Fundi Mchundo
Platinum Member
- Nov 9, 2007
- 10,448
- 8,705
Nakumbuka wakati tuna shirika linaitwa Tanzania Posts and Telecommunications Corporation. Hawa mabwana ndio walikuwa wana monopoly ya simu. Ilikuwa ukitaka simu lazima uhonge sana na pamoja na hayo utasubiri miezi kadhaa ndio wakufungie. Aidha, ikija bili yao mwisho wa mwezi utakoma maana utaambiwa una mtindo wa kuwapigia ndugu zako wanaoishi sayari ya Mars. Simu ilikuwa bidhaa adimu ambayo waliyoimudu walikuwa watumishi wa umma ambao simu zao za Mars zilikuwa zinalipiwa na serikali. Leo mrithi wake yuko ICU kwa sababu anashindwa kushindana na wakina Voda ambao gharama zao zilikuwa nafuu mpaka pale serikali ilipowageuza shamba la bibi kwa kuongeza kodi, masharti ambayo ni usumbufu kwa wateja wake ( mtu asiwe na lakini zaidi ya moja n.k.). Wengine ndio hao wameamua kufungasha.Ni kweli Mkuu lakini walafi pia wakiruhusiwa hili wataweka bei za juu ili wapate profit ya 90% baada ya kuondoa gharama zao matokeo yake umeme utakuwa very expensive kwa Watanzania wengi sana.
Tulikuwa na kampuni moja ya kutengeneza bia. Wakati huo tulikuwa tunanunua bia kwa kibali ns na chaguo peke yake ulilokuwa nalo lilikuwa ni kati ya Safari ya moto au baridi. Mameneja wa TBL walikuwa wanakunywa bia bure bar kwa sababu mwenye bar alitaka uhakika wa kupata bia. Leo wanafanya promotion za kubembeleza wateja kwa sababu hawako peke yao.
Kuna wakati kupata tiketi ya ndege ilikuwa kwa mbinde. Na hata kuwa na tiketi hakukuwa guarantee ya kusafiri maana boarding pass zilikuwa zinatolewa kwa upendeleo na priority ya kusafiri ilikuwa watumishi wa umma na wafanya biashara wakubwa. Ilikuwa si ajabu kuambiwa ndege imejaa lakini ukiingia unakuta viti vingi viko wazi. Wakaja wakina Fast Jet na tukapata uwezo wa kuwanunulia tiketi bibi zetu ili wapande ndege kabla mwenyezi Mungu hajawachukua. Tukawafanyia figisu wakaondoka. Leo tumerudi kupanda mabasi. Ambayo nayo karibu yatatushinda kwa sababu serikali imetaka kuwaingilia jinsi wanavyokata tiketi.
Mifano iko mingi tu ya jinsi monopoly inavyotugharimu. Ushindani ukiruhusiwa Tanesco utatuletea nafuu ili mradi serikali itakuwa makini kuwasimamia kwa haki ( kuzuia makubaliano ya bei angamizi) na kutowavisha mzigo wa kodi usiobebeka.
Soko huria sio adui yetu. Mbaya wetu ni yule anaewaza kukamua tu bila kuhakikisha kuwa wanaweza kufanya biashara kwa faida yao na ya wateja wake.
Amandla...