Msimshangae kukosea kuongea kiingereza.....kwa maana yeye si muingereza ni mtanzania ambayo lugha yake mama ni kiswahili....
halafu musijikie unyonge kushindwa kuongea kiingereza....maana hiyo siyo lugha yako....lugha yako ni kiswahili.....vivyo hivyo usijisikie fahari kama unajua kiingereza maan pia hiyo siyo lugha yako......
nasema hivi kwa kuwa ukienda uingereza ukimkuta mtu anaongea kiswahili kibovu wala hataona haya......au hata akiongea kiswahili kizuri hawezi jisifia......hali hiyo ni tofauti na kwetu kwa sababu bado akili zetu ziko kwenye ukoloni.....bado tunatawaliwa vibaya sana kifikra.....huo ni ukoloni mbaya sana.....ukoloni ambao kuutoa akilini ni ngumu sana kuliko kumfukuza mkoloni mwenyewe...... Nakumbuka baba wa Taifa aliwahi sema....''KUJUA LUGHA YA BWANA MKUBWA YAANI MKOLONI NI FAHARI'' hilo ndilo lililopo sasa.....watu wengi wakiongea kiingereza wanahisi ufahari.....sababu ni lugha ya mtawala..... Waziri Ghasia angekosea kuongea lugha ya kimatumbi au kichebha au kihehe au kihaya au kiha hakuna mtu ambaye angediriki kusema lolote au hata wewe Mkeshaji usinge anzisha hii mada......
Mwisho.....ni kuwa ukiwa unaongea kiingereza ambacho si kizuri haina haja yakufadhaika maana hiyo si lugha yetu...... na hata kama tunajifunza shuleni katika ngazi zote za elimu bado suala.....ni mazingira ya lugha (linguistic environment) si mazuri (conducive) kwa lugha ya kiingereza..... maana kiingereza kinatumika ndani ya darasa na baada ya hapo hamna...... na pia baada ya kumaliza shule mfano daktari... akirudi kwenye jamii anatibu watu ambao wanaongea lugha ya kiswahili..... hivyo kiingereza kinaishia darasani..... hilo linatokea kwa wanasheria, maafisa kilimo, wahandisi nk. hivyo kiingereza hakitakua kwa sababu hizo tajwa....
mimi binafsi najisikia faraja sana nikimsikia mtu ambaye anaeleza mikakati ya kukuza lugha yetu ya kiswahili.....lugha ambayo inakua kwa kasi duniani....