Waziri Mkuu Kassim Majaliwa aonya barua za Serikali kusambaa WhatsApp, Instagram

Waziri Mkuu Kassim Majaliwa aonya barua za Serikali kusambaa WhatsApp, Instagram

Huyu aliwahi kutuaminisha kuwa Rais magufuli ni mzima wa afya njema. Hata hii taarifa naichukulia ni ya kawaida tu
 

Waziri Mkuu wa Tanzania, Kassim Majaliwa amesema imeibuka tabia ya barua za ofisi za Serikali kuonekana mitandaoni akitaka taarifa hizo kuwa siri.

Majaliwa ameeleza hayo leo Jumatano Juni 30, 2021 katika mkutano wa mafunzo ya uongozi kwa wakuu wa mikoa na makatibu tawala Tanzania Bara na kubainisha kuwa barua hizo zinaonekana zaidi katika mitandao ya WhatsApp na Instagram.

“Hiyo tabia imeibuka sana kwa miaka ya hivi karibuni tunapotumia mitandao yetu. Kwa hiyo kuna haja ya kudhibiti utandawazi uliopo na matumizi ya mitandao ya kijamii naamini kila mmoja wenu atakuwa makini sana kwenye mada hii,” amesema

Amesema kuwa siri ndio uhai wa Serikali akiwataka watendaji hao pale ambapo itawasilishwa mada kuhusu usiri kwa taarifa za Serikali wawe makini kusikiliza.

Chanzo: Mwananchi
Hiyo no point maana ndo nucluleus ya serikali..big up
 
Ndio siri anayozungumzia hapo. Yeye hakupaswa kueleza Rais amepatwa na nini na haipo kwenye mamlaka yake. Huenda na yeye aliambiwa cha kujibu na taasisi ya Rais. Sasa utamlaumu vipi au kumshusha thamani.
Point sanaa hiyo ndgu.... Serikali Ina Mambo mengi sanaa sio kutoa tu taarifa but preparation pia zahitajika
 
Back
Top Bottom