Kennedy
JF-Expert Member
- Dec 28, 2011
- 54,894
- 64,043
Majizi Yamepenya HarakaKaz kaz....
mapigaji yanataka kurudi....
safi sana waziri mkuu
Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
Majizi Yamepenya HarakaKaz kaz....
mapigaji yanataka kurudi....
safi sana waziri mkuu
JPMMiaka 2 iliyopita tangu huo mfumo wa ukataji tiketi ulipokufa Rais alikuwa nani?
Yule dogo si bado ananyea kwenye ndoo au alishachomoka?Kama mtoa huduma bado ni samson group mjue hatuendi popote. Hao watapeli hawawezi kuaminika kutoa huduma nzuri. Kwanza sifa ya mwekezaji hawana wanategemea waibie serikali kwaza ndio wawekeze. Lengo lao kuu ni kupata mali kwa kuiba mali ya umma kujitajirisha. Uwekezaji ni kuleta mtaji na ujuzi sio ubabaishaji mtu huna kitu.
That was a black mark kwa WM.Tokea atudanganye kuhusu Afya ya aliyekuwa Rais Hayati Dkt. Magufuli kuwa yuko Ofisini anachapa Kazi ( na Kaongea nae akiwa kalala ICU kwa Mzena ) wakati kumbe tayari Israeli alishafanya Kazi yake nimeacha Kumuanini japo ni Mwana Simba SC Mwandamizi mwenzangu pia.
That was a black mark kwa WM.
Inabidi aobe radhi kinamna ili asionekane ana kitu cha kuficha.
Otherwise ataaminikaje akiongea mambo azito?
Bus zilizizopo barabarani hata 30 azifiki, hao jamaa uswahili mwingi biashara hawaiwezi,waporwe huo mradi harakaHayo mabasi 100 yanafanya kazi barabara zipi aisee?? Abiria wanajazana kituoni mabasi hayaji halafu mnasema mabasi yaliyo barabarani ni 100,aah wapi? Mwendokasi ubabaishaji ni mkubwa sana, mfumo wa kuonesha tiketi kwenye mashine umekufa zaidi ya miaka 2 sasa na hakuna hatua zinazochukuliwa. Mabasi yanayofanya kazi ni machache na hayo machache madereva wanapaki wanavyotaka..utasikia derava anakunywa chai, mara anapumzika nk
Tungekuwa serious; Nyumbu ilitakiwa iwe ndio supplier and maintainer wa mabasi ya mwendokasi. Tungekuwa tumekuza uchumi wa ndani; ajira kwa watanzania; na kuongeza uwezo wa teknolojia.Mradi wakikaa vibaya unazikwa kabisa maana hadi sasa umekufa.
Hahiwezekani mradi uwe wa gari zile zile tena zimechoka kiasi hicho na ukasema mradi bado upo hai..
Why Shabiby?hawezi kupewa Shabiby
Mtajuaje kuwa wao ni 'watetezi wa wanyonge'. In reality nyuma ya pazia ni waonevu na wala mali za wanyonge.Tunarudi kule kule. Haya mambo si ya kuulizana jukwaani. Angemwita yeye na viongozi wake ili wakae waone tatizo liko wapi. Kama ni uongozi lingeonekana tu. Na kama ni serikali ingeonekana tu maana Meneja angeweza kusema kweli yake bila kuonekana kuwa anamdhalilisha WM hadharani. Inabidi viongozi wakuu wabadilike.
Amandla...
Oh yes well said my friend!!!Tunarudi kule kule. Haya mambo si ya kuulizana jukwaani. Angemwita yeye na viongozi wake ili wakae waone tatizo liko wapi. Kama ni uongozi lingeonekana tu. Na kama ni serikali ingeonekana tu maana Meneja angeweza kusema kweli yake bila kuonekana kuwa anamdhalilisha WM hadharani. Inabidi viongozi wakuu wabadilike.
Amandla...
LEO NIMEPANDA MOJAMradi wakikaa vibaya unazikwa kabisa maana hadi sasa umekufa.
Hahiwezekani mradi uwe wa gari zile zile tena zimechoka kiasi hicho na ukasema mradi bado upo hai.
Gari zimeanza kuwaka sehemu tofauti tofauti.
Zile gari zinatakiwa kuwa-replace kabisa.
Faida kubwa wanasahau gharama za maintenance na replacement ya gari mpya.
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa leo amefanya ziara ya kushtukiza kituo cha mwendokasi eneo la gerezani na kukuta mfumo wa kusoma tiketi haufanyi kazi, mtendaji mkuu alisema mfumo haufanyi kazi baada ya kutokea mgogoro kati ya supplier na alieununua. Meneja huyo amesema mfumo mpya unajengwa na waziri mkuu kumuhoji inatumia miaka mingapi kukamilika?
Majaliwa amesema wanaibiwa mapato kwani wao wanatumia mtambo na wengine wanatumia mtambo mwingine na hawana namna ya ku-check.
Pia Meneja amehojiwa tangu aingie amenunua mabasi mangapi baada ya serikali kununua mabasi 140 huku mabasi yanayokadiriwa kuwa barabarani ni wastani wa 100.
Mtoa huduma ya mwendokasi aliagiza mabasi 70 ambayo yamekwama kuingia barabarani kutokana na mgogoro na waziri mkuu akasema anaenda kuyaona. Majaliwa amesema wananchi wanalalamika mabasi hayatoshi akitolea mfano Kimara watu wanaingilia dirishani na kuhoji mapato wanayokusanya wanapeleka wapi kama wanashindwa kununua mabasi.
Pia waziri mkuu amepita karakana ya Jangwani na sasa anaelekea Ubungo kuangalia mabasi yenye mgogoro
==========
UBUNGO: Kinachoendelea waziri mkuu anauliza hatua zinazoweza kuchukuliwa kwa mabasi yaliyokwama ambapo mtu TRA anasema sheria inamruhusu kamishna kuya-donate au kuyaharibu na waziri mkuu amesema hawezi kupewa Shabiby kwasababu hayamfai kwenda Dodoma kwani ni kwaajili ya barabara za mwendokasi na sasa anauliziwa mwanasheria
Pia waziri mkuu anawaambia forodha waendelee kufanya minada ya mizigo iliyokaa kupita kiasi mara kwa mara ili kusafisha nafasi ya kuagiza mizigo mingine na kuwataka wabadilike kwani baadhi ya wateja wanalalamika process zinachukua muda mrefu
Kassim Majaliwa anasema pesa zilizotumika zimekopwa world bank na zinalipwa na mabasi yameletwa na mjasiriamali laiki ameshindwa ku-comply na sheria na sheria zimechukua mkondo wake tangu 2018 na kutaka kesho wakae waamue
Majaliwa amesema serikali inao uwezo wa kununua mabasi lakini tatizo ni usimamizi na hawawezi kumsimamia msimamizi ambae hawezi na leo amemuweka pembeni mkurugenzi wa fedha na mwingine anamuachia Rais kwani yuko kwenye mamlaka yake.