Waziri Mkuu Kassim Majaliwa ziarani Loliondo na Tanga, leo Juni 23, 2022

Waziri Mkuu Kassim Majaliwa ziarani Loliondo na Tanga, leo Juni 23, 2022

JanguKamaJangu

JF-Expert Member
Joined
Feb 7, 2022
Posts
2,780
Reaction score
6,607


FV7GidQWYAEMcpp.jpg

FV7GidQWYAAx1n3.jpg

Waziri Mkuu Kassim Majaliwa, leo Juni 23, 2022 yupo katika ziara ya siku moja katika Mkoa wa Arusha na Tanga ambapo atashuhudia zoezi la awamu ya Pili ya wananchi takribani 117 kutoka kaya 27 wanaohama kwa hiari yao wenyewe kutoka katika eneo la hifadhi ya Ngorongoro kuelekea Kijiji cha Msomera, Handeni.

Majaliwa pia atakagua Makazi na miundombinu ya huduma kwa wananchi katika Kijiji cha Msomera, Handeni Mkoani Tanga

Pia atakagua alama zilizowekwa kubainisha eneo la hifadhi ya pori tengefu la Loliondo la Kilometa za mraba 1500.
 
Waende sehemu ambazo zinaendelezwa. Utakaaje eneo la wanyama ambalo halina huduma? Mimi ningeenda kabisa hata kama ningepewa chumba kimoja. Msidanganywe kuwa mtakaa hapo Ngorongoro milele, mtaondoka tu, hivyo ni nafuu muondoke sasa hivi ndugu zangu Wamaasai hamtajuta.

Msidanganywe na hao wabunge wenu wenye nyumba za maana Arusha, akina Millya kule Arusha na Mirerani wanakaa kwenye ustaarabu. Ondokeni maporini, hao wabunge wenu wanataka mkae kwenye nyumba za miti halafu vijana wenu wasiende shule baadaye wakawe walinzi kwenye guest houses. Ondokeni Ngorongoro hiyo ni golden chance mkiikosa mtalia
 
Back
Top Bottom