Waziri mkuu Kassim Majaliwa: Tutakomesha rushwa ya ngono vyuoni

Kinuju

JF-Expert Member
Joined
Mar 20, 2021
Posts
2,386
Reaction score
5,325
Waziri mkuu Kassim Majaliwa wakati akizungumza kwenye kongamano la kupinga unyanyasaji wa kinjinsia nchini amesema serikali imedhamiria kukomesha rushwa ya ngono vyuoni kwani kwa sasa imekithiri na kuwafanya vijana wa kike wakose uhuru wa kusoma.
Serikali imeamua kuanzisha madawati ya jinsia vyuoni yatakayoshughulikia hali hiyo.

=========

Waziri mkuu, Kassim Majaliwa leo Alhamisi Novemba 25, 2021 amezindua mwongozo wa uanzishwaji wa madawati ya jinsia kwenye vyuo vikuu na vya kati.

Mwongozo huo unalenga kukomesha vitendo vya rushwa ya ngono vinavyoelezwa kushamiri kwenye taasisi za elimu ya juu.

Akizungumza wakati wa uzinduzi wa kampeni ya siku 16 za kupinga ukatili wa kijinsia, Majaliwa amesema nguvu kubwa inatakiwa kuongezwa katika kukabiliana na tatizo hilo linaloathiri vijana wengi wa kike.

Majaliwa amesema vita dhidi ya vitendo vya ukatili wa kijinsia inapaswa kushirikisha watu wote wanaochukia vitendo hivyo.

Amebainisha hatua ya kuanzishwa kwa mwongozo inaweza kuwa mwarobaini wa kumaliza tatizo hilo la unyanyasaji kwa mabinti waliopo vyuoni.

Ameeleza taasisi za elimu ya juu ni maeneo ambayo mara kadhaa Serikali imekuwa ikipata taarifa za uwepo wa vitendo vya ukatili na unyanyasaji wa kijinsia.

“Tunahitaji Watanzania kuthamini maisha ya kila mmoja wetu, tunataka kila Mtanzania awe huru, anayesoma asome kwa uhuru."

“Ninaendelea kusisitiza uanzishwaji wa madawati ya jinsia kwenye vyuo vyote. Hii ni ajenda na ilani ya CCM nasisitiza haki na usawa na kuwalinda Watanzania dhidi ya ukatili wa kijinsia," amesema akitumia fursa hiyo kuwataka wadau wa masuala ya jinsia kutumia siku 16 kujadili upungufu wa sheria ili ziboreshwe.

“Maboresha haya yakiletwa yatafanyiwa kazi kwa haraka yakifika bungeni, tunataka Watanzania wote waishi kwa matumaini makubwa."
 
Watoto wa kike wapo kwenye mazingira magumu hasa wanapo kutana na wasio na maadili ya kazi. Japo wapo mabinti wasio penda kusoma wao ni bata hawa nao ujilengesha kabisa ndiot tatizo sasa
 
Sawa Yuko sahihi ,lakini madawati ya njisia sio suruhu ya hili tatizo,suruhu ya hili Jambo ni kuondoa mamlaka ya wahusika katika ufaulu wa wanafunzi,na kuwe na mtihani mmoja na msimamizi wa huo mtihani awe Baraza la mitihani,

Yaani iwe Kama tunavyofanya huku mashuleni,uwepo wa madawati ya jinsia hata Kama yatakuwa 100 kwa chuo lakini bado ufaulu wa mwanachuo uko mikononi mwa lecturer bado sio siruhu
 
Mabaraza wakiwa na msimamo tutafanikiwa
 
Vipi kuhusiana na Rushwa au hongo ilyofanywa na Rais kumpandisha Jaji cheo kuwa Jaji mkuu kiongoz katikati ya kesi, mbona hamuikemei??

Vip Rushwa waliopewa maaskali porisi kwa kuwapandisha vyeo baada ya kufanikisha zoezi la kuwabambikia Makomandoo na M/kit CHADEMA kesi ya ugaidi , mbona hamuikemei??

Nyani haoni kundule, toeni kibanz kwenye macho yenu Kwanza, hii ndiyo dawa ya Rushwa!!
 
