Waziri Mkenda awataka DIT waanze kutengeneza vipuri vya vyombo vya moto ikiwemo vya bajaji na pikipiki

Roving Journalist

JF Roving Journalist
Joined
Apr 18, 2017
Posts
3,984
Reaction score
13,760
Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia Profesa Adolf Mkenda ameitaka Taasisi ya Teknolojia Dar es Salaam (DIT) kujitanua zaidi kwa kutengeneza vipuri vya vyombo vya moto ikiwemo vya bajaji na pikipiki.

Ameyasema hayo Januari 28, 2022 Jijini Dar es Salaam wakati alipotembelea Taasisi hiyo ili kujionea shughuli mbalimbali zinazofanywa hapo ambapo amesema tunaweza kukua kiteknolojia kwa kuboresha vitu ambavyo tayari vimeshatengenezwa na nchi nyingine.

"Nimefurahi sana kuona mna kampuni inayosaidia kubiasharisha bidhaa za ubunifu ila niwatake mboreshe kwa kutengeneza vipuri ambavyo vinahitajika sana kama vya bajaji na pikipiki," amesema Prof. Mkenda.

Aidha Waziri Mkenda ameipongeza taasisi hiyo kwa kuwa na kampuni inayosaidia kubiasharisha bunifu mbalimbali na kuwataka DIT kuhamisha ujuzi wa kiteknolojia kutoka nchi nyingine na kuja kuutumia hapa nchini katika uzalishaji wa bidhaa zitakazokidhi mahitaji ya jamii.

"Tunaweza tukaleta nchini kitu ambacho kimezalishwa mfano nchi ya Uturuki kisha tukaangalia uwezekano wa kukitengeneza na kukiuza ndani na nje ya nchi ili kukuza uchumi wetu," amesema Prof. Mkenda.

Katika hatua nyingine Waziri Mkenda ameusisitiza uongozi wa DIT kuendelea kujenga na kukuza ushirikiano na taasisi nyingine hasa za nje ya nchi ili kubadilishana wataalamu watakaosaidia kuendelea kukuza teknolojia nchini.

Kwa upande wake Mkuu wa Taasisi hiyo, Prof. Preksedis Ndomba amesema wamepokea maelekezo hayo na kuahidi kuyafanyia kazi ili kuboresha utendaji wa taasisi hiyo.

IMG-20220129-WA0000.jpg
IMG-20220129-WA0001.jpg
 
Safi sana kwa kuanzia.

Huwa naumia sana ninavyoona nchi imejaa Bajaji na Pikipiki na zote zinatoka Nje ya nchi.

Nimewahi kujiuliza hivi hatuwezi kubadilisha hizi Pikipiki zikawa za matairi matatu tukaacha kuagiza Bajaji?.
 
Kwa nini? fafanua.
Kila lisemwalo na Mwanadamu laweza kuwa la kweli au uongo.
Huyu sio Ndalichako Mkuu. Ni mchaga na ni mbunifu. PhD yake imesimama sio Phd ya akina Doto Biteko
Mkuu hapa siongelei ndarichako au kutoweza kwa huyo unayempa kuwa na Phd, ni wangapi mlikuwa mnawasema humu kuwa na uwezo baadaye kilichotokea au kinachotokea mbona mnaanza kuponda huku mnajificha?.

Mfumo wetu siyo huo wa msomi wa Phd ndiye atafanya mapinduzi kwa sababu ni mchaga au kasoma sijui urusi au Mangapwani NO, kama na wewe ni mchaga na unampigia debe huyo mjombako umechemsha sana, Afrika we`re different from yo` brain thinker, na bahati mbaya hata pale DIT hujawahi kufika au kutembelea baadhi ya vyuo vya ufundi na sayansi uende kukaa au hata kuangalia nini wanachofanya.
 
Inawezekana hata tukaunda za kwetu wenyewe...
Unafanya kuagiza tu engine, gearbox na spares nyinginezo...

Hata haya magari tunayoendesha huundwa na vifaa toka sehemu tofauti...
Kabisa, najua kabisa inawezekana tukiamua.

Tunawatajirisha wengine kizembe sana..ifike mahali tuache kuagiza Bajaji, Pikipiki au yale Maguta.
 
Its all about costs na durability...

Waangalie isije ika-cost twice as much (na haya mambo ya mgao hilo linawezekana) na na ubora wake kuwa robo ya zilizopo sokoni
 
Kabisa, najua kabisa inawezekana tukiamua.

Tunawatajirisha wengine kizembe sana..ifike mahali tuache kuagiza Bajaji, Pikipiki au yale Maguta.

Bongo tunakosa tu viwanda vya kuunda body, yaani vile vya kuunda maumbo au kujenga blocks...
 
Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia Profesa Adolf Mkenda ameitaka Taasisi ya Teknolojia Dar es Salaam (DIT) kujitanua zaidi kwa kutengeneza vipuri vya vyombo vya moto ikiwemo vya bajaji na pikipiki.

