Waziri Mkuu Majaliwa: Atakeyeonea waandishi wa habari kukiona

Waziri Mkuu Majaliwa: Atakeyeonea waandishi wa habari kukiona

Naomba anaye amini maneno ya huyu Mheshimiwa PM anyooshe kidole tafadhali! 🤭

Hivi amefufuka kutoka wapi huyu PM! Au ameshushwa tu kutoka mbinguni ndani ya hii miezi miwili iliyopita!!!
Huyu Bwana Mkubwa akikwambia kuwa kumepambanzuka nje, huna budi kutoka ujiridhishe kuwa kweli jua limetoka. Tofauti na hapo si wa kumuamini hata chembe. Hakawii kusema kaongea na marehemu na anatusalimia sana.
 
Amesema, "Sio Sera ya Serikali kuonea Waandishi wa Habari. Serikali haitomvumilia mtu yeyote atakayemkwaza Mwandishi wa Habari akiwa katika kazi, na hatua kali zitachukuliwa dhidi yake.

[emoji3064][emoji3064][emoji3064][emoji3064][emoji3064][emoji3064][emoji3064][emoji3064][emoji3064][emoji3064][emoji3064][emoji3064][emoji3064][emoji3064][emoji3064]
 
Huwezi kutoa kauli kama hii wakati sheria za habari ni kandamizi.Yaani anatoa kauli kama hii wakati walishatunga sheria kandamizi dhidi ya waandishi wa habari.
 
Alikuwa wapi kutoa tamko la aina hii wakati wa utawala wa yule mentor wake?
Hata haya anayofanya SHS Hakuyafanya kipindi cha Mwendazake kwani isingewezekana. Ni sawa kwa Waziri mkuu kusimamia msimamo wa bosi aliyepo madarakani.
 
Walikuwa wapi ?, Ila Better late than Never...,
Then again, tunajuaje kama hizo sio Siasa tu na maneno matupu ?
Nadhani kujua uzito wa hayo maneno mpaka tukiona waliookiona kwa kuonea waandishi wa habari ndio tutajua ukweli...

Alaafuuuu..., kwani kuna raia ambaye ni ruksa kuonewa ?
 
Ukifikiria sana unaweza ukadhani huyu ni waziri mkuu mwingine tofauti na yule wa miaka michache nyuma.Ila hili ndio linaonyesha dhahiri kua nchi inahitaji mapinduzi makubwa yakimfumo ili kumfanya kila kiongozi kwa nafasi yake atekeleze majukumu yake kwa uhuru yeye kama yeye badala ya kucheza na upepo wa kiti cha uraisi unavuma kuelekea wapi.
 
Ni kati ya mawaziri wakuu ambao hawana mvuto kabisa wa kiuongozi
Huyu Aliwekwa kimkakati! Ila akili yangu inaniambia huenda na yeye "akastaafu" kabla ya "mitano tena"
 
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa, amesema yoyote atakaye waonea waandishi wa habari wakati wakitimiza majukumu yao watakiona, kwani serikali inawatambua na kuwathamini na isingependa kuona hata siku moja mwandishi anapata tatizo anapotimiza wajibu wake.

===

SERIKALI: HATUTAKUBALI KUONA MWANDISHI WA HABARI ANAONEWA

Waziri Mkuu wa Tanzania, Kassim Majaliwa amesema Serikali haitakubali kuona Mwandishi anapata uonevu popote kutokana na thamani ya mchango wanaotoa katika kuufahamisha Umma, Ameeleza hayo wakati wa Ufunguzi wa Mkutano Mkuu wa Jukwaa la Wahariri Tanzania (TEF) Mkoani Morogoro.

Amesema, "Sio Sera ya Serikali kuonea Waandishi wa Habari. Serikali haitomvumilia mtu yeyote atakayemkwaza Mwandishi wa Habari akiwa katika kazi, na hatua kali zitachukuliwa dhidi yake.

Vilevile, amesema hatua kadhaa zinaendelea ili kuyafungulia Magazeti ya Mawio, Mseto, Tanzania Daima na Mwanahalisi akifafanua yalifungiwa Kisheria na Sheria hizo hizo zitafuata taratibu.
Ni rahisi kwa Ngamia kupenya kwenye tundu la sindano kuliko MwanaCCM kuacha Unafiki.
 
Back
Top Bottom