Waziri Mkulo na Hekaya Za Abunuasi - Alisema Tanzania Haitaathirika na Mtikisiko

Allien

JF-Expert Member
Joined
Jul 6, 2008
Posts
5,546
Reaction score
1,861
Source: http://www.ippmedia.com/ipp/nipashe/2009/02/28/132510.html.



Mkulo akihojiwa baada ya Rais kupresent "Economic Stimulus Package" alikibu kuwa Rais kamrahisishia kazi ya kuwakilisha bajeti yake.

Hivi jamani nauliza: wakubwa hawaruhisiwi kuchapwa viboko?

Hii inanikumbusha Hekaya za Abunuasi juu ya mjinga aliyeuziwa ghorofa ya juu kisha Abunuasi akamlalia kwa kumwambia shikilia ghorofa yako mimi nabomaa yangu ya chini

Hivi hawa mawaziri wetu huwa wanafikiria nini kutoa matamko yasiyo na kichwa wala miguu? Wanawachukuliaje Watanzania Hasa? Kila waziri na matamko ya ajabu ajabu. Kama hawawezi kazi si waachie ngazi tu? @#$%^&*!@$^%$^%^

Ukisikiliza Matamko au Kauli ya Maboss Zao JK /MKP ni toafauti na zao:


Listi yao ni kubwa tu . . . .
  • Mkulo
  • Sofia Simba
  • Mkuchika
  • Masha
  • . . . . .
 
Full Story . . .

Wasomi wabeza kauli ya Mkulo



 
Bora mkuu Allien umetukumbusha hiki kituko......! Mkullo alitamka wazi kwamba eti crdit crunch tz haitaathirika nayo.....Ndulu naye akaitikia kwa the same kibwagizo!

Shangaa sasa hata miezi sita haijafika, bosi wao JK anatangaza Stimulus Package.....for what sasa.....mbona wanatuchanganya raia na walipa kodi?
 


Kutokana na utandawazi uchumi wa dunia uko centralized. Kwa maana hakuna uchumi usio tegemea mwingine. Nchi masikini zina tegemea nchi tajiri vise versa. Kwa maana hiyo hata kwa mtu asiye msomi ni rahisi kujua mtikisiko wowote wa kiuchumi duniani uta athiri nchi karibia zote. Mfano tu wa Tanzania ni hii misaada. Sisi kama uchumi unao tegemea misaada hao wenzetu wanao tupa hiyo misaada waki patwa na tatizo la kiuchumi lazima wapunguze kiwango cha pesa wanazo tupa. Mfano mwingine ni waki biashara. Mnunuzi aki pungukiwa na hela ata ounguza kiasi cha pesa anacho toa kwa bidhaa au kupunguza idadi ya matumizi. Muuzazi nae aki kosa wateja biashara ina patwa na matatizo. Sasa sijui Mkulo aliona nini mpaka kuona uchumi wetu uko immune na haya matatizo.
 


Mkuu; ndiyo maana naulizia hawa Wakubwa hawarusiwi kutandikwa viboko? Nashindwa hata la kusema. Ni aibu tu!
 


Mkuu; mimi kwa kweli naingiwa na wasiwasi sana kama kweli nchi yetu itakuja kuendelea. Such a very key and sensitive Minister anaongea PUMBA hivi ni nini hasa tutegemee katika maendeleo ya nchi yetu?
 
Mkuu; mimi kwa kweli naingiwa na wasiwasi sana kama kweli nchi yetu itakuja kuendelea. Such a very key and sensitive Minister anaongea PUMBA hivi ni nini hasa tutegemee katika maendeleo ya nchi yetu?

Unajua mimi ninacho shangaa ni kwamba hili swala lilikua la logic tu haya mimi na wewe tukikaa tunaona kabisa sisi hatuwezi kukwepa hali iliyopo. Lakini pia Waziri wa fedha ata zungumziaje swala kama hilo bila report toka kwa wataalamu?
 
Uchumi auongeleao Mkulo ni wa kuchukua Nyanya toka Ilula kuleta Dar ndizi toka Mbeya ana Moshi kuleta Dar bila kujali kwamba Magari yanatumia vipuri ambavyo havitengenezwi Tanzania pia Mafuta ambayo hayachimbwi wala kuwa processed Tanzania.

Hata hivyo tunashangaa nini?
Huyu Mkulo ni kilaza wa siku zote, mtu wa kufoji vyeti, zaidi alisha shindwa vibaya kuongoza shirika. Kwa ushoga na MH Rais kapewa uwaziri wa fedha, tunategemea nini kutoka kwake zaidi ya Pumba??
Haoni chochote vitu vinamuona kwa sana.
The guy is iddiote, period.

Hata hao wengine wamesoma historia ya shule si shule yenyewe.
Kuna kusoma utafiti wa watu wengine na kuukariri na kugani kwa majigambo hadharani, na kuna kutumia utafiti wa watu wengine kama jiwe la pembeni kujua kiini halisi cha matatizo yanayokukabili.

Mawaziri wetu ni watu wa kuendeleza kawaida na kujificha ndani ya mazoea.
Si wepesi wa kuunganisha mambo na kujiuliza kwa nini,( mswahili siku zote anajua kwa nini ni chanzo cha ugomvi), na siku zote hutafuta sababu za kuhalalisha kushindwa kwao.

Tuna laana.
 
Unajua mimi ninacho shangaa ni kwamba hili swala lilikua la logic tu haya mimi na wewe tukikaa tunaona kabisa sisi hatuwezi kukwepa hali iliyopo. Lakini pia Waziri wa fedha ata zungumziaje swala kama hilo bila report toka kwa wataalamu?

wadanganyika kumbe waambiwe nini?
On a serious note, nadhani hakuwa amepima ramifications za tamko lake kama mwenye dhamana ya Wizara ya Fedha.. he was playing constituency politics kama kwenye tamko lake la DECI and this time alisahau kuwa anaongea na Taifa na siyo jimbo lake la uchaguzi.
 

Tanzania tuna viongozi hawaoni mbali ndiyo maana tupo katika hali tulio nayo sasa.
 

I have come to lower my expectations over our leaders. Uki jipa matumaini sana mwishoni una kuwa disappointed to. JK kaingia kwa shangwe na vigelegele. Maisha bora kwa kila Mtanzania, wapi?! Ajira milioni moja, wapi?! Nguvu mpya, ari mpya na kasi mpya imefanywa na mafisadi.
 
Hao viongozi hata vitovu vyao hawavioni ndio itakuwa yatakayojiri kesho katika nchi?

Not suprised and will not!
 
Nimeamini kuwa Tanzania tuna clowns for Mawaziri
 
Mkulo alisema kweli tu. Maisha ya Mtanzania wa kawaida ni yaleyale ya kuzidi kuzama kwenye lindi la umasikini wa kutupa kila kukicha. Subirini muone hizo stimulus packages zitakakoelekezwa na watakaofaidika nazo. Mmewabana huku kwenye ufisadi sasa wamepata mwanya mwingine mzuri tu.
 
Mkulo Bwana . . . . We achaaaa tuuuuuuuu . . . .

Sofia Simba . . . . Mtajiju. . . .

Masha . . . . 7 days alete ushahidi

Mkuchika . . . Nawafungia kwa sheria . . . analeta ubaguzi wa rangi . . .

Polepole ndo mwendo. Tutafika.
 
Mimi nadhani ni Abunwasi!


Mkuu; mimi naona sawa tu Jamaa aitwe Abunuasi.

Kama inawezekana ianzishwe thread ya kumbatiza hilo jina. Wadau tutaiunga mkono.

Jamaa anabore big time!
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…