Waziri Mkuu: Kama Mtu anataka kuhama Ngorongoro, Serikali itamuhudumia

Waziri Mkuu: Kama Mtu anataka kuhama Ngorongoro, Serikali itamuhudumia

Analogia Malenga

JF-Expert Member
Joined
Feb 24, 2012
Posts
5,108
Reaction score
10,191
1645173324166.png

Picha: Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa

Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa amesema suala la idadi ya watu ndani ya Hifadhi ya Ngorongoro ni kubwa, hivyo kama kuna watu watakaotaka kuhama kwa hiyari serikali itawahudumia.

Pia amewataka wakazi wa Ngorongoro wasiwalazimishe watu watu kubaki kwa kuwa Tanzania ni ya wote na mtu anaweza kuishi kokote sio lazima abaki Ngorongoro.

Ameyasema hayo akiongea na viongozi na wananchi wa tarafa ya Ngorongoro kwenye kikao cha ndani kilichofanyika makao makuu ya zamani ya NCAA, wilayani Ngorongoro.

=====

MAJALIWA: TUMEPOKEA KAULI YA WAKAZI WA NGORONGORO

WAZIRI MKUU Kassim Majaliwa amesema Serikali imepokea kauli ya wakazi wa Ngorongoro kwamba wako tayari kupokea maelekezo ya Serikali na kushirikiana pamoja katika kuulinda utalii na uhifadhi wa eneo hilo.

"Kwa kauli yenu kwamba mko tayari kushirikiana na Serikali kuendeleza uhifadhi na kukuza utalii, sisi tumeipokea na tutaitekeleza ahadi yenu''

Mheshimiwa Majaliwa ametoa kauli hiyo leo jioni (Alhamisi, Februari 17, 2022) wakati akizungumza na viongozi na wananchi wa Tarafa ya Ngorongoro kwenye kikao cha ndani kilichofanyika makao makuu ya zamani ya NCAA, wilayani Ngorongoro, mkoani Arusha.

Amesema, kama ambavyo Serikali imetoa nafasi ya kusikiliza maoni ya wananchi wa tarafa hiyo, nao hawana budi kuipa nafasi Serikali kuendelea na mpango wa maboresho wa maeneo ambayo yanatakiwa kufanyiwa uhakiki ili ije na mpango bora wa kuliendeleza eneo hilo.

Amesema atapitia changamoto alizokabidhiwa na Diwani wa Naiseko, Bw. James Moringe na akawataka wakazi hao waendelee kuiamini Serikali yao kwa sababu ina nia njema na wananchi wake.

"Endeleeni kuiamini Serikali yenu kwani ina njema na nyie. Tunahitaji kuona shughuli za ufugaji zikiendelea na utalii ukiendelea. Na kwa maana hiyo, mnakubaliana na Watanzania wanaotaka kuona utalii ukiendelea. Na kwa maana hiyo tufuate misingi ya uhifadhi.”

"Na mnapotoka hapa, kila mmoja wetu akatafakari kuhusu changamoto ya kuongezeka kwa mifugo na idadi ya watu. Muwe watulivu wakati Serikali ikifanyia kazi maoni yenu. Tutapokea pia maoni ya taasisi na asasi za kiraia, nazo pia tutazifanyia kazi," amesisitiza.

Amesema Serikali itaratibu maoni yanayotolewa na pande zote. "Tunapofanya hilo, mahali pote tunaangalia maslahi ya Taifa. Wana-Ngorongoro endeleeni kuiamini Serikali yenu, endeleeni kumuamini Rais wetu Mheshimiwa Samia Suluhu na endeleeni kuamini miongozo inayotolewa kwani ina tija kwenu."

"Wakati wote Mheshimiwa Rais amesema anawapenda Watanzania wake na ni kweli anatupenda sana. Yeye ndiye mtumishi nambari moja na sisi ni wasaidizi wake na ni lazima tufuate philosophy yake ambayo anataka kuona Watanzania wanasikilizwa na wanashauriwa."

Waziri Mkuu amesema muendelezo wa vikao anavyofanya katika wilaya ya Ngorongoro ni utekelezaji wa maelekezo ya Mheshimiwa Rais Samia Suluhu Hassan ya kuwataka viongozi wakutane na wakazi hao na kuwasikiliza maoni yao.

Mkutano huo pia umehudhuriwa na Waziri wa Maliasili na Utalii, Mifugo na Uvuvi, TAMISEMI, Naibu Waziri wa Ardhi, Makatibu Wakuu wa wizara za Maji na TAMISEMI na viongozi wa Chama cha Mapinduzi (CCM) na viongozi wa dini.

