Waziri mkenda adhibitiwe au apuuzwe

Waziri mkenda adhibitiwe au apuuzwe

Madibira 1

JF-Expert Member
Joined
Jan 6, 2023
Posts
358
Reaction score
831
Huyu waziri tangu anaingia madarakani amekuja na Mambo ya ajabu ajabu sana na mengi hayaeleweki. Baadhi ya Mambo hayo ni mabadiriko ya mtaala wa elimu kuanzia msingi mpaka sekondari, mabadiriko ya mfumo wa upatikanaji wa walimu na mabadiriko ya sera ya elimu.

Niache mengine na kuzungumzia hili la mabadiriko ya mfumo wa upatikanaji wa walimu. Kwamujibu wa maelezo yake ni kuwa walimu watalazimika kufanya mtihani wa mchujo Ili kupata ajira. Huyu waziri ukimuuliza atakujibu kuwa hata wao miaka hiyo walipita Kwa mfumo huo, yaani mfumo wa miaka ya 1980s uutumie Leo 2020s seriously!

Mwalimu amehitimu mafunzo ya chuo kikuu mwaka 2015 yaani miaka 8 iliyopita a serikali hamjampa ajira Leo apige paper Kwa material yepi? Yale aliyosoma miaka 8 iliyopita au atapewa muongozo mwingine?

Kama kutakuwa na mtihani wa ajira je kule vyuoni mitihani itaondolewa au nayo utakuwepo? Kama itakuwepo je, itakua ni ishara ya serikali kutovuamini vyuo vya ualimu nchini?

Hivi wizara ya elimu hawakujifunza jambo kupitia mtihani wa wanasheria? Ile ni ishara kuwa watu wakishamaliza vyuo hujichanganya na Mambo yasiyo ya kitaaluma na kuwapigisha paper ni kama kuwanyima kazi. Kama serikali haitaki kuajiri isemw na sio kuja na hoja za mitihani, kwasababu wengi watakosa kwa kigezo Cha kufeli na utahoji wapi? Je wale wanaopita mkato na kupewa alama tu watadhibitiwaje? Vipi kwenye masomo ya mkakati ambayo hata walimu hawatoshi (hesabu na physikia) nao watapiga paper au litatuhusu wazee wa Australopithecus na vishazi huru.

Niombe huyu waziri adhibitiwe namatamko yake asifikiri ni sifa au tunampenda sana. Kama hoja yake inatolewa Ili kuzima jambo Fulani sawa lakini Kama yupo serious adhibitiwe. Mwenzake nae alitoa matamko na juzi kadhibitiwa na nchi imetulia. Kama wizara inamshinda aachie ngazi na sio kututisha.
 
Elimu yenyewe ya kukariri ili tusipate sup na mbaya zaidi tulichagua ualimu ili tupate mkopo LOAN Board alafu mje mtupe mitihani nyie vichaa kweli aisee
 
Mbona nyie kuingia kufanya wizara ya elimu n utamaduni hamjapewa mitihani au na yeye tumtungie mtihani wa UWAZIRI
 
Mtajua hamjui[emoji2][emoji2][emoji2][emoji2][emoji2]kafanyeni Pepa hilooo
 
Umepanic kama na wewe ni mmoja wa wasaka hiyo ajira,
Anyway
Kumaliza elimu ya ualimu na kufaulu mitihani vyuoni hakukufanyi wewe kuwa mwalimu Bora ama unaweza kufundisha,
Kufanyishwa mtihani ni sahihi kabisa,mbona kada nyingine wanafanya na hawalalamiki
Ualimu usiwe kigezo Cha kumpa Kila aliehitimu kazi,bali wanaostahili na wenye kuweza wakafundishe, shule zinazofanya vizuri zote waalimu wake wamepitia interviews tena ngumu.
Tena angeongeza na practical zisizopungua tatu maana tunawapa dhamana ya kulea na kufundisha watoto wetu kwa muda mrefu sana
 
  • Thanks
Reactions: Eco
mmm kazi ipo.sasa si hiyo mitihani wapeleke vyoni huko au hata vyuo hawaviamin.mbona naona jambo jepesi tu.
 
Back
Top Bottom