Waziri Menejimenti ya Utumishi wa Umma: Lugha ya malkia Elizabeth, mhhhhh!

Mkuu tutake radhi walimu, mbona sisi lugha inapanda vizuri tu, tena ndio tunayoitumia kufundishia darasani.
Labda kama Lukuvi ni katika wale walimu wa UPE ''Ualimu Pasipo Elimu''.

Mkuu PF sorry sikumaanisha kwamba waalimu hamjui kiingereza la hasha mko poa infact ndio maana mmeweza kutufundia tukakijua japo kidogo. Nilichomaanisha ni kwamba ukiwa na watu wawili mmoja ana diploma na mwingine ana MSc katika hali ya kawaida unatarajia huyu mwenye MSc awe fluent zaidi. Ni hicho otherwise vidole juu kwa ajili ya waalimu wote wa watanzania ambao maslahi ni madogo sana ilihali mazingira ni magumu kuliko maelezo lakini bado mnafanya kazi nzuri sana.
 

... nimeiona jana na imeniacha hoi. Jamani huu si ushabiki wa kichama. Huyu mdada ni Waziri wa nchi yangu na ni lazima nijisikie kichefuchefu ati leo hii mtu anayejiita msomi anashindwa kilugha chepesi kama kiingereza. Mbinu za kujifunza na kujiendeleza zipo kibao. Lazima tumshangae na tusikitike. Kwani hiyo Masters degree yake ameipataje bila kujua lugha tajwa? Na huyo aliyemteua bana!
 

Hiyo pia ni hoja. Iweje waziri tena mwenye masters anaongea vibaya kuliko hata mtoto wa chekechea. Presentation alifanyaje? Au masters yake ndo kama zile za mh. jk?
 
Jaribu kujua unachochangia. Unaposema hotuba alitayarishiwa na wasaidizi wake ndiyo maana hakuisoma fluently ni ujinga. Hujui kuwa hotuba zote huwa zinatayarishwa na wasaidizi? Mtu mwenye akili huwa anatayarishiwa na kuipitia mapema sana na kuifanyia mazoezi ya kuisoma. Hivi ndivyo ulimwengu wa hotuba unavyofanya kazi, huyo mpuuzi hajui Kiingereza wa nidhamu ya hotuba.
 

Msimshangae kukosea kuongea kiingereza.....kwa maana yeye si muingereza ni mtanzania ambayo lugha yake mama ni kiswahili....
halafu musijikie unyonge kushindwa kuongea kiingereza....maana hiyo siyo lugha yako....lugha yako ni kiswahili.....vivyo hivyo usijisikie fahari kama unajua kiingereza maan pia hiyo siyo lugha yako......

nasema hivi kwa kuwa ukienda uingereza ukimkuta mtu anaongea kiswahili kibovu wala hataona haya......au hata akiongea kiswahili kizuri hawezi jisifia......hali hiyo ni tofauti na kwetu kwa sababu bado akili zetu ziko kwenye ukoloni.....bado tunatawaliwa vibaya sana kifikra.....huo ni ukoloni mbaya sana.....ukoloni ambao kuutoa akilini ni ngumu sana kuliko kumfukuza mkoloni mwenyewe...... Nakumbuka baba wa Taifa aliwahi sema....''KUJUA LUGHA YA BWANA MKUBWA YAANI MKOLONI NI FAHARI'' hilo ndilo lililopo sasa.....watu wengi wakiongea kiingereza wanahisi ufahari.....sababu ni lugha ya mtawala..... Waziri Ghasia angekosea kuongea lugha ya kimatumbi au kichebha au kihehe au kihaya au kiha hakuna mtu ambaye angediriki kusema lolote au hata wewe Mkeshaji usinge anzisha hii mada......

Mwisho.....ni kuwa ukiwa unaongea kiingereza ambacho si kizuri haina haja yakufadhaika maana hiyo si lugha yetu...... na hata kama tunajifunza shuleni katika ngazi zote za elimu bado suala.....ni mazingira ya lugha (linguistic environment) si mazuri (conducive) kwa lugha ya kiingereza..... maana kiingereza kinatumika ndani ya darasa na baada ya hapo hamna...... na pia baada ya kumaliza shule mfano daktari... akirudi kwenye jamii anatibu watu ambao wanaongea lugha ya kiswahili..... hivyo kiingereza kinaishia darasani..... hilo linatokea kwa wanasheria, maafisa kilimo, wahandisi nk. hivyo kiingereza hakitakua kwa sababu hizo tajwa....

mimi binafsi najisikia faraja sana nikimsikia mtu ambaye anaeleza mikakati ya kukuza lugha yetu ya kiswahili.....lugha ambayo inakua kwa kasi duniani....
 