Ameyasema hayo Januari 28, 2022 Jijini Dar es Salaam wakati alipotembelea Taasisi hiyo ili kujionea shughuli mbalimbali zinazofanywa hapo ambapo amesema tunaweza kukua kiteknolojia kwa kuboresha vitu ambavyo tayari vimeshatengenezwa na nchi nyingine.

"Nimefurahi sana kuona mna kampuni inayosaidia kubiasharisha bidhaa za ubunifu ila niwatake mboreshe kwa kutengeneza vipuri ambavyo vinahitajika sana kama vya bajaji na pikipiki," amesema Prof. Mkenda.

Aidha Waziri Mkenda ameipongeza taasisi hiyo kwa kuwa na kampuni inayosaidia kubiasharisha bunifu mbalimbali na kuwataka DIT kuhamisha ujuzi wa kiteknolojia kutoka nchi nyingine na kuja kuutumia hapa nchini katika uzalishaji wa bidhaa zitakazokidhi mahitaji ya jamii.

"Tunaweza tukaleta nchini kitu ambacho kimezalishwa mfano nchi ya Uturuki kisha tukaangalia uwezekano wa kukitengeneza na kukiuza ndani na nje ya nchi ili kukuza uchumi wetu," amesema Prof. Mkenda.

Katika hatua nyingine Waziri Mkenda ameusisitiza uongozi wa DIT kuendelea kujenga na kukuza ushirikiano na taasisi nyingine hasa za nje ya nchi ili kubadilishana wataalamu watakaosaidia kuendelea kukuza teknolojia nchini.

Kwa upande wake Mkuu wa Taasisi hiyo, Prof. Preksedis Ndomba amesema wamepokea maelekezo hayo na kuahidi kuyafanyia kazi ili kuboresha utendaji wa taasisi hiyo.

View attachment 2099078View attachment 2099079
Huwezi kutengeneza vipuri vya brand fulani bila ya kuwa na leseni ya mhusika wa hiyo brand.

Mathalani, watengenezaji wa pikipiki wote wapo protected na Patent rights ambayo huwezi kuitumia bila wao kukuruhusu kimkataba .

Ni ngumu sana kupewa patent right za mchina maana wao wenyewe wanategemea kuuza spea tupu.
 
Waanze kutengeneza vijiko vya kulia kwanza

Na uma etc

Ova
 
Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia Profesa Adolf Mkenda ameitaka Taasisi ya Teknolojia Dar es Salaam (DIT) kujitanua zaidi kwa kutengeneza vipuri vya vyombo vya moto ikiwemo vya bajaji na pikipiki.

Ameyasema hayo Januari 28, 2022 Jijini Dar es Salaam wakati alipotembelea Taasisi hiyo ili kujionea shughuli mbalimbali zinazofanywa hapo ambapo amesema tunaweza kukua kiteknolojia kwa kuboresha vitu ambavyo tayari vimeshatengenezwa na nchi nyingine.

"Nimefurahi sana kuona mna kampuni inayosaidia kubiasharisha bidhaa za ubunifu ila niwatake mboreshe kwa kutengeneza vipuri ambavyo vinahitajika sana kama vya bajaji na pikipiki," amesema Prof. Mkenda.

Aidha Waziri Mkenda ameipongeza taasisi hiyo kwa kuwa na kampuni inayosaidia kubiasharisha bunifu mbalimbali na kuwataka DIT kuhamisha ujuzi wa kiteknolojia kutoka nchi nyingine na kuja kuutumia hapa nchini katika uzalishaji wa bidhaa zitakazokidhi mahitaji ya jamii.

"Tunaweza tukaleta nchini kitu ambacho kimezalishwa mfano nchi ya Uturuki kisha tukaangalia uwezekano wa kukitengeneza na kukiuza ndani na nje ya nchi ili kukuza uchumi wetu," amesema Prof. Mkenda.

Katika hatua nyingine Waziri Mkenda ameusisitiza uongozi wa DIT kuendelea kujenga na kukuza ushirikiano na taasisi nyingine hasa za nje ya nchi ili kubadilishana wataalamu watakaosaidia kuendelea kukuza teknolojia nchini.

Kwa upande wake Mkuu wa Taasisi hiyo, Prof. Preksedis Ndomba amesema wamepokea maelekezo hayo na kuahidi kuyafanyia kazi ili kuboresha utendaji wa taasisi hiyo.

View attachment 2099078View attachment 2099079
Tamko ni zuri lakini Je wamewezeshwa?
 
DIT wanaanda vijana wa kufanya kazi hizo. Sio kazi yao kutengeneza.

