Toxic Concotion
JF-Expert Member
- Aug 5, 2015
- 5,760
- 20,837
Huyu Bwana Mkubwa akikwambia kuwa kumepambanzuka nje, huna budi kutoka ujiridhishe kuwa kweli jua limetoka. Tofauti na hapo si wa kumuamini hata chembe. Hakawii kusema kaongea na marehemu na anatusalimia sana.Naomba anaye amini maneno ya huyu Mheshimiwa PM anyooshe kidole tafadhali! 🤭
Hivi amefufuka kutoka wapi huyu PM! Au ameshushwa tu kutoka mbinguni ndani ya hii miezi miwili iliyopita!!!
Aah wacha hizo mkuu,Naamini Mh Waziri Mkuu amenukuliwa vibaya.
Asante ndugu mwandishiWaziri Mkuu wa Tanzania, Kassim Majaliwa amesema Serikali haitakubali kuona Mwandishi anapata uonevu popote kutokana na thamani ya mchango wanaotoa katika kuufahamisha Umma...
Hata haya anayofanya SHS Hakuyafanya kipindi cha Mwendazake kwani isingewezekana. Ni sawa kwa Waziri mkuu kusimamia msimamo wa bosi aliyepo madarakani.Alikuwa wapi kutoa tamko la aina hii wakati wa utawala wa yule mentor wake?
Angeenda na majiAlitakiwa kusema haya sikuile iliposikika ile sauti iliyonena "watch it, not to that extent".
Angechanganywa na mashangazi zake!Angeenda na maji
Ni kati ya mawaziri wakuu ambao hawana mvuto kabisa wa kiuongoziAngechanganywa na mashangazi zake!
Huyu Aliwekwa kimkakati! Ila akili yangu inaniambia huenda na yeye "akastaafu" kabla ya "mitano tena"Ni kati ya mawaziri wakuu ambao hawana mvuto kabisa wa kiuongozi
Ni jambo jema!
Amesema sio sera ya serikali ----ukijiongeza =====bali ilikuwa sera za mwendazake kaendanazoAlikuwa wapi kutoa tamko la aina hii wakati wa utawala wa yule mentor wake?
Ni rahisi kwa Ngamia kupenya kwenye tundu la sindano kuliko MwanaCCM kuacha Unafiki.Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa, amesema yoyote atakaye waonea waandishi wa habari wakati wakitimiza majukumu yao watakiona, kwani serikali inawatambua na kuwathamini na isingependa kuona hata siku moja mwandishi anapata tatizo anapotimiza wajibu wake.
===
SERIKALI: HATUTAKUBALI KUONA MWANDISHI WA HABARI ANAONEWA
Waziri Mkuu wa Tanzania, Kassim Majaliwa amesema Serikali haitakubali kuona Mwandishi anapata uonevu popote kutokana na thamani ya mchango wanaotoa katika kuufahamisha Umma, Ameeleza hayo wakati wa Ufunguzi wa Mkutano Mkuu wa Jukwaa la Wahariri Tanzania (TEF) Mkoani Morogoro.
Amesema, "Sio Sera ya Serikali kuonea Waandishi wa Habari. Serikali haitomvumilia mtu yeyote atakayemkwaza Mwandishi wa Habari akiwa katika kazi, na hatua kali zitachukuliwa dhidi yake.
Vilevile, amesema hatua kadhaa zinaendelea ili kuyafungulia Magazeti ya Mawio, Mseto, Tanzania Daima na Mwanahalisi akifafanua yalifungiwa Kisheria na Sheria hizo hizo zitafuata taratibu.