Waziri Mkuu Majaliwa Kassim Majaliwa, amewataka watanzania wawapuuze Wapotoshaji wa mitandaoni wanaotaka kuleta taharuki juu ya Afya ya Rais Magufuli "Rais ana shughuli nyingi, Wanataka atoke aende wapi, Kariakoo au Magomeni tangu lini?"
Leo asubuhi wakati nakuja huku nimeongea naye kwa simu na ameniagiza niwaambie wana Njombe kuwa anawapenda sana na anawashukuru sana kwa kura nyingi mlizompigia
Kuna wenzetu hawaishi hapa nchini, wao kazi yao ni kutuombea mabaya tu, kupandikiza chuki tu. Sasa unamuombea mwenzako kufa hiyo ni akili kweli? Nawatoa hofu watanzania, Rais wenu yuko imara anafanya kazi zake kama kawaida za ofisini.
Tuhakikishe tunamuabudu Mungu, tunamuomba Mungu katika kila jambo, tunamtegemea Mungu katika kila jambo, hata asubuhi nilivyokuwa natoka Dodoma nimempigia kumjulisha ratiba yangu, hata juzi alikuwa anajua ninakuja akanituma, wasalimie wana Njombe na nilitoa Salamu.
Naomba nirudie, kwa salam alizotupa leo kweli wana Njombe, mheshimiwa Rais anawasalimia sana wana Njombe, mheshimiwa Rais anawashukuru wana Njombe.
Ila kwa uhalisia kama Rais angekuwa katika hali kama hiyo inayosemwa ni dhahiri kungekuwa na taharuki na isingewezekana kamwe kwa waziri Mkuu kuendelea na ziara kama hizo.
Mungu mwepushe na Hilo janga wanalomwombea wabaya wa nchi ili akamilishe mazuri aliyoanza ili Tanzania iwe Kama Amsterdam, Tundu akimbilie uhamishoni huku Tanzania palipokuwa nchi yake ya awali
Au amezinduka kama wanavyosema kuwa ni "kawaida" yake, wapambe sasa wanapata nguvu ya kuja front na kunena jambo juu yake-Wiki nzima hii walikuwa kimya!
Binafsi, anayesema Rais anaumwa na anayesema Rais ni mzima, Kwa kipindi hiki na kipindi chochote, kama hatumwoni hadharani, hawana tofauti ... wote wanazusha tu...