Ingekuwa vema DIT watafute wafadhili wa kufanya reseach and development wa ndani na nje pia, halafu wakishaweza kufanikiwa kuwa ba technology nzuri, hao wafadhili ambao lazima wawe wafanyabiashara ndio wawekeze
 
Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia Profesa Adolf Mkenda ameitaka Taasisi ya Teknolojia Dar es Salaam (DIT) kujitanua zaidi kwa kutengeneza vipuri vya vyombo vya moto ikiwemo vya bajaji na pikipiki.

Ameyasema hayo Januari 28, 2022 Jijini Dar es Salaam wakati alipotembelea Taasisi hiyo ili kujionea shughuli mbalimbali zinazofanywa hapo ambapo amesema tunaweza kukua kiteknolojia kwa kuboresha vitu ambavyo tayari vimeshatengenezwa na nchi nyingine.

"Nimefurahi sana kuona mna kampuni inayosaidia kubiasharisha bidhaa za ubunifu ila niwatake mboreshe kwa kutengeneza vipuri ambavyo vinahitajika sana kama vya bajaji na pikipiki," amesema Prof. Mkenda.

Aidha Waziri Mkenda ameipongeza taasisi hiyo kwa kuwa na kampuni inayosaidia kubiasharisha bunifu mbalimbali na kuwataka DIT kuhamisha ujuzi wa kiteknolojia kutoka nchi nyingine na kuja kuutumia hapa nchini katika uzalishaji wa bidhaa zitakazokidhi mahitaji ya jamii.

"Tunaweza tukaleta nchini kitu ambacho kimezalishwa mfano nchi ya Uturuki kisha tukaangalia uwezekano wa kukitengeneza na kukiuza ndani na nje ya nchi ili kukuza uchumi wetu," amesema Prof. Mkenda.

Katika hatua nyingine Waziri Mkenda ameusisitiza uongozi wa DIT kuendelea kujenga na kukuza ushirikiano na taasisi nyingine hasa za nje ya nchi ili kubadilishana wataalamu watakaosaidia kuendelea kukuza teknolojia nchini.

Kwa upande wake Mkuu wa Taasisi hiyo, Prof. Preksedis Ndomba amesema wamepokea maelekezo hayo na kuahidi kuyafanyia kazi ili kuboresha utendaji wa taasisi hiyo.

View attachment 2099078View attachment 2099079
Inawezekana, Mhimbili KWa kushirikisha na MOJA ya chuo pale mbeya wanaendelea tengeneza vijana katika fani ya kukarabati vifaa vya mahospitali, ikiwemoa,MRI,CT SCAN ,X RAY N.K,

JUZI nikaambiwa kwamba lengo la mwendazake kununua ndege bado lipo lengo la kuzalisha maarubani pitia chuo Cha usafirishaji, na wanajenga chuo kikubwa Sana KINGINE Dodoma maeneo ya Msalato,
Sijawahi mpenda mwendazake, lakin speed yake WENDA ilikua kubwa Sana,
Tatizo alikua anadanganya kwamba pesa ni za ndani kumbe anakopa,na katuachia jumba bovu
 
Sidhani kama dhumuni la kuanzisha chuo ni kuja kuwa kiwanda, huku ni kuchanganya siasa kwenye taaluma za watu. Sioni kama DIT wanauwezo wa kinyenzo, eneo na nguvu kazi kuanzisha kiwanda cha vipuri vya kuhudumia taifa zima.
Kama kweli Waziri anania ya kuanza kuvuna ujuzi na taaluma ya chuo hicho basi angewapa kazi inayoweza kufanyika na si kutoa tamko la kuitwisha taasisi hiyo mzigo wa kazi ambayo si yake na haiwezi kuitekeleza kwa namna yeyote ile.

Njia pekee ya kuvuna ujuzi na taaluma za wataalamu ni kuainisha mahitaji ya taifa ya kitekinolojia na kujua vipuri muhimu tunavyo vihitaji kwenye maeneo ya tekinolojia tuliyo yaainisha. Tuwape jukumu hilo waatalamu wa vyuo vya kitekinolojia na ufundi wafanye tafiti, na Serikali inapaswa kufadhiri tafiti na project za wafunzi waliojikita kwenye maeneo tuliyo yaainisha.

Hatuhitaji watu hawa watengeneze kipuri chochote, bali tunataka waunde prototype models na kuchora mechanical blueprints au electronic schematic diagrams zenye ufumbuzi wa matatizo tunayotaka kutatua kwenye lugha rahisi zenye kueleweka kwa makundi ya wasomi na mfundi wenye elimu ya kati.

Taasisi kama SIDO kwa kushirikiana na wadau wenye viwanda vidogo pamoja na makundi ya mafundi, wazifanye blueprints hizo kuwa vipuri na vifaa tunavyo vihitaji kama taifa.
Huu unaweza kuwa mchakato unaowezekana, lakini swala la kuitaka DIT kuanza kutengeneza vipuri ni UTOPIAN na sikutegemea lingetolewa na msomi kama Prof. Mkenda
 
Back
Top Bottom