Wadau walioshiriki kikao ni Mbunge wa Ngorongoro, Malaigwanan, Wenyeviti wa vijiji na Vitongoji, Baraza la Wafugaji la Ngorongoro, viongozi.
 
Habari!

Pendekezo: Serikali iweke dau maalumu kwa familia iliyo tayari kuhama katika hifadhi ya Ngorongoro kwenda nje ya hifadhi.

Itaje kiasi cha fedha watakachotoa kwa familia iliyo tayari kuhama katika hifadhi ya Ngorongoro. Hapa ninaamini watawapata watu wengi tu, na watakaobaki katika hifadhi wataendelea na uhifadhi mseto.

Isizungukezunguke kama mwanaume anamtongoza binti.

Iseme ni kiasi gani Cha fedha wataipa familia husika, au iseme itajenga nyumba zenye thamani fulani mahali ambapo familia itapendekeza.

Kama Wamasai wa Ngorongoro wanatumiwa na matajiri kufuga ng'ombe wao katika hifadhi ya Ngorongoro hapo itajulikana, kama ni ubishi tu wa asili itajulikana.

Wakigoma, serikali ipendekeze mahali, hata Lindi , Kigoma, Simiyu, Pwani, Mtwara , Singida, Tabora n.k, ijenge nyumba sare na kuwatengea maeneo ya kufugia wapelekwe kwa magari ya jeshi.

Sasa sio muda wa kumembelezana
 
Kwamba Serikali isizunguke kama Mwanaume Anamutongoza demu.
 
Ni wazo zuri sana huwezi kumbia mtu hahame mahali pasipo kuweka mzigo mezani.
Nilimsikia Majaliwa anasema aliye tayari kuhama aseme serikali itamsapoti .
Itamsapoti kwa kiwango gani na itamsapoti kitu gani?
Hatoa jibu
 
Jamii zingine zinatandikwa na zinasagwa nje ya hifadhi ila hawa unataka waombwe na walipwe. Naunga mkono waliosema kanywe kwanza chai ndio uje hapa..
 
Kwa serikali zetu hizi zinazoabudu ubabe, hakuna shilingi itatoka. Na hata ikipitishwa hiyo budget ya kulipa watu waondoke ama wajengewe nyumba, ni asilimia ndogo sana ya fungu hilo litawafikia walengwa. Zote zitaishia kwa hao wapitishaji budget.
Mwisho wa siku hii vita ni ya wenye nacho, maskini na wenye madaraka na muhanga wa mwisho ni yule fukara wa kimasai asie na mbele wala nyuma aliyekuwa akitumiwa na mwenye nacho kumfugia ng'ombe wake.
 
Kwa serikali zetu hizi zinazoabudu ubabe, hakuna shilingi itatoka. Na hata ikipitishwa hiyo budget ya kulipa watu waondoke, ni asilimia ndogo sana ya fungu hilo litawafikia walengwa. Zote zitaishia kwa hao wapitishaji budget.
Mwisho wa siku hii vita ni ya wenye nacho, maskini na wenye madaraka na muhanga wa mwisho ni yule fukara wa kimasai asie na mbele wala nyuma aliyekuwa akitumiwa na mwenye nacho kumfugia ng'ombe wake.
Wawajengee nyumba za gharama za chini na kuwapa mashamba kwaajili ya kufungia na kulima.
Mapori yako mengi. Ningezunguka tz, Sehemu kubwa ya nchi hii ni pori.
 
Wawajengee nyumba za gharama za chini na kuwapa mashamba kwaajili ya kufungia na kulima.
Mapori yako mengi. Ningezunguka tz, Sehemu kubwa ya nchi hii ni pori.
Unaongea kama hauna kichwa vile. Hayo umewahi kuona wapi yakifanyika nchi hii?
Nimeamini watanzania wengi Wana matatizo ya akili, wewe ni mmoja wao
 
Wapigwe mpka wapewe masharti ya kutozaliana, wasimiliki zaid ya ekari 5, mifugo ilipiwe kodi ili kutunza mqzingira
 
natafakari vikao vya wamasai vinavyoendelea "underground"....nawafahamu fika walivyo jeuri kwenye suala la ardhi....hofu yangu maeneo watakayopelekwa kusiwe na wakulima......bomu lingine linakuja.......sipendekezi walipwe kabisa....ila ni wapi watapelekwa...hata kama sio wote,,, au hata kama wataondelewa kidogo..........hapa PM Majaliwa asitumie mihemko.....hekima na busara ya hali ya juu......ila lazima waondoke.....
 
Back
Top Bottom