the guardian 17
JF-Expert Member
- Aug 15, 2024
- 395
- 570
Kunazidi kuchangamka sasa, ni kama ujumbe umetumwa kwa machalii wa Arusha, Gambo na Makonda
===
Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Kassim Majaliwa, amewataka viongozi wa kisiasa na wa dini kuwa mstari wa mbele katika kuhubiri amani na mshikamano, akisisitiza kuwa migogoro mingi ya kisiasa inatokana na tamaa ya madaraka.
Akizungumza mkoani Arusha, Februari 26, 2025 wakati wa maadhimisho ya Siku ya Maridhiano katika Kituo cha Kimataifa cha Mikutano cha Arusha (AICC), Majaliwa ameeleza kuwa migogoro mingi inayojitokeza katika jamii inachochewa na watu binafsi au vikundi vinavyotafuta madaraka kwa njia zisizo halali.
"Suala la migogoro limezungumzwa sana hapa, tunajua. Na Sheikh Kishki aliwasema sana wanasiasa kwa sababu huko ndiko kuna migogoro mingi. Kila mtu anatamani cheo, wanasahau kuwa cheo kinatolewa na Mwenyezi Mungu," amesema Majaliwa.
Ameongeza kuwa watu wengi wanapotamani nafasi za uongozi, huanza kutumia mbinu zisizofaa, ikiwemo kumchafua au kumhujumu aliyepo madarakani kwa fitna na hata mbinu za kishirikina.
"Badala ya kumwendea Mwenyezi Mungu na kumuomba akupatie nafasi, unamfuata aliyepo madarakani, unamfitini, unampiga vita, unampa shida yeye na familia yake. Lakini je, unapomtengenezea madhara huyo, hiyo nafasi inakuwa yako moja kwa moja? Mwenyezi Mungu amekuhakikishia kuwa ni yako?" amehoji Majaliwa.
Aidha, amesisitiza kuwa amani ya taifa inaweza kuvurugika kwa sababu ya migogoro inayosababishwa na watu wachache wenye tamaa ya madaraka, na hivyo ni jukumu la viongozi wa dini kuyasema haya wazi ili kulinda mshikamano wa kitaifa.
"Amani inatoweka na mtu mmoja mmoja, watu wawili, kikundi, na kundi likiwa kubwa inakuwa shida. Viongozi wa dini tuyaseme haya kwa uwazi ili kuhakikisha tunalinda utulivu wa nchi yetu," amehimiza Waziri Mkuu.
Kupata taarifa na matukio ya kimkoa kuhusu Uchaguzi Serikali za Mitaa ingia hapa: LGE2024 - Special Thread: Orodha ya Mijadala ya Mikoa yote Tanzania Bara inayoshiriki katika Uchaguzi wa Serikali za Mitaa 2024