Waziri Mkenda asema ufaulu somo la hisabati ni janga linalotakiwa kutafutiwa ufumbuzi

Waziri Mkenda asema ufaulu somo la hisabati ni janga linalotakiwa kutafutiwa ufumbuzi

peno hasegawa

JF-Expert Member
Joined
Feb 24, 2016
Posts
14,255
Reaction score
23,949
Ninapata shida kidogo kuhusu kauli ya Prof Mkenda.

Wanaofaulu somo la Hisabati wanaajiriwa wapi?

Somo la hisabati linawasaidia nini wansfaulu kama wanashindwa kujiajiri na kuajiriwa?

Prof Mkenda, kwa ufahamu wako mkubwa tambua kuwa walimu wanao fundisha somo la Hisabati Form four walifeli Hisabsti na ndio walimu walio ajiri na wizara yako.

Ushauri wa bure, fanya utafiti wa walimu wanao fundisha hisabati wao walifaulu hilo somo?
 
Wanajua kutunga mitihani ya Hisababti lakini kufundisha ni tatizo!!

hatari sana!
 
Mitaalam yenyewe yakizamani mtu unamfundisha mitopic usiyoitumia katika maisha ya nini sasa?
Mitaala kwanza iangazwe sio hesabati tu kila somo hasa masomo ya sayansi.
 
Namna ya kusolve hili tatizo ni kuajiri walimu wengi wasomo husika, maana tumeshuhudia ajira za walimu wa sayansi especially physics zimekuwa nyingi na zimepelekea improvement katika Somo .

Wizara iwaze kuajiri walimu wa Hisabati wengi kuendana na ratio ya namba ya wanafunzi, maana Kuna namba ya walimu Hisabati kubwa ipo mtaaani, Serikali imebase kuajiri walimu tu wa physics ambao wengi hawezi kumudu kufundisha madarasa yote.

Walimu wengi wenye masomo ya Math&Geo, math&ICT, Math& Economic na Mathematics (only) , ajira zinazotolewa mara nyingi haziwaconsider.

NB: napingana na hoja ya mtoa Uzi, walimu Wana qualification, hawakufeli kama wewe unavyodai, bali kulemewa na ratio ya wanafunzi, na kushindwa kufuatilia zaidi mwenendo wanafunzi kwenye Somo husika.(Bora liende)
 
Mtoa mada una uhakika kuwa wanaofundisha hesabu walifeli somo hilo au ndo yaleyale, mwendo wa kukaririshwa upumbavu humu mitandaoni?!!
 
Zamani miaka ya 80, ukifeli sekondari inaenda ualimu! Ilifika mahali ikahalalishwa division 4 ni ualimu!! Sasa aliyefeli anafundishaje? Tuige Ujerumani, anaefaulu vizuri ndiye anaechukuliwa ualimu. Chunguza kwa makini wanaofundisha Kiingereza na hesabu!
 
Tanzania lolote linawezekana, ni nchi ya kufanyiwa majaribio.
 
Ukweli ni kwamba hakuna mtu form 6,aliyepasua A,au B au hata C,alienda kuchukua edctn . Pure math waliofauru vzr A,B au C wamecgukua fani nyngne like engineer,mechanics , statistics n.k, D,E ndo waalimu .

mkitaka kujenga foundation nzr ya somo la hesabu ,basi badirisheni vigezo vya ajira ya ualimu, waigeni German kule waliofauru vizuri zaidi ndo wanapewa koz za ualimu na salary zao ,znakuwa juu .sio huku kwetu mwa. Salary laki 5,mtu aliyepata A pure math ,sahau yy kuja huko kwenye ualimu!
 
Hata mwenye D mbili miaka yetu humkuti kwenye UALIMU maana sifa ya kuingia Muhimbili ilikuwa D mbili ya Biology na Chemistry.

Kikubwa serikali iboreshe maslahi ya walimu kuwavutia wanaopata one na two.
 
Tunamuomba Prof. Mkenda alitazame swala hili kwa weledi wa hali ya juu haswa kuanzia Elimu ya Msingi.

iweje watoto wafundishwe halafu wafeli Hasabati huku wakifaulu masomo mengine?!!
Hili linatokea hapa kwetu Tanzania tu!!!

Je? tatizo ni ufundishaji mbovu au NECTA wanatunga mitihani ambayo sio standard kwa watoto wa Darasa la 7?!

Yote hayo yanapaswa yachunguzwe na ufumbuzi upatikane.
 
Ninapata shida kidogo kuhusu kauli ya Prof Mkenda.

Wanaofaulu somo la Hisabati wanaajiriwa wapi?

Somo la hisabati linawasaidia nini wansfaulu kama wanashindwa kujiajiri na kuajiriwa?

Prof Mkenda, kwa ufahamu wako mkubwa tambua kuwa walimu wanao fundisha somo la Hisabati Form four walifeli Hisabsti na ndio walimu walio ajiri na wizara yako.

Ushauri wa bure, fanya utafiti wa walimu wanao fundisha hisabati wao walifaulu hilo somo?
Mkuu....

Ni wapi huko wanaofundisha somo la hisabati walifeli form four?
 
Kinachonifurahisha watu wote wanaosema walimu wanaofundisha ndoo ni wale waliofeli na ndoo waliowafundisha hao hao ,sasa je kama ilifundishwa na aliefeli wewe si ndoo majanga kabisaaa?,Naomba tukubali kabisaa Tanzania wote waliosoma ni wapumbavuuu wakutupwa kwa kuwa walifundishwa na wamefundishwa na waliofeli.
 
Tatizo namba moja ni uchache wa walimu wa somo la hisabati kwa ngazi zoote za elimu pia Tatizo lipo shule za msingi mwalimu wa grade A aliyepata F ya hesabu ndo anafundisha hesabu. Siku waalimu wa msingi wakiwa na masomo mahususi tatizo litaanza kupungua
 
Nimefundishwa na mwalimu ambaye alipata F ya MATH lakini mimi nilipata A.

Maana hiyo aliipata kwenye mtihani wa form four...shule ya msingi enzi zake alipata A.

Baada ya kwenda form one hawakumkuta mwalimu wa Math hadi wanamaliza form four.!!
 
Uko sahihi kabisa. Hiyo ni case iliyotokea kwako nakubaliana na wewe. Nataka uamini kwamba sijawadharau walimu wa hisabati shule za msingi na sio wote ila wengi wanaolifundisha somo la hisabati kwa level za chini baadhi yao uwezo ni mdogo ama hukabiliwa na majukumu ya ufundishaji makubwa sana kwa sababu ya uchache wao na wanafunzi ni wengi. Hili somo linataka full 100% participatory yaan mwanafunzi afatilie kila hatua kwa makini na baada ya hapo mwalimu nae afatilie vitendo anavyovifanya mwanafunzi. Sasa unakuta mwalimu wa hisabat kwa wiki anavipindi 72 na wanafunzi anahudumia wapo kama elfu 1 yeye yupo peke yake.
 
Back
Top Bottom