Waziri Medard Kalemani asiondolewe Wizara ya Nishati

Waziri Medard Kalemani asiondolewe Wizara ya Nishati

Madalali wakubwa wamerudi tena kazini hivyo ushauri wa mleta mada ni wa haki kabisa.

Mwananchi anataka umeme wa bei ndogo na hao wazee wa asilimia zao za pembeni hawawezi kuupenda umeme wa maji.
 
Pamoja na mapungufu yake Waziri Kalemani bado ana vision sahihi ya umeme nafuu Kwa Watanzania.

Kampeni ya kumchafua na kumshambulia ikemewe kwa nguvu zote.

Kuna madadali wa kununua umeme wa gesi wameanza kampeni ya kumchafua na kumchomekea Mama wale matapeli wa zamani

Kama Professa Muhongo na Ngeleja ili ili waanze upigaji tena.
Yaani huyo ndiye kirusi mwenyewe,huyo ndiyo wale wenye kinyongo na Mama wanamtengenezea shoti kumchonganisha na Watanzania
 
Yule jamaa alikuwa akikatiza madongo paromoko wananchi wakimwambia nguzo zinapita tu lakini atuoni umeme au sijui tunatozwa bei ya mjini wakati huku ni vijijini.

Kinachofuata ni mawili wewe ebu mpigie Kalemani au kama hana muda salamu zake ni ‘message sent and delivered kwa wahusika’.

Kesho yake watatoka huko walipo na makamera uwaone kwenye eneo, mawili either wanatoa ufafanuzi au wanatatua changamoto.

Iweje leo watu wale wale hawana muda. Mama lazima atoe mfano hivi karibuni wa kutimua mtu kutokana na kero za wananchi na Kalemani ndio fursa yenyewe.
 
Mkuu makampuni binafsi yalishaalikwa miaka ya nyuma, ilishindikana kutokana na makampuni hayo kutaka kuzalisha tu umeme kisha yaiuzie TANESCO ndio isambaze.

Kwa kifupi hayataki gharama na hasara zinazotokana na kusambaza Kwa wateja
Nimeona baadhi ya Nchi unakuta kuna makampuni zaidi ya mawili na yote yanatumia waya zilezile tofauti ni Software tu unaungiza kadi ya kampuni umeme unawaka

Hata Kenya tu wana Kengen na Kenya Power and lighting
 
Ndani ya mwezi mmoja mifumo ya tra,tpa na tannesco imekua down kwa kipindi flan.hili swala ni nadhani ni hujuma kwa mama au kulikua na hujuma sasa wanaweka mambo sawa.
 
Muarobaini wa Umeme ni kuruhusu Makampuni Binafsi kama kwenye Simu
Kakuongopea nani?

Kama tutaacha kila kitu kuhusu nishati ya umeme kwa sekta binafsi kuna uwezakano na hata jeshi mbele ya safari tutaliacha kwa sekta binafsi, waza na fikiri kitatokea nini?
 
Mawaziri wengi wanasahau kuwa ni wanasiasa na sio watendaji. Wao wanasimamia policy issues na sio management issues. Sasa waziri anajiona yeye ni Katibu Mkuu, Chairman of the Board na Managing Director kwa pamoja. Waziri angewaita Katibu Mkuu, Mwenyekiti wa Bodi na Mtendaji Mkuu wa Tanesco na kuwataka wamueleze nini kimesababisha tatizo. Baada ya hapo ndio angetoa tamko linaloeleweka.

Waziri kuwashughulikia hivyo vidagaa ni kujidhalilisha. Yeye saizi yake ni MD ambae kama angegundua ni kimeo angemshauri aliyemteua ampe adhabu anayostahili. Na kama makosa ni ya waliokuwa chini yake angemuagiza achukue hatua zinazostahili. Tatizo ni kuwa utendaji wa namna hii hauwezi kuufanya mbele ya kamera. Wao wanataka waonekane wanafanya kazi hata kama hamna kitu wanachofanya. Hayuko peke yake mwenye hulka hii.

Amandla...
 
Kakuongopea nani?

