Waziri Mkuu, ingilia kati suala hili la VETA

Pole sana mkuu
Form za veta huanza kutolewa mwezi wa 8 katika vituo vyote nchi nzima. Bei ya form ni 5000 tu unalipa baada ya kupewa control namba.
Hivo wala hauna shida ya kupiga simu wewe nenda kwenye chuo kilicho jirani yako wambie unataka form ya kujiunga.
Unaweza pia kuchukua form kwenye website ya veta na ukaijaza ukapeleka chuo chochote kilicho jirani na wewe.website ya veta ni
Www.veta.go.tz. karibu sana
 
Kama imeshindikana panda gari nenda mpaka hapo veta utapata majibu MAZURI,Ila PM muache ni kiongozi MKUBWA sana na ana majukumu mazito na makubwa sana wapo watu wengi wakumsaidia chini yake
 
Hizi ni namba rasmi za kutoa huduma kwa wateja?
 
Pamoja na hayo

Veta mnaboa
 
Wewe nae mjinga kweli, si uende kwenye ofisi zao. Na hili sio swala la kushughulikiwa na waziri mkuu. Watu wengine sijui mkoje.
 
Hii tatizo ya simu kutokupatikana au kupokelewa si VETA pekee yake, bali imekithiri karibu ofisi zote za serikali, mashirika na serikali za mitaa. Inashangaza wakati Tanzania tunazindua mfumo wa fibre optic wa mtandao kurahishisha mawasiliano lakini watumiaje wenyewe hawana uelewo na umakini wenyewe.

Ni kawaida sana ukipiga namba zilizotangazwa aidha "haipatikani", "imesitishwa" "imezuiwa" au ilie tu na haipokelewi.

Na hata ikipokelewa kwa bahati finyu sana, mpokeaji hana Telephone Skills zozote za kukuhudumia ipasavyo. Hivyo inakuwa ni waste of time and resources.

Mashirika mengi inayojali mawasiliano ya simu huajiri watu wa simu na kuwapa training ya namna ya kumhudumia mteja kwa simu na huweka standards za huduma.

Ningeshauri sana serikali isiishie kuzindua mitandao tu lakini pia ihakikishe taasisi zake zinatumia mitandao ya simu na internet kwa manufaa ya umma.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…