Waziri Mhagama Akagua Ujenzi wa Hospitali ya Halmashauri ya Wilaya ya Handeni

Stephano Mgendanyi

JF-Expert Member
Joined
May 16, 2020
Posts
2,833
Reaction score
1,301

Waziri Mhagama Akagua Ujenzi wa Hospitali ya Halmashauri ya Wilaya ya Handeni

Waziri wa Afya Mhe. Jenista Mhagama Februari 22, 2025 amefanya ziara ya kukagua miundombinu pamoja na huduma zinazotolewa katika Hospitali ya Halmashauri ya Wilaya ya Handeni (Mkata) Mkoani Tanga inayotarajiwa kuzinduliwa rasmi kesho Februari 23, 2025 na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan.

Miongoni mwa wodi alizotembelea na kuzikagua Waziri Mhagama ni pamoja na wodi ya wazazi, mama na mtoto, wodi ya watoto wachanga, wodi ya huduma za dharura pamoja na huduma zinazotolewa katika jengo la wagonjwa wa nje (OPD).

Waziri Mhagama ameambatana na timu kutoka Wizara ya Afya akiwemo, Mkurugenzi wa Huduma za Tiba Dkt. Hamad Nyembea pamoja na Kaimu Mkurugenzi wa Sera na Mipango Bw. Tumainiel Macha.
 
Attachments

  • GkZeMDtXgAAGEfp.jpg
    GkZeMDtXgAAGEfp.jpg
    142.3 KB · Views: 1
  • GkZeMDlXIAArsZd.jpg
    GkZeMDlXIAArsZd.jpg
    149.2 KB · Views: 1
  • GkZeMDtXEAA0gnH.jpg
    GkZeMDtXEAA0gnH.jpg
    108.9 KB · Views: 1
  • GkZeMDnXoAEBWIp.jpg
    GkZeMDnXoAEBWIp.jpg
    101.4 KB · Views: 1
  • GkZeNMoWwAIc61n.jpg
    GkZeNMoWwAIc61n.jpg
    125.3 KB · Views: 1
  • GkZeNMoWMAAKQDV.jpg
    GkZeNMoWMAAKQDV.jpg
    191.1 KB · Views: 1
  • GkZeNMsW4AAPzbs.jpg
    GkZeNMsW4AAPzbs.jpg
    153.7 KB · Views: 1

Waziri Mhagama Akagua Ujenzi wa Hospitali ya Halmashauri ya Wilaya ya Handeni

Waziri wa Afya Mhe. Jenista Mhagama Februari 22, 2025 amefanya ziara ya kukagua miundombinu pamoja na huduma zinazotolewa katika Hospitali ya Halmashauri ya Wilaya ya Handeni (Mkata) Mkoani Tanga inayotarajiwa kuzinduliwa rasmi kesho Februari 23, 2025 na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan.

Miongoni mwa wodi alizotembelea na kuzikagua Waziri Mhagama ni pamoja na wodi ya wazazi, mama na mtoto, wodi ya watoto wachanga, wodi ya huduma za dharura pamoja na huduma zinazotolewa katika jengo la wagonjwa wa nje (OPD).

Waziri Mhagama ameambatana na timu kutoka Wizara ya Afya akiwemo, Mkurugenzi wa Huduma za Tiba Dkt. Hamad Nyembea pamoja na Kaimu Mkurugenzi wa Sera na Mipango Bw. Tumainiel Macha.
Tawala za Afrika ni za ajabu Sana.
Hivi amekosekana kabisa Daktari wa Afya ya Binadamu (MD) hadi ameteuliwa huyu Mtu ambaye Hana kabisa taaluma yoyote ile kuhusiana na masuala ya Afya ya binadamu ili kuongoza Wizara ya Afya?
 
Siyo lazima Waziri by professional awe amesomea hicho kitu. Ila Katibu Mkuu wa Wizara ndiyo lazima awe by professional amepitia huko maana yeye ni Mtendaji. Waziri, RC, DC ni political position ila Katibu Mkuu, DED, DAS, Mkurugenzi wa Taasisi hawa ni watendaji.
 
Kenya Development Budget of sh 4,791,772,950,556.28

Tanzania Development Budget of Sh 1,419,843,057,000
 
Tawala za Afrika ni za ajabu Sana.
Hivi amekosekana kabisa Daktari wa Afya ya Binadamu (MD) hadi ameteuliwa huyu Mtu ambaye Hana kabisa taaluma yoyote ile kuhusiana na masuala ya Afya ya binadamu ili kuongoza Wizara ya Afya?
Hoja ya kipumbavu sana hii

Waziri Lazima awe mwanataaluma?

Halafu katibu mkuu awe nani?

This is a very stupid idea… what we need is a competetent person siyo a medical person
 
Back
Top Bottom