Sawa Yuko sahihi ,lakini madawati ya njisia sio suruhu ya hili tatizo,suruhu ya hili Jambo ni kuondoa mamlaka ya wahusika katika ufaulu wa wanafunzi,na kuwe na mtihani mmoja na msimamizi wa huo mtihani awe Baraza la mitihani,

Yaani iwe Kama tunavyofanya huku mashuleni,uwepo wa madawati ya jinsia hata Kama yatakuwa 100 kwa chuo lakini bado ufaulu wa mwanachuo uko mikononi mwa lecturer bado sio siruhu
Kumbuka kuwa vyuoo vikuu ni taasisi huru ambazo haziingiliwi katika uwendweshaji wake, hvyo wao ndio wanaoanzisha kozi pamoja na mitaala yake.. TCU ipo kwaajili yakuregulate university fees only
 
[emoji120][emoji120][emoji120]
 
Katika vitu ambavyo Majaliwa atakuwa amefanya vya msingi katka taifa hili ni kulisimamia hili na kulifanikisha.
Ataacha alama kubwa ambayo atakumbukwa nayo.
Tatizo hili ni kubwa sana kwa mustakali mzima wa maendeleo ya taifa letu.mana kama nchi tutajinasibu kuwa tumepiga hatua kubwa katika sekta ya elimu kwa kuwa na wasomi wengi kumbe ni vilaza ambao wamepata degree, na doctorate zao kupitia sehemu za siri.
Nchi haiwezi kusonga mbele kwa elimu za namna hii tutaachwa na wenzetu
 
Mzee wa kabobo huyo 😅 toka tamko lake la mwezi March huwa simzingatii sana!

Anazinguaga mno yani 😅
 
Waziri mkuu Kassim Majaliwa wakati akizungumza kwenye kongamano la kupinga unyanyasaji wa kinjinsia nchini amesema serikali imedhamiria kukomesha rushwa ya ngono vyuoni kwani kwa sasa imekithiri na kuwafanya vijana wa kike wakose uhuru wa kusoma.
Serikali imeamua kuanzisha madawati ya jinsia vyuoni yatakayoshughulikia hali hiyo.

=========

Waziri mkuu, Kassim Majaliwa leo Alhamisi Novemba 25, 2021 amezindua mwongozo wa uanzishwaji wa madawati ya jinsia kwenye vyuo vikuu na vya kati.

Mwongozo huo unalenga kukomesha vitendo vya rushwa ya ngono vinavyoelezwa kushamiri kwenye taasisi za elimu ya juu.

Akizungumza wakati wa uzinduzi wa kampeni ya siku 16 za kupinga ukatili wa kijinsia, Majaliwa amesema nguvu kubwa inatakiwa kuongezwa katika kukabiliana na tatizo hilo linaloathiri vijana wengi wa kike.

Majaliwa amesema vita dhidi ya vitendo vya ukatili wa kijinsia inapaswa kushirikisha watu wote wanaochukia vitendo hivyo.

Amebainisha hatua ya kuanzishwa kwa mwongozo inaweza kuwa mwarobaini wa kumaliza tatizo hilo la unyanyasaji kwa mabinti waliopo vyuoni.

Ameeleza taasisi za elimu ya juu ni maeneo ambayo mara kadhaa Serikali imekuwa ikipata taarifa za uwepo wa vitendo vya ukatili na unyanyasaji wa kijinsia.

“Tunahitaji Watanzania kuthamini maisha ya kila mmoja wetu, tunataka kila Mtanzania awe huru, anayesoma asome kwa uhuru."

“Ninaendelea kusisitiza uanzishwaji wa madawati ya jinsia kwenye vyuo vyote. Hii ni ajenda na ilani ya CCM nasisitiza haki na usawa na kuwalinda Watanzania dhidi ya ukatili wa kijinsia," amesema akitumia fursa hiyo kuwataka wadau wa masuala ya jinsia kutumia siku 16 kujadili upungufu wa sheria ili ziboreshwe.

“Maboresha haya yakiletwa yatafanyiwa kazi kwa haraka yakifika bungeni, tunataka Watanzania wote waishi kwa matumaini makubwa."
Tatizo la elimu ya juu, mwalimu huyo huyo anakufundisha, anakutungia mtihani, anausahihisha , anatoa matokeo na mwisho anakupa cheti cha kumaliza chuo kikuu . Huu mfumo ni mbaya na haufai. Otherwise. Wanawake wafundishe wanawake ili kupunguza ngono vyuoni. Tunakoelekea wanaojiuza ndio watakuwa na degree mitaani
 
Mzee wa kabobo huyo [emoji28] toka tamko lake la mwezi March huwa simzingatii sana!

Anazinguaga mno yani [emoji28]
Lile ilikuwa hamna namna ili kushusha presha ya watu mana maneno yalikuwa mengi lolote lingeweza kutokea wakati wao wakiwa bado hawajajipanga.
 
Back
Top Bottom