Waziri Mkuu Kassim Majaliwa avipongeza vilabu vya Yanga na Simba

Ojuolegbha

JF-Expert Member
Joined
Sep 6, 2020
Posts
1,278
Reaction score
797
Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Kassim Majaliwa ameungana na Watanzania kuipongeza klabu ya Yanga kwa hatua ya nusu fainali waliyofikia katika mashindano ya kombe la Shirikisho Barani Afrika (CAF).

Waziri Mkuu Majaliwa amesema hayo Mei 11, 2023 Bungeni jijini Dodoma ikiwa ni utaratibu aliojiwekea katika mikutano ya Bunge kila siku ya Alhamisi kupata wasaa wa kujibu maswali ya Wabunge ya papo kwa papo ili kutoa ufafanuzi wa masuala mbalimbali.

“Hakika Dar Young Afrika inaendelea kupeperusha vyema bendera ya Tanzania, na niwapongeze sana kwa matokeo ya jana, tunawaombea kwa mchezo wa marudiano kule Afrika Kusini mshinde kwa magoli mengi” amesema Waziri Mkuu.

Waziri Mkuu Majaliwa amesisitiza kuwa Watanzania wanahamu ya kuona Tanzania inaingia kwenye mashindano hayo ya CAF kwenye ngazi ya fainali.

Aidha, Waziri Mkuu ameipongeza timu ya Simba kwa hatua iliyofika ambapo amesema anaamini wamejifunza kutoka kwa klabu jirani na hatua waliyofika huku akiamini msimu ujao vilabu viwili au zaidi vifanye vizuri zaidi.

Katika msimu wa 2022/2023 timu za Tanzania za Yanga na Simba zimefanya vizuri kwenye mashindano ya Afrika kwa timu ya Yanga hadi sasa ipo hatua ya nusu fainali Kombe la Shirikisho Barani Africa (CAF) na timu ya Simba ikifikia hatua ya robo fainali ya kombe la Klabu Bingwa Afrika.View attachment 2618423
2.jpg
 
Aliyefika robofainali ya kombe la klabu bingwa akajifunze kwa aliyefika nusufainali ya kombe la shirikisho na huku wote walianzia klabu bingwa lakini mmoja akafuruhushwa na kurudi kwa vilaza wenzake.Haya nayo ni maajabu mengine.
 
Endelezeni ubishi tu kwa sababu mlizaliwa nao. Nyie pamoja na kuwanga mchana kweupe bado mlipigwa tu. Ila kupanga ni kuchagua mjifunze kwa majirani au muendelee kuwa wabishi, ili muendelee Kufa kiume.
 
Na timu ipi lakini? Malumo unawalinganisha na Orando Pirates? Mkuu , Kwa hapa Tz ni sawa na kuwalinganisha Azam na Ruvu shooting .

Ukweli lazima usemwe . Mlikimbia vita ya wanaume wanaopigana kwa bunduki na kurudi vita ya wanawake wanaopigana vita kwa Miko.
 
Nyie kama wanaume kweli mko wapi. Unabakia na misifa isiyoeleweka wakati umeambulia patupu. Huwezi kukilinganisha na timu kubwa wewe wakati hata hilo kombe unaloliita la Luza huna ni makelele tu. Sawa endelezeni kujifananisha na Al Ahly.
 
Kama hao Orlando wangekua Bora wasingeishia kucheza ligi ya ndani na Marumo gallant acheze kimataifa
 
Endelezeni ubishi tu kwa sababu mlizaliwa nao. Nyie pamoja na kuwanga mchana kweupe bado mlipigwa tu. Ila kupanga ni kuchagua mjifunze kwa majirani au muendelee kuwa wabishi, ili muendelee Kufa kiume.
Tujifunze kwa looser maana ni sawa sawa mwanafunzi wa form four akajifunze kwa mtoto wa darasa la 7 kiujumla itakuwa ni unazi wa hali ya juu
 
Nyie kama wanaume kweli mko wapi. Unabakia na misifa isiyoeleweka wakati umeambulia patupu. Huwezi kukilinganisha na timu kubwa wewe wakati hata hilo kombe unaloliita la Luza huna ni makelele tu. Sawa endelezeni kujifananisha na Al Ahly.
Wazee wa kitonga naona mnajipiga vifua kuwepo kwenye mashindano ya looser.
 
Endelezeni ubishi tu kwa sababu mlizaliwa nao. Nyie pamoja na kuwanga mchana kweupe bado mlipigwa tu. Ila kupanga ni kuchagua mjifunze kwa majirani au muendelee kuwa wabishi, ili muendelee Kufa kiume.
Kwani nyie hadi mnafikia hatua ya robo mlijifunza kwa jirani gani?
 
Tumejifunza kwa Simba, na uchungu tumeutoa kwenu kwa hiyo tumejidhatiti kuchukua ubingwa wa Luza. Nyie endeleeni na ushindi wenu wa robo fainali.
Mkiukosa ubingwa wa luza mtakuja na kauli gani?
 
Back
Top Bottom