Akizungumza katika mkutano wa hadhara uliofanyika Nyamuswa, mkoani Mara tarehe 3 Oktoba 2026 wakati akiendelea na ziara yake katika Kanda ya Ziwa, Waziri Mkuu Dkt. Mwigulu Nchemba amesisitiza kuwa vitendo vya kujichukulia sheria mkononi vinavunja undugu na kuacha makovu yasiyopona katika jamii.Pia, Dkt. Mwigulu ameeleza kuwa utawala wa sheria ndio msingi mkuu ulioweka amani, utulivu na kuunganisha Watanzania kwa muda mrefu.
"Nchi yetu hii imekuwa nchi ya kipekee kwa muda mrefu kwa sababu ya utawala wa sheria, lazima hili jambo tuendelee kulisisitiza. Na tuendelee kuamini kwamba moja ya kitu ambacho kimetuunganisha kwa muda mrefu Watanzania, kimeweka undugu kwa muda mrefu Watanzania, ni utawala wa sheria"