- Source #1
- View Source #1
- Tunachokijua
- Kassim Majaliwa ni Waziri mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ambaye pia amekuwa Mbunge wa Jimbo la Ruangwa kupitia Chama Cha Mapinduzi (CCM) tangu mwaka 2010. Alihudumu kama Naibu Waziri wa Hali ya Serikali katika Ofisi ya Waziri Mkuu, Idara ya Usimamizi wa Mikoa na Serikali za Mitaa (PMO - RALG) anayehusika na Elimu hadi mwaka 2015.
Madai
Kumekuwepo na taarifa inayosambazwa mtandaoni ikieleza kuwa Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Kassim Majaliwa atafanya mkutano na waandishi wa habari saa 7 Mchana kuhusu hatma yake kisiasa na uchaguzi mkuu 2025
Uhalisia wa taarifa hiyo
Ufuatiliaji wa kimtandao uliofanywa na JamiiCheck kupitia utafutaji wa maneno muhimu umejiridhisha Taarifa hiyo ya Septemba 02, 2025 Si ya kweli kwani haijachapishwa wala kutolewa na ofisi ya waziri mkuu ama Waziri Mkuu mwenyewe kupitia kurasa zake za mitandao ya kijamii kama inavyoonekana katika grafiki hiyo.
Kwa mujibu wa Idara ya Mawasiliano ya Ofisi ya Waziri Mkuu ni kwamba taarifa hii siyo ya kweli na haijatoka kwa Waziri Mkuu Kassim Majaliwa au Ofisi yake na pia hakuna tukio la aina hiyo.