Waende sehemu ambazo zinaendelezwa. Utakaaje eneo la wanyama ambalo halina huduma? Mimi ningeenda kabisa hata kama ningepewa chumba kimoja. Msidanganywe kuwa mtakaa hapo Ngorongoro milele, mtaondoka tu, hivyo ni nafuu muondoke sasa hivi ndugu zangu Wamaasai hamtajuta.
Msidanganywe na hao wabunge wenu wenye nyumba za maana Arusha, akina Millya kule Arusha na Mirerani wanakaa kwenye ustaarabu. Ondokeni maporini, hao wabunge wenu wanataka mkae kwenye nyumba za miti halafu vijana wenu wasiende shule baadaye wakawe walinzi kwenye guest houses. Ondokeni Ngorongoro hiyo ni golden chance mkiikosa mtalia