#COVID19 Waziri Mkuu awataka Watanzania kuachana na wapotoshaji na kusikiliza wataalam

beth

JF-Expert Member
Joined
Aug 19, 2012
Posts
3,880
Reaction score
6,368
Waziri Mkuu Kassim Majaliwa ametoa wito kwa Watanzania kuwasikiliza Wataalamu katika suala la Chanjo ya COVID19. Asema ni muhimu kuchanja kwasababu inasaidia kupunguza makali ya Ugonjwa.

Ameeleza, "Hii sio Chanjo ya kwanza, tumechanja Magonjwa mengine. Nawasihi achaneni na wapotoshaji. Watu wanafikiria kila kinachotoka huko ni kibaya"

Ameongeza, toka Ugonjwa ulipoingia Viongozi wa Kitaifa akiwemo Rais Samia walisema watajiridhisha na Wataalamu wameridhia aina za Chanjo zilizochaguliwa ni salama.

Msikilize:

Hata wakati ule mlitakiwa kusikiliza wataalamu, bahati mbaya mkawapuuza na wengine mkawaondoa kabisa ofisini, leo mmegeuka na kufuata njia sahihi.

Sasa mnatakiwa muache tabia ya kushikiwa akili na wakubwa wenu wa kazi, hili liwe fundisho kwenu, masuala ya kitaalamu waachiwe wataalamu, wanasiasa mfunge midomo yenu.
 
Yeye kama waziri mkuu amechukua hatua gani kwa hao wapotoshaji?

Nakumbuka enzi za Marehemu Pombe Majaliwa alisema barakoa kazi yake ni kuziba tu mate 🤣
 
Vyeti vya chanjo tunapataje?
Mumetuchanja lakini vyeti hamutuambii tunapataje?
Mukitupa vyeti watakuja wengi tu
 
Serikali itumie media na wataalamu wa afya ili kuelimisha zaidi kuhusu chanjo. Hawa wanaopinga chanjo wanatumia media kurubuni watu.
Kabisa mkuu tatizo ni uelewa katika jamii na pre conceived information.Serikali itumie media kikamilifu.
 
Tatizo suala limeshikwa na wanasiasa zaidi kuliko wataalamu. Acha wapambane nalo.
 
Serikali itumie media na wataalamu wa afya ili kuelimisha zaidi kuhusu chanjo. Hawa wanaopinga chanjo wanatumia media kurubuni watu.
Watuelimishe nini sisi tunajua chanjo ya korona ni ya majaribio hakuna neno jipya
 
Wasomi wote wanajua ila ni unafiki tu
Kauli yako ya SISI TUNAJUA ndiyo nataka unipe ufafanuzi wewe na nani mnajua? Unatembea na miili ya wenzako hapo ulipo au una mwili wako mwenyewe?
 
Kwani ukwenda shule sisi aimanishi na wewe kama wewe ujui shauri yako
 
Waziri Mkuu Kassim Majaliwa ametoa wito kwa Watanzania kuwasikiliza Wataalamu katika suala la Chanjo ya COVID19. Asema ni muhimu kuchanja kwasababu inasaidia kupunguza makali ya Ugonjwa.

Ameeleza, "Hii sio Chanjo ya kwanza, tumechanja Magonjwa mengine. Nawasihi achaneni na wapotoshaji. Watu wanafikiria kila kinachotoka huko ni kibaya"

Ameongeza, toka Ugonjwa ulipoingia Viongozi wa Kitaifa akiwemo Rais Samia walisema watajiridhisha na Wataalamu wameridhia aina za Chanjo zilizochaguliwa ni salama.

Msikilize:

View attachment 1908883

Ameyasahau ya mwendazake.

😂😂😂!

Hiiiiii bagosha!
 
Waziri mkuu muongo muongo hafai
IMG_20210707_084839_278.jpg
 
Back
Top Bottom