Kwa nini alazimishe kuongea kiingereza wakati walengwa wakuu ni wananchi wa Tanzania ambao wengi wetu hatuielewi lugha hiyo. Hata hivyo alikuwa Tanzania na sio Uingereza iweje aongee lugha hiyo..? Kulikuwa na ulazima gani?
Suala hapa ni kuwa alitaka kuonesha ufahari (kama ambavyo umesema huko juu kuwa mtanzania akiongea kiingereza ndo anajisikia fahari) matokeo yake akaishia kwenye aibu.
 
Wacha matusi ndugu yangu, sioni sababu ya kuniita mjinga. Nilichaongea ni kwamba lugha ambayo haipo kwenye utamaduni wako(culture) nilahisi kuikosea na kwa hotuba iliyotayarishwa na mtu mwingine sio ajabu kukosa 'fluency' ktk kuisoma. Sasa cha ajabu nini mpaka unanitukana? "Who told you that being compentant and conversant in foreign language is synonymous to intellegence?" wacha hizo, sio uugwana kuwatukana watu unaotofautiana nao mitazamo. Na wala hukuwa na sababu yoyote ya kumuita mtu ati ni mpuuzi kwa sababu kwa mtazamo wako hajui kiingereza. Jiulize wewe mwenyewe unaijua lugha hiyo kwa kiwango gani kiasi cha kuwadharau wengine kiasi hicho. Basi changia hoja kwa kiingereza tuuone umahiri wako hapa.
 
Kumbe ulivamia kitu usichokijua. tehe tehe tehe.
Walengwa walikuwa wananchi, sasa ni asilimia ngapi ya wananchi wanaijua lugha hiyo achilia mbali kuwa aliboronga hata kama angeongea barabara. Acha kudandia kijana, utaumia.
Nini kitaniumiza? huu utumwa wako wa kiakili wa kukumbatia lugha ya watawala na kuona wanao ikosea ni wakulaumiwa? Mimi nilidhani usingelaumu ubovu wa kiingeza cha mama Ghasia kana kwamba ni dhambi, labda ungenyapalia "audience" walengwa wa hotuba. Lakini hata hiyo sio hoja ya msingi kwani walikuwepo wageni kutoka nje ambao walihitaji kusikiliza na kuielewa hotuba hiyo.
 

Pumbavu kabisa wewe!
Hao wageni ni asilimia ngapi ya watanzania wote? Kama ilikuwa ni kwa ajili ya hao wageni si angewafata huko makwao?
Usitake kupindisha nilichomaanisha. Hoja hapa ni kwa nini alazimishe kuongea lugha hiyo hali walengwa wengi hatuielewi lugha hiyo? Ni wazi kuwa alitaka kujionesha kuwa na yeye yumo. sasa unapotaka kuonesha ufahari inabidi uwe unajua kweli, huyu bibiye ilikuwa ni kinyume. Upo hapo bibiye Hawa Ghasia?
 

Hapo pekundu...Sisi tulitarajia aimudu lugha ya Kiingereza kwa kuwa alifundishwa shuleni na si kuijua mitaani na aliifanyai mitihani ambayo tunaamini alipasi...kuthibitisha intelijensi yake...na kila mara mkazo wa watu kutoharibu hii lugha ni kwa sababu tunaelewa watu wamefundishwa na kutahiniwa....sasa ukikuta mtu ana masters halafu lugha hovyo manake nini? ni intelligent huyo kweli?
 
tatizo lugha yetu hatuithamini tunaamini ya wenzetu lakini tungali inatushinda
 
yanini kujilazimisha kama lugha haipandi? aliyemkataza asihutubie kwa kiswahili nani? ameyataka mwenyewe maaibu hayo

Lugha aliyotumia jana kuwasilisha bajeti ya wizara yake bungeni ndiyo alipaswa kuitumia siku hiyo ya sherehe, lakini yeye alijifanya kuleta mashauzi. Mbona jana kaongea lugha ya taifa (japo kwa kizenji) lakini watu tumemwelewa. Alishindwa nini kufanya hivyo siku hiyo....?
 
Hiyo pia ni hoja. Iweje waziri tena mwenye masters anaongea vibaya kuliko hata mtoto wa chekechea. Presentation alifanyaje? Au masters yake ndo kama zile za mh. jk?

Ndugu yangu afadhali angekuwa anaongea,alishindwa kusoma kilichokwisha andikwa kwenye karatasi ya hotuba.Sijawahi ona kitu kama cha siku ile.
 
Ndugu yangu afadhali angekuwa anaongea,alishindwa kusoma kilichokwisha andikwa kwenye karatasi ya hotuba.Sijawahi ona kitu kama cha siku ile.
ilikuwa aibu,yule omera wa kenya alikuwa anachana lugha as if kazaliwa royal palace.mh waziri wetu alishindwa hata kusuma jamani.hizi masters za wanamagamba nina shaka nazo.alitia aibu.
 
Jamani tusimsakame sana huyu Dada kuhusu lugha ya Kiingereza, ilo ni tatizo la Taifa, mfano kidogo tu hii thread tuigeuze kuwa ya Kingereza tuone kama kuna mtu atabakia humu, tutabaki wachache
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…