Waziri Mkuu Kasimu Majaliwa, hata wakisoma VETA Baada ya kuhitimu wanahitaji aidha mtaji au waajiriwe


Hawawezi kukubali kuondoka meza Kuu
 
Sio haohao waliwaambia wasome kwani Elimu ni ufunguo WA maisha?
Dunia imebadilika uwezo wa kuwaajiri haupo ndio maana kazi ya watu 300 wanaomba 10000 hivo Bora watu waelezwe hata kama wataumia lakini ndio ukweli kijana anamaliza chuo miaka 5 hadi 10 anaomba Tu ajira lazima wajiongeze kupata ujuzi wa stadi za maisha
 
Umenena vyema mkuu, lakini utakuta huyu PM na akili yake ndogo na viunga wenzake wa CCM wanataka wapewe Tena kuongoza nchi. Kwanini msiwaachie wengine tuone kama matatizo mliyoyatengeneza mbwa ninyi CCM tuone kama kweli suluhisho ni Kwa wasio na ajira hasa hasa degree holders waende wakasome VETA regardless Wana Bachelor degree za electrical engineering, mechanical engineering. Halafu huko kwako linapitaga bila kupingwa,
 
1.Kwa Sasa mafundi ni wengi au wachache? Na Je wameajiriwa au wamejiajiri? Au umewahi sikia kazi za ufundi hazipo?

2.Tangu lini kazi za Ujenzi au uundaji au maintenance zikaisha Duniani? Mfano Canada inasema ndani ya miaka 5 ijayo italazimika ku import hasa kwenye sekta hizo za ujenzi, uzalishaji na madereva maana hata Sasa wanakabiliwa na Upungufu wa Nguvu kazi.

3.Uchumi wa Nchi yetu na Nchi zingine unajua hizo kazi Huwa haziishagi lakini pia hao wahitimu wa VETA ni rahisi kufanya ubunifu wa kujiajiri kuliko wale mliosomea maelezo meengi huko Chuo Kikuu.

5.Ieleweke vyema kwamba sio lengo la Serikali kumaliza unemployment 100% maana jambo Hilo haliwezekani practically and theories za Labor economics zinakataa.Serikali inalenga kuondoa tatizo la Ajira Kwa viwango vinavyokubalika kiuchumi.

6.Mwisho kwani huko Kwa wenye hizo kampuni sijui wanaovamia hakuna shida ya unemployment? Mfano China, Egypt,USA nk? So hio sio suluhisho na Wala hakuna namna ukifanya hivyo ndio utaondoa unemployment.
 
Sioni hoja ya watu kurudi VETA zaidi ya kuboresha Vyuo vikuu vidiri na Vitendo zaidi kama MUST. DIT viboleshewe mazingira
 


Kujiajiri ni suala la FIKIRA za mtu tangu akiwa Mdogo, hivyo anaanza kujenga mifumo ya kujiajiri NDANI yake katika hatua zote za ukuaji wake na wakati sahihi ukifika kile kilichojengenga NDANI kinajidhihilisha katika vitendo


Capital Sio tatizo kwa wanahitaji kujiajiri tatizo ni mipango na mikakati thabiti ya kufikia malengo ambayo MTU amejiwekea i.e FIKIRA
 
Ni kitambo toka BILL GATES aishauri Afrika iwekeze vyema katika elimu ya kati na vyuo vya ufundi....I concur with him that we should reduce enrollment of universities beneficieries especially on cutting down the number of students per faculties ,na hapa TCU iache kutoa ITHIBATI kwa vyuo vikuu vichipukao kila uchao......

#JMT milele dumu !!
 
Nitatoa maoni yangu siku si nyingi juu ya suala hilo na maoni ya watu mitaani. Ila kwa sasa nipo Bize sana na Ziara ya Mheshimiwa Stephen Wasira Makamu Mwenyeki wetu CCM Taifa ambaye yupo mkoani Songwe kwa ziara ya siku tatu.
 
Wanachuo 😂

Your browser is not able to display this video.
 

Wakimaliza VETA nani atawapa mitaji?

Vipi mazingira ya Kodi.
Vipi ushindani wa kimataifa utadhibitiwaje?
 

Biashara ni Capital Mkuu.
Kama wewe ni mfanyabiashara Hilo lipo wazi.

Wangapi wanafikra za kujiajiri na hawajajiajiri Kisa Mitaji?
 
Lakini sijaona ubaya wa waziri mkuu ulipo swala la ajira ni la dunia nzima kinacho mata hapa wewe nenda veta kapate ujuzi kama ni makenika piga ufundi wako huku ukiendelea kufukuzia kazi ya degree yako

Kwamba watu waende VETA ndio watapata Mitaji ya kujiajiri?
 
Hao waliomaliza DIT na MUST mtaani wanafanya nini?
Wanasubiri ajira na ajira wamezikalia hawataki kutoa na wanaotakiwa kustaafu hawataki kustaafu km akina Wasira miaka 80+ bado wanakomaa kufanya kazi za Vijana
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…