Pre GE2025 Waziri Mkuu Kassimu Majaliwa ashiriki Tulia Marathon Mkoani Mbeya, watu wamiminika na kufurika kwa wingi

Mijadala ya Uchaguzi Mkuu wa Tanzania 2025 (Kabla, wakati na baada)

Lucas Mwashambwa

JF-Expert Member
Joined
Jul 28, 2022
Posts
28,722
Reaction score
20,610
Ndugu zangu Watanzania,

Mheshimiwa Waziri Mkuu wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania Kassimu Majaliwa leo hii ameshiriki Tulia Marathon Mkoani mbeya. Mbio ambazo zimekuwa zikifanyika kila mwaka chini ya udhamini wa Tulia Trust iliyo chini ya Mheshimiwa Speaker wa bunge la jamuhuri ya muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt Tulia Acksoni Mwansasu Rais wa IPU.

Ambapo mbio hizo kilele chake ilikuwa ni katika uwanja wa kumbukumbu ya Sokoine iliopo ndani ya jiji la mbeya . Ambapo ni mahali hapo patafanyika pia tamasha kubwa sana la kukata na shoka la mziki chini ya wasanii mbalimbali wa kizazi kipya ambao watatumbuiza na Kuitetemesha kwa raha mioyo ya wana mbeya. Ambapo ZUCHU msanii maarufu wa kike hapa nchini na ambaye anaendelea kutamba na vibao vyake mbalimbali ataongoza wasanii wengine mbalimbali ambao wamefurika kwa wingi.

Kwa ajili ya kupiga vibao vikali kwa ajili ya maelfu ya wananchi ambao wamefurika na kumiminika kwa wingi toka mikoa mbalimbali ya nyanda za juu kusini ,ambao wamekesha wakitembea kwa ajili ya kuwahi kushiriki na kushuhudia tukio hilo kubwa.ambapo misururu mirefu ya watu na magari imeshuhudiwa ikielekea uwanja wa Sokoine.

Lakini pia taarifa za kiintelijensia zinaonyesha kuwa wana CHADEMA mkoani Mbeya wamechanganyikiwa sana na kupata presha baada ya kushuhudia maelfu ya watu wakimiminika na kufurika katika tukio hilo,wakati wao CHADEMA walikuwa wanatamani watu wasihudhurie .kwa hakika Dkt Tulia ndio Mbeya yenyewe na Mbeya ni Dkt Tulia. Tulia kalituliza jiji na wana Mbeya kwa ujumla. Ni raha na furaha tupu chini ya ubunge wa dkt Tulia katika jiji la mbeya,tofauti na wakati wa Sugu ambapo watu walijaa msongo wa mawazo na hasira tupu utafikiri wana matatizo fulani kichwani.watu Muda mwingi walikuwa wanatembea wanaongea peke yao mabarabarani.

Kazi iendelee, mama Ametufikia na kuwafikia watanzania kwa utumishi wake uliotukuka wa kugusa maisha ya watanzania wanyonge wasio na Sauti.

Lucas Hebel Mwashambwa.Mama ANATOSHA kuendelea kuliongoza Taifa letu kwa muhula wa pili.
 
Marathon inafaa sana kupunguza unene, vitambi, matumbo, mashavu kuvimba, nyama uzembe na changamoto nyingine za kiafya zitokanazo na ulaji uliopitiliza usio sawa pamoja na kukosa kufanya kazi ngumu.
 
Ni kweli kabisa mbio hizo zina Umuhimu mkubwa sana sana katika suala zima la afya.
 
Kule kwetu Katavi mtu mrefu na mwenye miguu miembamba mithili ya njiti za viberiti kama Tulia huwa tunamuita "mironjo". Kwa hiyo Tulia tunamuita Bi. Mironjo.
 
Tumekuja kumuona zuchu tu hapa akimaliza kuperform tunasepa 😊
 
Ndugu zangu Watanzania,

Mheshimiwa Waziri Mkuu wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania Kassimu Majaliwa leo hii ameshiriki Tulia Marathon Mkoani mbeya. Mbio ambazo zimekuwa zikifanyika kila mwaka chini ya udhamini wa Tulia Trust iliyo chini ya Mheshimiwa Speaker wa bunge la jamuhuri ya muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt Tulia Acksoni Mwansasu Rais wa IPU.

