Waziri Mkuu Kassmu Majaliwa awanyooshea kidole TARURA, awataka kusimamia miradi kwa weledi na uaminifu

Wiki 4 zilizopita nlipita barabara moja kinondoni
Iliwekwa lami nlijua lami imepigwa sehemu kubwa mpaka napochomekea..
Eh kumbe lami imeishia kati tu mtaa wenyewe hawajamaliza,barabara yenyewe haijawekwa mifereji ..
Kuuliza naambiwa kazi imeisha hapo

Ova
 
Hao ndio TARURA
 
Anataka uaminifu gani? Mimi simuamini huyo jamaa toka alivosema jiwe Ni mzima anachapa kazi
 
Ni mara 10 serikali ingerejesha CommWorks kwasababu hawa TARURA wameshindwa kazi, kuna barabara zimechongwa hivi karibuni mjini Morogoro hazikudumu hata wiki mbili zikageuka vumbi afadhali wakati ambapo hazikuwa zimechongwa, na hivi sasa mvua zimenyesha barabara hizo hazipitiki, ukiwauliza wanasema matengenezo yake yasubiri budget ijayo kwasasa wameshamlipa mkandarasi hawana fedha,

Enzi zile Comm Works walikuwa na vifaa vyao wenyewe walikuwa wanapita kutengeneza barabara regularly hapakuwa na ushenzi wanaofanya hawa TARURA
 
Kuna matuta yamechimbwa yamekuwa kero tupu, ni bora yangebakia majani tulikuwa tunapita misimu yote siyo hizo barabara mnazosema mmefungua.

Kama mnataka transparency fungueni ukurasa kwenye website yenu tuwatumie picha za barabara wanazochonga hao wakandarasi wenu muone kama siyo heri kuchonga barabara kwa majembe ya mkono tu
 
TARURA ilianzishwa ki makosa sana, walichukuliwa watumishi wa ovyo ovyo waliozoea rushwa huko halmashauri ndo wakaamishiwa huko TARURA.
Wanaleta miradi ya kuparua barabara lakini badala ya barabara kua ukombozi inabadilika kua kero, mitaro yapo ovyo...vivuko vinavyoingia kwa watu na maduka na sehemu ya wananchi kupatia hudama hazitengenezwi....usimamizi hafifu kwelikweli.

Sijui wanajisikiaje wakiona barabara zao zinakua kero na ovyoovyo wanajisikiaje. Mafundi wanajenga mitaro ovyo ovyo wala wahandisi wa TARURA hawaonekani kabisa.

Ujinga mtupu
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…