Waziri Mkenda awataka DIT waanze kutengeneza vipuri vya vyombo vya moto ikiwemo vya bajaji na pikipiki

Sote tukiwa wauzaji nani watanunua?
Halafu inabidi wawaambie waache kwanza kuimba na kufundishana nyimbo za dini mida ya usiku pale gorofani kwenye jengo la mwisho
Wa base kwenye huo Urundi sio kutuchanganyia mambo
 
hili sio wala la DIT, hii production mentality inapaswa kuwa ya watanzania woote..

Kwanza kabisa Serikali ianze kuchimba kile chuma mchuchuma na kuanza kukiprocess hapa, Copper pia ichimbwe na kuprocessiwa nk..

Vijana wengi tunasema hawana ajira wako uraiani wakati veta zipo, Kambi za jeshi zipo, JKT ipo, Engineers wapo nk..

Serikali iwekeze pande hizo, mitambo inunuliwe, production zifanyike... Jeshi limiliki mashamba makuubwa ya kilimo, liajiri vijana weeengi darasa la saba, form four, form six, liwele irrigations scheme vijana wakapige kazi huko kuendesha matractor, mitambo, nk Kifupi jeshi letu linaswa kuwa na askari wengi balaa wakijilipa mishahara wenyewe...

Engineers kwenye fani za Electornics na computer, electric engineering, Electromechanical, mining, Mechanical, na watu wa agriculture wapewe mikopo nafuu inayowaelekeza kwenye production chini ya usimamizi wa mamlaka, watu hawa watatoa ajira nyingi sana..

Vipuri vingi kuchonga, unahitaji lathe machines, milling machines, shaping machines, foundry, chuma...

Angalizo: huwezi kufanya mass production ya spare parts kwa kutegemea chuma cha kuagiza au raw materials za kuagiza...India, China, Malysia nk wametoboa kutokana na urahisi wa upatikanaji wa chuma... ukitegemea raw materials za kuagiza lazima product yako price iwe juu na matokeo ni kufail sokoni...
 
Maprofesa wetu kazi kweli kweli. Wamesikia chuo gani kinatengeneza vipuri? Badala ya watu kufanya tafiti ambazo zitawasaidia watu kuanzisha viwanda vya kutengeneza vitu vya maana anataka vyuo vigeuke viwanda vya kutengeza vitu ambavyo tayari vina patent. Na anatoa maelekezo bila feasibility study! Na Profesa mwenzake anapokea maelekezo!

Kama wanataka vipuri ni bora kushawishi wanaovitengeneza kufungua viwanda nchini kwa sababu kuna soko na mazingira rafiki. Vyuo vibakie kuwa sehemu ya kufundisha na utafiti.

Amandla....
 
Kwamba prof ajui namna, na utaratibu wa kuwekeza kwenye industrial mpaka hanatoa tamko za ovyo ivyo....
DIT Ni taasisi changa sana hawana budgets ya kutosha kuwekeza kwenye uzalishaji wa materials.... kwanza material gafi wanatoa wapi...
 
Mimi naiuliza serkali kwa nn wameruhusu utengenezaji wa mifuko ya plastiki( Rambo), mifuko imejaa madukani
 
Kiufupi ameongea siasa, ila safari ni ndefu na siku wakiwa na dhamira ya dhati watenge pesa ya kutosha pengine itawezekana. Ukitembelea vyuo vyetu vya sayansi na teknologia utaamini bado safari ni ndefu, wanatengeneza vibuyu chirizi, mashine za kukoboa karanga n.k, na bado quality yake ni ngumu kushindana sokoni
 
👇
Pamoja na hilo Muhitimu nimekuwa napata nafasi kupita katika vyuo kadhaa hapa nchini kikiwepo hicho DIT mfano, pale kuna vijana wanabuni vitu vizuri sana na ambavyo kwa hapa nchini is to hard to make it possible sababu bado tupo nyuma kama mdau alivyosema hapo juu.

Kuna mtu hapa kanipinga sijui kwa sababu ya akili zake au huyo prof ni mjomba au mchaga mwenzake but nikitoa mfano mmoja pale DIT kuna binti amebuni mfumo unaoweza kutumika hospitali ambao unawekwa kwenye kitanda cha mgonjwa na kuunganishwa kwenye chumba cha mhudumu wa zamu, endapo hali ya mgonjwa inabadirika gafla wakati mhudumu either daktari au ward attendant yupo pale kwenye chumba/ofisi basi kile kifaa kinapeleka taarifa haraka na daktari au muhumu anawahi kwa mgonjwa husika.

Sasa basi, nakumbuka alikuwepo Naibu waziri fulani siku hiyo (nadhani ni prof kama sijakosea)baada ya kupewa maelezo na yule binti jinsi kinavyofanya kazi, binafsi nilivutiwa sana na kutamani huo mfumo serikali uhuchukue na baada ya kuboreshwa usambazwi kwa hospitali mbalimbali za afya nchini ila yule naibu waziri alisema huo mfumo hauwezekani kwa nchi yetu sababu UTAHARIBIWA au KUFUKUZISHA WATU KAZI sababu jiulize
 
Inawezekana hata tukaunda za kwetu wenyewe...
Unafanya kuagiza tu engine, gearbox na spares nyinginezo...

Hata haya magari tunayoendesha huundwa na vifaa toka sehemu tofauti...
... very funny kwa kweli! Tunashindwa ku-reverse engineer hata kibajaji tukatoka na version yetu! I don't believe; ni utashi tu unakosekana.
 
Sio kazi ya vyuo kutengeneza vifaa vya kushindana kwenye masoko. Kazi hiyo ni ya wenye viwanda na wakina Sido. Umewahi kusikia M.I.T wanatengeneza vifaa vya kuuza kwenye masoko? Wao wanafanya utafiti na kufundisha watu ambao wakiajiriwa Apple na Tesla wanatumia walichojifunza MIT kuboresha bidhaa zao au kutengeneza mpya. Chuo sio kiwanda.

Amandla...
 
Mkuu inatakiwa kwanza utashi,kuna chuo kimmoja cha umma nchini kilinunua CNC machine yaani Computer Numerical Controlled machine ambayo lathe au milling machines zaweza kuchonga vipuri kutumia program za computer .
Lakini cha ajabu wameifunika isipate vumbi tu kwa zaidi ya miaka 6 hawaitumii kabisa.Ila kwenye ukaguzi wa vifaa vya kufundishia inakaguliwa tu.
Toka aondoke Mwalimu Julius K.Nyerere vyuo na taasisi za umma zitoazo elimu ya kiufundi zipo ICU.
Hivi unajifunza welding skills kwa week mmoja eti kubana matumizi, ukimaliza chuo uwasimamie G6 First Class Welders ?
 
Waziri anatakiwa awahimize wafanye kutafiti kwenye vitu ambavyo wanaweza kuviandikisha na kupata patent au trade mark juu yake. Huku kukazana na infantile projects ambazo wenzetu waliisha ziacha zamani hakutatufikisha mbali.

Amandla...
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…