Ambapo mbio hizo kilele chake ilikuwa ni katika uwanja wa kumbukumbu ya Sokoine iliopo ndani ya jiji la mbeya . Ambapo ni mahali hapo patafanyika pia tamasha kubwa sana la kukata na shoka la mziki chini ya wasanii mbalimbali wa kizazi kipya ambao watatumbuiza na Kuitetemesha kwa raha mioyo ya wana mbeya. Ambapo ZUCHU msanii maarufu wa kike hapa nchini na ambaye anaendelea kutamba na vibao vyake mbalimbali ataongoza wasanii wengine mbalimbali ambao wamefurika kwa wingi.

Kwa ajili ya kupiga vibao vikali kwa ajili ya maelfu ya wananchi ambao wamefurika na kumiminika kwa wingi toka mikoa mbalimbali ya nyanda za juu kusini ,ambao wamekesha wakitembea kwa ajili ya kuwahi kushiriki na kushuhudia tukio hilo kubwa.ambapo misururu mirefu ya watu na magari imeshuhudiwa ikielekea uwanja wa Sokoine.

Lakini pia taarifa za kiintelijensia zinaonyesha kuwa wana CHADEMA mkoani Mbeya wamechanganyikiwa sana na kupata presha baada ya kushuhudia maelfu ya watu wakimiminika na kufurika katika tukio hilo,wakati wao CHADEMA walikuwa wanatamani watu wasihudhurie .kwa hakika Dkt Tulia ndio Mbeya yenyewe na Mbeya ni Dkt Tulia. Tulia kalituliza jiji na wana Mbeya kwa ujumla. Ni raha na furaha tupu chini ya ubunge wa dkt Tulia katika jiji la mbeya,tofauti na wakati wa Sugu ambapo watu walijaa msongo wa mawazo na hasira tupu utafikiri wana matatizo fulani kichwani.watu Muda mwingi walikuwa wanatembea wanaongea peke yao mabarabarani.

Kazi iendelee, mama Ametufikia na kuwafikia watanzania kwa utumishi wake uliotukuka wa kugusa maisha ya watanzania wanyonge wasio na Sauti.

Lucas Hebel Mwashambwa.Mama ANATOSHA kuendelea kuliongoza Taifa letu kwa muhula wa pili.
kwa hakika bunge la Tamzania chini ya Dr.Tulia limetulia tuliiiiii :KasugaYeah:

na Tanzania chini ya Dr.Samia Suluhu Hassan imetulia bara-bara na tunasinga vyema:whatBlink:
 
Tumekuja kumuona zuchu tu hapa akimaliza kuperform tunasepa 😊
Kwa hiyo ulitaka mbaki kugawiwa pesa? Mumshukuru sana Mheshimiwa Dkt Tulia Acksoni Mwansasu kwa kumleta ZUCHU mkoani mbeya.hii ndio raha ya kuwa na mbunge anayewapenda watu wake na siyo yule mbunge wa zamani ambaye kazi yake alikuwa hata yeye mwenyewe hazijuwi nini ukimuuliza. Jiji ni lazima lichangamke muda wote.

Niambie ni kiasi gani cha pesa wanakwenda kuvuna waendesha bajaji, bodaboda na daladala? Vipi wauza ndizi,maji,ice cream,biscuit n.k pesa wanazokwenda kupata leo hii? Sasa ni mwana Mbeya yupi mwenye akili Timamu atashindwa kuwahi asubuhi kwenda kumpigia kura ya ndio dkt Tulia Acksoni Mwansasu uchaguzi ujao?
 
Kule kwetu Katavi mtu mrefu na mwenye miguu miembamba mithili ya njiti za viberiti kama Tulia huwa tunamuita "mironjo". Kwa hiyo Tulia tunamuita Bi. Mironjo.
Jitahidi kutumia vyema akili yako unapoandika jambo.
 
Wana Mbeya hawajabubujikwa na Machozi ya furaha?
 
Back
Top Bottom