PreGE2025 Waziri Mkuu Kassim Majaliwa: Tanzania imepata Mafanikio Makubwa Katika Miaka 61 ya Muungano"

Mijadala ya Uchaguzi Mkuu wa Tanzania 2025 (Kabla)

Mkalukungone Mwamba

JF-Expert Member
Joined
Aug 29, 2022
Posts
3,141
Reaction score
7,205
Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Kassim Majaliwa amesema Tanzania ni Taifa lililopata mafanikio makubwa katika sekta mbalimbali za maendeleo katika kipindi cha miaka 61 ya Muungano.

Amesema hayo leo (Ijumaa, Aprili 25, 2025) wakati akizungumza na maelfu ya wakazi wa Wilaya ya Ukerewe Mkoani Mwanza katika mkutano wa hadhara uliofanyika kwenye uwanja wa Getrude Mongela.

Mhe. Majaliwa amefanya ziara ya siku moja katika Wilaya ya Ukerewe ikiwa ni sehemu ya maadhimisho ya miaka 61 ya Muungano.

Amesema kuwa Muungano wa Tanzania Bara na Zanzibar umewezesha kujenga Taifa imara na lisiloyumba “Muungano huu umewezesha kuwa na Taifa ambalo limepata mafanikio katika miradi mbalimbali ya maendeleo Bara na Visiwani, Muungano huu ni tunu ambayo kila mmoja anapaswa kuilinda, kuienzi na kuisemea popote.”

Kupata matukio na taarifa zote kwa kila mkoa kuelekea Uchaguzi Mkuu 2025 ingia hapa: Special Thread: Mijadala na Matukio ya Uchaguzi Mikoa yote Tanzania Bara na Zanzibar kuelekea Uchaguzi Mkuu 2025

“Kwenu hapa Ukerewe Serikali ya Awamu ya Sita inayoongozwa na Mheshimiwa Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan mabilioni mengi ya fedha yameletwa kutekeleza miradi mikubwa ya maendeleo katika sekta elimu, afya, maji, mawasiliano na maeneo mengine muhimu. Serikali hii imefanya mabadiliko mengi.”

Kadhalika,Waziri Mkuu alikagua maendeleo ya ujenzi wa mradi wa hospitali ya rufaa ya kibingwa yenye hadhi ya mkoa inayojengwa katika Wilaya ya Ukerewe Mkoani Mwanza.

Screenshot 2025-04-25 194601.png
 
Huyo tumeshamzoea kusema uongo.. Aliwaambia Masheikh huyu tena siku ya Ijumaa Msikitini Mwendazake yuko hai na anawasalamia, wakati tayari alikuwa mortuary..
 
Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Kassim Majaliwa amesema Tanzania ni Taifa lililopata mafanikio makubwa katika sekta mbalimbali za maendeleo katika kipindi cha miaka 61 ya Muungano.

Amesema hayo leo (Ijumaa, Aprili 25, 2025) wakati akizungumza na maelfu ya wakazi wa Wilaya ya Ukerewe Mkoani Mwanza katika mkutano wa hadhara uliofanyika kwenye uwanja wa Getrude Mongela.

Mhe. Majaliwa amefanya ziara ya siku moja katika Wilaya ya Ukerewe ikiwa ni sehemu ya maadhimisho ya miaka 61 ya Muungano.

Amesema kuwa Muungano wa Tanzania Bara na Zanzibar umewezesha kujenga Taifa imara na lisiloyumba “Muungano huu umewezesha kuwa na Taifa ambalo limepata mafanikio katika miradi mbalimbali ya maendeleo Bara na Visiwani, Muungano huu ni tunu ambayo kila mmoja anapaswa kuilinda, kuienzi na kuisemea popote.”

Kupata matukio na taarifa zote kwa kila mkoa kuelekea Uchaguzi Mkuu 2025 ingia hapa: Special Thread: Mijadala na Matukio ya Uchaguzi Mikoa yote Tanzania Bara na Zanzibar kuelekea Uchaguzi Mkuu 2025

“Kwenu hapa Ukerewe Serikali ya Awamu ya Sita inayoongozwa na Mheshimiwa Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan mabilioni mengi ya fedha yameletwa kutekeleza miradi mikubwa ya maendeleo katika sekta elimu, afya, maji, mawasiliano na maeneo mengine muhimu. Serikali hii imefanya mabadiliko mengi.”

Kadhalika,Waziri Mkuu alikagua maendeleo ya ujenzi wa mradi wa hospitali ya rufaa ya kibingwa yenye hadhi ya mkoa inayojengwa katika Wilaya ya Ukerewe Mkoani Mwanza.

View attachment 3315419
Kwani kaacha Uongo huyu mzee?
 
Attachments

  • VID-20250426-WA0026.mp4
    14.7 MB
Back
Top Bottom