Waziri Mkuu aipongeza DAWASA kuchagiza matumizi ya nishati safi

Roving Journalist

JF Roving Journalist
Joined
Apr 18, 2017
Posts
3,984
Reaction score
13,760
Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Kassim Majaliwa (Mb) ameipongeza Mamlaka ya Majisafi na Usafi wa Mazingira Dar es salaaam (DAWASA) kwa kuchagiza agenda ya matumizi ya Nishati safi ya kupikia kupitia utekelezaji wa Mradi wa uchakataji topetaka (Fecal Sludge Treatment Plant) katika Kata ya Somangila Wilayani Kigamboni.

Ameeleza kuwa utekelezaji wa mradi huo utaleta manufaa ya matumizi ya nishati ya kupikia kwa Wananchi na Wakazi wa Wilaya Kigamboni na maeneo jirani.

"Niwatake DAWASA mshirikiane na Sekta binafsi katika kutoa huduma hii ikiwezekana kila Wilaya iwe na mradi kama huu wa mfanano ili Wananchi wetu wapate Nishati safi ya kupikia kama ambavyo Serikali ya awamu ya sita chini ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania , Dkt Samia Suluhu Hassan inasisitiza" alisema Mhe. Majaliwa.

Kaimu Afisa Mtendaji Mkuu DAWASA, Mhandisi Mkama Bwire amesema utekelezaji wa mradi huu umefikia asilimia 88 na ukikamilika utakuwa na uwezo wa kuzalisha nishati safi ya gasi itakayotumika kwa matumizi mbalimbali ikiwemo kupikia majumbani.

DAWASA inatekeleza miradi ya ujenzi wa mitambo ya kisasa ya kuchata topetaka katika maeneo ya Wilaya za Kigamboni (Gezaulole, vijibweni na Golani) na katika Wilaya ya Ubungo (Kisopwa na Vikunai) na Wilaya ya Temeke (Vikunai) yenye thamani ya Shilingi Bilioni 16.
IMG-20241007-WA0049.jpg
IMG-20241007-WA0048.jpg
IMG-20241007-WA0047.jpg
Soma, Pia:
Rais Samia Ameibeba Ajenda ya Nishati Safi ya Kupikia Kimataifa
Naibu Waziri TAMISEMI ahamasisha matumizi ya Nishati safi Kigoma, Agawa Mitungi ya Gesi 200
Waziri Lukuvi aunga mkono matumizi ya nishati safi ya kupikia, atoa mitungi ya gesi kwa vijana
 
AGIZA GESI YA KUPIKIA HAPOHAPO ULIPO USIONDOKE KAA HAPOHAPO MTAANI KWAKO
Gesi zote zipo: Oryx Gas, Taifa Gas, Manjis Gas, O-Gas, Total Gas, Mihan Gas, na Puma Gas: zote zinapatikana hapo
 
Back
Top Bottom