Waziri Mkuu Kassim Majaliwa aagiza kusimamishwa kazi kwa maafisa wa Halmashauri ya Kilolo kwa Tuhuma za Matumizi Mabaya ya Fedha za Umma

Waziri Mkuu Kassim Majaliwa aagiza kusimamishwa kazi kwa maafisa wa Halmashauri ya Kilolo kwa Tuhuma za Matumizi Mabaya ya Fedha za Umma

Mangi Meno

JF-Expert Member
Joined
Jun 26, 2024
Posts
292
Reaction score
895
IRINGA - Waziri Mkuu Kassim Majaliwa ameagiza kusimamishwa kazi mara moja kwa Mhandisi wa Halmashauri ya Wilaya ya Kilolo, Emanuel Sigachuma, na Ofisa Elimu Sekondari wa halmashauri hiyo, Nelson Milanzi, ili kupisha uchunguzi wa tuhuma zinazowakabili na kuwafikisha mahakamani. Wawili hao, pamoja na Mkurugenzi wa halmashauri hiyo mstaafu, Laini Kamendu, wanatuhumiwa kushindwa kutekeleza wajibu wao na kusababisha kuwepo kwa mashaka ya matumizi ya zaidi ya Sh Milioni 700 za ujenzi wa bwalo la Shule Mpya ya Sekondari ya Wasichana ya Mkoa wa Iringa ya Lugalo.

Kiasi hicho cha fedha ni sehemu ya zaidi ya Sh Bilioni Tatu zilizotolewa na serikali kupitia mpango wa Rais Samia Suluhu Hassan wa kujenga shule moja ya sekondari ya wasichana katika kila mkoa.

Akitoa taarifa ya ujenzi wa shule hiyo inayojengwa katika Kata ya Mbigili wilayani Kilolo, na ambayo imeanza kupokea wanafunzi wa kidato cha tano mwaka huu, mhandisi wa halmashauri hiyo alisema ujenzi wa bwalo hilo, ambao umefikia zaidi ya asilimia 40, umegharimu zaidi ya Sh Milioni 300.

Alipoulizwa zilipo fedha zingine za kukamilisha ujenzi wa bwalo hilo, mhandisi huyo alisema zilitumika kukamilisha miundombinu mingine ya shule hiyo, majibu yaliyomkasirisha Waziri Mkuu na kumfanya aulize tena: “Kwa nini fedha za bwalo zifanye kazi nyingine tofauti na maelekezo ya serikali yanayoonesha kila jengo linatakiwa kujengwa kwa gharama yake?”

Akiuliza zilipo zaidi ya Sh Milioni 400 za ujenzi huo, sababu za bwalo hilo kutokamilika, na wapi wanafunzi wa shule hiyo wanalia chakula; mhandisi huyo alikaa kimya akionekana hana majibu.

Akimuagiza mwanasheria wa serikali kuhakikisha wawili hao wanafikishwa mahakamani, Waziri Mkuu alimtaka Katibu Tawala wa Mkoa wa Iringa kumtafuta popote alipo na kumrejesha Iringa aliyekuwa Mkurugenzi wa Halmashauri hiyo, Kamendu, ili naye aunganishwe katika kesi hiyo.

Aidha, Waziri Mkuu amehoji sababu ya halmashauri hiyo kumlipa mkandarasi fedha zake zote pamoja na kwamba hajakamilisha sehemu ya ujenzi wa jengo la utawala, huku akitaka madawati yote katika shule hiyo yaliyotengenezwa chini ya kiwango, yaondolewe mara moja.

“Leteni roli sasa hivi lije libebe madawati haya, sitaki kuyaona hapa,” alisema.

Nimefanya kazi Kilolo kama DMO, kwa huyo DED Mstaafu. Mungu kajibu maombi yangu.

R.I.P Mzee Shehemba Kuziwa.
 
Imagine hiyo ni sehemu moja tu! Kilolo!! Vipi akikagua maeneo yote yenye hayo majengo ambayo mpaka sasa hayajakamilika kutokana na upigaji!!
 
Fedha za wananchi zinaliwa bila kunawa mikono. Nchi ya amani sana hi!!!!
 
Nchi inapigwa na wanaopiga wapo kama hakuna kinachofanyika. Terrible. Halafu uhalali wa kukusanya kodi unatoka wapi kama kodi zinaishia kuibwa au kuchezewa na wajanja walio kwenye ofisi za umma?
 
Nina mashamba kangi Lulanzi ka parachichi hela hamsini
 
Siasa tu izo ivi kwa halmashauri zetu Unadhani ni Rahisi kula 300m.

Waliopo Huko wanajua palivo nwaambia izo ni Siasa tu
 
Nelson Milanzi kitu gani kilimhamisha Dodoma na Masasi akapelekwa Iringa?
Hapo Millanzi hana hatia kwani huyo DED alikiwa anamtuma asimamie shule nyingine ili yeye na huyo Sigachuma wafanye uhuni.

Mbona nasikia palepale kwenye mkutano PM alibatilisha maamuzi kuhusu Milanzi mkuu. Milanzi hausiki huko tena.
 
Siasa tu izo ivi kwa halmashauri zetu Unadhani ni Rahisi kula 300m.
Waliopo Huko wanajua palivo nwaambia izo ni Siasa tu
Ni kweli haiwezekani ila huyo mstaafu kaumizia sana watu. Leo akina Mukungu, Assey, Mang'una hadi madereva wanakula bia huko walipo.
 
Mkuu usifurahie mwenzio kukutwa na changamoto
Kutoka moyoni, mzee huyo mstaafu kaumiza sana watu hadi kusababisha mauti ya mzee mmoja alikuwa Afisa Kilimo mzee Kuziwa. Inasikitisha sana.

Nimefanya kazi chini yake, sijawahi nyanyasika kama alivyokuwa ananinyanyasa huyo mzee.
 
Asante, sijasema kama anahusika, bali nimehoji tu kufahamu sababu za yeye kuhamishwa kutoka Dodoma -Masasi-Iringa.
Hiko si kitu cha kawaida mkuu kwa mtumishi kuhamishwa.
 
  • Thanks
Reactions: K11
Imagine hiyo ni sehemu moja tu! Kilolo!! Vipi akikagua maeneo yote yenye hayo majengo ambayo mpaka sasa hayajakamilika kutokana na upigaji!!
Usikute shida haiko kwa wasimamazi wala wakandarasi, bali kwa wakaguzi wenyewe.

Kuna haja ya kuunda tume ili ikateue kamati ya kwenda kuandaa kamati fulani ndogo ili kamati hiyo imtafute mkaguzi wa kumkagua huyo mkaguzi.

My point is, wakaguzi wengine ni wasomi vichomi haswa!
 
Back
Top Bottom