweli atasikiliza zaidi criticism zetu kuliko mapambio yenu ili aboreshe utendaji wenu pale atakapoona kuwa ukosoaji wetu una ukweli.

Amandla...

Kunywa mtori hapo kwa mangi ni PM bill. Nimekuelewa sana hapo uliposema ukimya wetu ndio umetufikisha hapa tulipo.
 
Back
Top Bottom