carbohydates
JF-Expert Member
- Oct 13, 2026
- 260
- 607
Waziri Mkuu wa Ethiopia, Abiy Ahmed, amewaweka mawaziri na maafisa wengine wa serikali katika mafunzo ya kijeshi, akisema nidhamu na misingi ya kijeshi vinaweza kusaidia kujenga uongozi imara na kuharakisha maendeleo ya taifa.
Picha zilizochapishwa na Abiy Ahmed kwenye mitandao ya kijamii zinamuonesha akishiriki mazoezi ya kijeshi pamoja na mawaziri, manaibu mawaziri na wakuu wa taasisi mbalimbali za serikali katika Kituo cha Mafunzo ya Kijeshi cha Hurso.
Miongoni mwa viongozi wanaoshiriki mafunzo hayo ni Spika wa Baraza la Shirikisho, Muferiat Kamil, Waziri wa Fedha, Fitsum Assefa, pamoja na Waziri wa Afya, Mekdes Daba.
Hata hivyo, haijafahamika rasmi mafunzo hayo yalianza lini wala yanatarajiwa kudumu kwa muda gani.
Akielezea umuhimu wa mafunzo hayo, Abiy amesema azma ya Ethiopia ya kufikia ustawi wa pamoja inahitaji viongozi wenye afya njema ya mwili, uimara wa maadili na uwezo mkubwa wa kiakili.
Kwa mujibu wa Abiy, kuunganisha misingi hiyo ya kijeshi na maadili ya utumishi wa kiraia kunaweza kusaidia kujenga viongozi wenye uwezo mkubwa wa kutekeleza malengo ya taifa na kusukuma mbele maendeleo ya Ethiopia.
===============
Ethiopian Prime Minister Abiy Ahmed has put cabinet ministers and senior government officials through military training, arguing that military discipline can help develop stronger leadership and advance national development.
Photographs shared by Abiy on social media show him participating in military exercises alongside ministers, deputy ministers and heads of government institutions at the Hurso military training centre.
Among those taking part are Speaker of the House of Federation Muferiat Kamil, Finance Minister Fitsum Assefa and Health Minister Mekdes Daba. It remains unclear when the training started or how long it will last.
Abiy said Ethiopia’s ambition to achieve universal prosperity required leaders who were physically fit, morally strong and intellectually capable.
He cited military institutions as sources of lessons in discipline, patriotism, teamwork, accountability and leadership, arguing that combining military and civilian values could produce leaders capable of achieving national goals.
Soma pia :Makundi 7 ya Waasi yaungana kupindua Serikali ya Abiy Ahmed