Kama tutaacha kila kitu kuhusu nishati ya umeme kwa sekta binafsi kuna uwezakano na hata jeshi mbele ya safari tutaliacha kwa sekta binafsi, waza na fikiri kitatokea nini?
Mbona kuna Nchi za wenzetu wameweza bila bila kubifsisha Jeshi hoja yako haina mashiko
 
Huogopi kuitwa yale majina.
haya shauri yako, waache wampotoshe mama,watamwambia amfukuze.Hii wizara inahitaji mtu msafi kama huyu.Maana mawaziri wengi waliliwa vichwa.
 
Atoke tu huyo Kalemani, Kwanza anatokea Chato, Atokeee
 
Medard aondolewe ikiwezekana ashtakiwe, hawezi kututesa hadi kisamvu kimeoza leo unamtetea, The Boss nakuheshimu why unatetea uzembe?
 
Mawaziri wengi wanasahau kuwa ni wanasiasa na sio watendaji. Wao wanasimamia policy issues na sio management issues. Sasa waziri anajiona yeye ni Katibu Mkuu, Chairman of the Board na Managing Director kwa pamoja. Waziri angewaita Katibu Mkuu, Mwenyekiti wa Bodi na Mtendaji Mkuu wa Tanesco na kuwataka wamueleze nini kimesababisha tatizo. Baada ya hapo ndio angetoa tamko linaloeleweka.

Waziri kuwashughulikia hivyo vidagaa ni kujidhalilisha. Yeye saizi yake ni MD ambae kama angegundua ni kimeo angemshauri aliyemteua ampe adhabu anayostahili. Na kama makosa ni ya waliokuwa chini yake angemuagiza achukue hatua zinazostahili. Tatizo ni kuwa utendaji wa namna hii hauwezi kuufanya mbele ya kamera. Wao wanataka waonekane wanafanya kazi hata kama hamna kitu wanachofanya. Hayuko peke yake mwenye hulka hii.

Amandla...
Shida kubwa ya shirika la umeme TANESCO iko hapa 0689877735.
 
Pamoja na mapungufu yake Waziri Kalemani bado ana vision sahihi ya umeme nafuu Kwa Watanzania.

Kampeni ya kumchafua na kumshambulia ikemewe kwa nguvu zote.

Kuna madadali wa kununua umeme wa gesi wameanza kampeni ya kumchafua na kumchomekea Mama wale matapeli wa zamani

Kama Professa Muhongo na Ngeleja ili ili waanze upigaji tena.

Anapenda kupiga kelele kukishatokea tatizo An approach to crisis management by Murphy's Law: Nothing is as easy as it looks, everything takes longer than you expect and if something can go wrong it will at worse
 
Pamoja na mapungufu yake Waziri Kalemani bado ana vision sahihi ya umeme nafuu Kwa Watanzania.

Kampeni ya kumchafua na kumshambulia ikemewe kwa nguvu zote.

Kuna madadali wa kununua umeme wa gesi wameanza kampeni ya kumchafua na kumchomekea Mama wale matapeli wa zamani

Kama Professa Muhongo na Ngeleja ili ili waanze upigaji tena.
Mkuu hakuna anayemchafua bali amejichafua mwenyewe, kachukua muda mrefu sana kutatua tatizo la mfumo wa umeme, kabaki kufoka tu kwenye runinga ili aonekana anafanya kazi, umeme umekuwa ni kero kwanza unakatika mara kwa mara na yeye akiwa mwenye dhamana hatujui anafanya nini, kazi yake sio kusimamisha tu mameneja kwa siku 10 naye asimamishwa wizara imemshinda, tumepata hasara sana vifaranga vyetu sisi wanyonge vimekufa vyote sababu ya kukosa huduma ya umeme. Kiongozi unatakiwa uwe mbunifu, kawa waziri wa nishati kwa muda mrefu ilitakiwa aelekeze nguvu zake kwenye shirika muhimu ambalo ni roho ya uchumi, leo anauliza plan B baada ya kutokea tatizo ina maana siku zote alikuwa wapi kuwataka Tanesco wawe na plan B pia anashangaza anauliza eti huu mfumo unathibitiwa nje na kutoa maamuzi kuwa kuanzia mwakani kila kitu kifanyike hapahapa, je ina maana siku zote alikuwa anafanya nini,je alikuwa hajui matatizo/madhara ya mfumo wa shirika muhimu kama umeme kudhibitiwa kutoka nje? Kalamani kajichafua mwenyewe na kibarua kimemshinda.
 
Back
Top Bottom