The Watchman
JF-Expert Member
- Nov 7, 2023
- 2,186
- 4,940
Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia, Mhe. Prof. Adolf Mkenda, pamoja na Naibu Waziri, Wanu Hafidh Ameir, wamesisitiza dhamira ya Serikali ya Awamu ya Sita kuendeleza mageuzi makubwa katika sekta ya elimu nchini.
Akizungumza mara baada ya kuwasili katika Ofisi za Wizara tarehe 18 Novemba 2025 jijini Dodoma, Prof. Mkenda amesema Wizara imejipanga kuhakikisha elimu inayotolewa inawawezesha vijana kupata maarifa, stadi stahiki na ujuzi utakaowawezesha kujiajiri na kushindana katika soko la ajira la ndani na nje ya nchi.
Prof. Mkenda ameongeza kuwa Wizara itaendelea kusimamia kikamilifu elimu katika ngazi zote huku ikitoa kipaumbele kwa mafunzo ya amali ili kuongeza ujuzi kwa wanafunzi.
Kwa upande wake, Naibu Waziri Wanu Hafidh Ameir ameahidi kutoa ushirikiano wa karibu katika utekelezaji wa mageuzi hayo, huku akisisitiza umuhimu wa kuendeleza misingi ya ushirikiano, weledi na uwajibikaji ili kufanikisha malengo ya Serikali ya utoaji wa elimu bora kwa wote.