Waziri Mkenda: Kila Mwanafunzi kutumia Komputa yake katika Vyuo vya Ualimu

Waziri Mkenda: Kila Mwanafunzi kutumia Komputa yake katika Vyuo vya Ualimu

Roving Journalist

JF Roving Journalist
Joined
Apr 18, 2017
Posts
3,984
Reaction score
13,760
Waziri wa Elimu, Sanyansi na Teknolojia Prof Adolf Mkenda amesema, katika Vyuo vyote 35 vya Ualimu, Wanafunzi Wanatumia Komputa ambapo Uwiano sasa ni Komputa moja kwa Wanafunzi wawili awali ilikuwa Kumputa moja kwa Wanafunzi 28. Ameyasema hayo tarehe 05 April 2022 Jijini Dar wakati wa Ugawaji vifaa vya tehama vya elimu msingi, wathibiti ubora na Vyuo vya Ualimu.

"Wizara imekwisha gawa vifaa vya TEHAMA ikiwa ni Kompyuta za Mezani (Desktop) 1,120, Kompyuta za mkononi au Kompyuta Mpakato (laptop) 413, na Projekta 186 kwenye vyuo vyote vya Ualimu vya Serikali. Vifaa hivi viligawiwa kwa Vyuo vyote 35 vya Ualimu, ili kusaidia kupunguza uwiano wa matumizi ya kompyuta kwa Wanachuo kutoka Wanachuo 28 kwa Kompyuta 1 (28 :1) hadi kufikia Wanachuo 2 kwa Kompyuta 1 (2 :1) vyuoni. Lengo la usambazaji wa vifaa hivyo ni kuhakikisha kuwa uandaaji wa walimu unakuwa wa kisasa na unaendana na maendeleo ya Sayansi na Teknolojia." kasema Prof. Mkenda.

Waziri Mkenda Leo amezindua ugawaji wa vifaa vya TEHAMA kwa ajili ya taasisi za elimu zikiwemo ofisi za Wathibiti ubora wa shule, Maafisa Elimu Kata na shule za Sekondari. Vifaa vinavyozinduliwa jumla ya kompyuta 3,354 ambapo kati ya hizo Laptop ni 1637 na Deskotop kompyuta ni 1717, printer 12, projector 12 na internet switches 12 vikiwa vimenunuliwa na Serikali pamoja na wadau wa Elimu.

"Kati ya komputa zinazozinduliwa leo, laptop 1337 zinatokana na program Covid Recovery ambao ni mradi wa kuboresha mazingira Salama ya Kujilinda na Maambukizi ya Virus vya CORONA. Komputa hizi zitagawiwa kwa Maafisa Uthibiti ubora na Maafisa Elimu Kata ili kuboresha utendaji kazi wao Komputa Mpakato na TEHAMA zitasaidia Kurahisisha Utendaji wa Kazi; Utunzaji na uchakataji wa Taarifa na Takwimu; zitapunguza gharama ya viandikia kwakuwa taarifa zinaweza kupatikana katika nakala laini. Komputa zitarahisisha Mawasiliano baina ya maaafisa na wadau wa Elimu." Amesema Mkenda

Naye Balozi wa Sweden nchini Tanzania, Balozi Anders Sjoberg amesema Pamoja na maeneo mengine, Nchi yake itaendelea kuunga Mkono na kusaidia jitahada za Serikali ya Tanzania katika kuhakikisha Elimu inakuwa bora ili kwendana na dunia ya Kidijitali.

IMG-20220405-WA0025.jpg
IMG-20220405-WA0012.jpg
IMG-20220405-WA0015.jpg
IMG-20220405-WA0021.jpg
 
Inapendeza!

Wakiajiri walimu 30,000 kwa shule za msingi na 7000 wa sayansi kwa sekondari na wakaleta madawati 400,000 kwa shule za msingi, mzaz hutakvwa na sababu ya kumpeleka mwanao private.
 
Hayo ni rahisi sana kuyafanya tena hata bila sijui kwa ufadhiri wa covid, ni mapato ya ndani tu although upigaji na makongamano ndiyo sababu ya upotevu wa pesa.

Sasa tuingie kwenye walimu hapo hatusikii mkiita media kusema walimu wapya 10000, leo tunawagawa ili waende kwenye vituo vyao vya kazi na pesa ya covid bado ipo mh!.
 
Vyuo vya ualimu ni vya kubadilisha viwe vya ufundi.
Nchi hii ina waalimu walio mtaani zaidi ya laki moja, bado vyuo vikuu vya serikali na binafsi vinamwaga kila mwaka, hakuna uhitaji wa hivyo vyuo vya kati vya serikali kwa sasa
 
Back
Top Bottom