Waziri Medard Kalemani asiondolewe Wizara ya Nishati

Waziri Medard Kalemani asiondolewe Wizara ya Nishati

Pamoja na mapungufu yake Waziri Kalemani bado ana vision sahihi ya umeme nafuu Kwa Watanzania.

Kampeni ya kumchafua na kumshambulia ikemewe kwa nguvu zote.

Kuna madadali wa kununua umeme wa gesi wameanza kampeni ya kumchafua na kumchomekea Mama wale matapeli wa zamani

Kama Professa Muhongo na Ngeleja ili ili waanze upigaji tena.
Analijua hili?

Mkuu hii kuna nchi ili jaribu matokeo yake bei ya umeme ilipanda sana hadi ikawa haishikiki. Ikiletwa hapa hilo pia linaweza kutokea na watu kuamua kurudi kwenye vibatari.
Mkuu, Monopoly huwa inasababisha watu wawe wazembe
 
  • Nzuri
Reactions: BAK
Mawaziri wengi wanasahau kuwa ni wanasiasa na sio watendaji. Wao wanasimamia policy issues na sio management issues. Sasa waziri anajiona yeye ni Katibu Mkuu, Chairman of the Board na Managing Director kwa pamoja. Waziri angewaita Katibu Mkuu, Mwenyekiti wa Bodi na Mtendaji Mkuu wa Tanesco na kuwataka wamueleze nini kimesababisha tatizo. Baada ya hapo ndio angetoa tamko linaloeleweka.

Waziri kuwashughulikia hivyo vidagaa ni kujidhalilisha. Yeye saizi yake ni MD ambae kama angegundua ni kimeo angemshauri aliyemteua ampe adhabu anayostahili. Na kama makosa ni ya waliokuwa chini yake angemuagiza achukue hatua zinazostahili. Tatizo ni kuwa utendaji wa namna hii hauwezi kuufanya mbele ya kamera. Wao wanataka waonekane wanafanya kazi hata kama hamna kitu wanachofanya. Hayuko peke yake mwenye hulka hii.

Amandla...

Mkuu ulichoongea Uko sahihi kabisa...Ila Kumbuka Kilichotokea kina Impact sana Kisiasa...yaani Wananchi walishafura..
Hivyo hatua Alioichukua Politically iko OK...
Ila Kinyume chake haipo ok!
So lazima Acheze na Mlio wa ngoma ulivyo huu ndo ukweli mchungu hata kama Utaukataa...Yeye kaangalia Political effects kwake sio kwako wewe...over.
 
Narudia tena na tena, merdard kalemani,Doto biteko,Dr Dorothy Gwajima,Prof Ndalichako, mganga mkuu wa serikali, sio msaada kwa sasa kwenye serikali ya awamu ya Sita . Kuna vijana wadogo wenye uwezo kuliko lini kundi ambalo kwa sasa wamekata tamaa tangu 17.3.2021.

Mi nasema hivi Kalemani Abakie mpaka Amalize Stiegliers gorge kwanza...
Baada ya Hapo ndio waje wengine...
 
hivi ni kipi kinashindikana katika kuleta makampuni binafsi ya kufua,kusambaza na kucharge umeme.?

je kuna athari gani kama nchi tukifanya hvyo?
 
Umefika wakati wa Tanesco kupata mshindani, haya yote tunayoyaona sasa yanasababishwa na ukiritimba wa Tanesco kuhodhi kila kitu.

Ndio maana wanatokea hao wajanja wanataka kumuharibia Waziri kama unavyosema japo sina hakika.

Miaka yote Tanesco imekuwa inaendeshwa kwa hasara na kutoa huduma mbovu licha ya kuwa shirika pekee linalotoa nishati ya umeme nchini tena bila upinzani.
Tatizo ni mfumo wa kiurasimu wa utoaji umeme. Tanesco apewe kazi moja tu ya production na distribution wafanye wengine. Vinginevyo Waziri yuko vizuri sana mbali na njama za kumchafua sababu za siasa za umeme na mafuta we know it.
 
Hivi wewe huwa una akili kweli, au shule mgogoro
Hivi why una attack hivyo we unapimaje akili ya mtu we una tatizo kama kweli hujaona hoja ya si uulize pata muda utafakari
 
Pamoja na mapungufu yake Waziri Kalemani bado ana vision sahihi ya umeme nafuu Kwa Watanzania.

Kampeni ya kumchafua na kumshambulia ikemewe kwa nguvu zote.

Kuna madadali wa kununua umeme wa gesi wameanza kampeni ya kumchafua na kumchomekea Mama wale matapeli wa zamani

Kama Professa Muhongo na Ngeleja ili ili waanze upigaji tena.
Mimi naona nibora atimuliwe tu kwani toka aondoke jiwe kigoma umeme unakatika sana baki ukitoa 50 unapata unit 14 tu kwanini ametuweka kwenye matumizi makubwa hatahivyo unit zinakimbia ilemvaya wakati natumia taa za wat5 zipo 3 na 2 nazima wakati wakulala lakini hadi nauona umeme kama anasa tu
 
Umefika wakati wa Tanesco kupata mshindani, haya yote tunayoyaona sasa yanasababishwa na ukiritimba wa Tanesco kuhodhi kila kitu.

Ndio maana wanatokea hao wajanja wanataka kumuharibia Waziri kama unavyosema japo sina hakika.

Miaka yote Tanesco imekuwa inaendeshwa kwa hasara na kutoa huduma mbovu licha ya kuwa shirika pekee linalotoa nishati ya umeme nchini tena bila upinzani.
Likiamua kupata faida, tutaiweza bei ya umeme?.
 
Back
Top Bottom